Mafunzo Saba (07) Muhimu Kutoka Kwa Wajasiliamali Saba Waliofanikiwa Kibiashara Kwenye Karne Ya 19


Siku ya leo ninaenda kukuletea masomo saba muhimu kutoka kwa wajasiliamali na wagunduzi bora a karne ya 19. Kutoka kwa watu hawa utaweza kujifunza mengi ambayo unaweza kuchukua hatua.

Ujue ipo hivi rafiki yangu. Kwenye maisha unaweza kuamua kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa au unaweza kuamua kujifunza ambao hawajafanikiwa. ubora wa kujifunza kwa watu waliofanikiwa ni kwamba wanakupa uhalisia ambao wao wamepitia mpaka kuweza kufikia mafanikio na hivyo wewe mwenyewe unakuwa unaona wazi kwamba hapa kuna upenyo wa mimi pia kufanya mambo makubwa.

Ubovu wa kujifunza kutoka kwa watu ambao hawajafanikiwa ni kwamba, na wao wanakuwa wanakushirikisha jinsi ambavyo wao pia walishindwa. Hivyo wanakukatisha tamaa na kukuonesha kwamba haiwezekani. Ebu chukulia mfano kwamba leo hii ukienda kuomba ushauri juu ya biashara kwa mjomba wako ambaye yeye alisoma mpaka chuo kikuu, akaajiriwa na sasa hivi amestaafu ila fedha yote ya mafao tayari ameitumia imeisha. Unadhani utapokea ushauri gani kutoka kwa mjomba wako huyu? Bila shaka kitu kikubwa ambacho utaambiwa ni kwamba huwezi kuwa mjasiliamali. Atakwambia katafute ajira sehemu fulani na kisha ufanye kazi miaka 30 baadae utastaafu kama yeye.

 

Na mara nyingi ushauri wa watu kama hawa huwa unasikilizwa sana kuliko ushauri wa watu ambao wamefanikiwa. Mtu anakuwa tayari kusikiliza ushauri wa mjomba ambaye hakuwahi kuanzisha hata biashara ya mtaji wa elfu kumi, kuliko kumsikiliza bilionea aliyeanza na mtaji wa elfu kumi na kuufikia ubilionea.

Ndio hayohayo unakuta kwamba kwenye familia karibia watu wote wamesomea fani ile ile. Kwa sababu mjomba alikuwa mwanajeshi, basi wote wanafuata mkondo ule ule maana wanajua kwamba huko ndiko kuna dedha.

 

Ili kukuepusha na janga hili rafiki yangu, siku ya leo nimekuletea masomo saba kutoka kwa wajasiliamali na wagunduzi wa karne 19 ambao walikuwa wamefanikiwa sana. Kabla sijakupa mafunzo haya ningependa nikwambie kitu kimoja muhimu sana. kitu hiki ni kwamba, miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo, ispokuwa kwa vitu viwili. Vitabu ambavyo unasoma na watu ambao unakutana nao. Sasa mimi leo hii nimeamua nikutanishe na watu saba ambao walikuwa wamefanikiwa kwenye biashara na ugunduzi kwenya karne ya 21. Unaweza ukawa unajiuliza, huyu mtu anaweza kunikutanisha na watu waliokufa kwa zaidi ya karne sasa. iko hivi, vitabu vinaweza kukutanisha na mtu yeyote ambaye unataka hata kama yuko mbali kiasi gani. Sasa kwa maneno hayo bila kuongeza au kupunguza kitu kingine, ebu sasa tuwaone watu hawa saba na kile ambacho wanataka kukwambia wewe ili ubadili maisha yako kuanzia siku hii ya leo.

 ANGALIA VIDEO HII: CHUMA HUNOA CHUMA

1. Kama unataka kufanikiwa, unatakiwa kuwa tayari kuchukua njia moja hata kama njia hiyo haina watu wanaoitumia. John D. Rockefeller

Barabara ya mafanikio ni barabara ambayo haina wasafiri wengi sana. kiasi kwamba wakati unaedelea na safari unaweza kuangalia kulia usione mtu ambaye anatembea kwenye hiyo barabara. Na pia ukiangalia kushoto usione mtu ambaye anatembea kwenye hiyo bara bara.

Kwa harakaharaka unaweza kuona kwamba umekosea njia maana ukiangalia njia nyingine unaona foleni ni ndefu.  Ukweli ni kwamba kama kitu ambacho unafanya ni sahihi. Endelea kukifanya bila kujali kuna watu nyuma yako ambao wanakufuatilia kuona kile ambacho unafanya au la.  Kitu huwa hakiwi kizuri kwa sababu ya wingi wa watu ambao wanakifuata. Kama unachofanya hakiendani kinyume na sheria za nchi, basi wewe endelea kufanya tu.

 

2. Watu ambao hawawezi kujihamasisha wenyewe, itabidi waridhike na matokeo ya kawaida bila kujali wana vipaji kiasi gani. Andrew carngie

Kuwa na kipaji peke yake haitoshi. Unaweza ukawa na kipaji na bado watu wengine wakawa wanafanya vizuri kwenye eneo ambalo wewe una kipaji. Kipaji kinahitaji kiambatanishwe na vitu vifuatavyo.

Kwanza, kujihamasisha kama ambavyo anasema ANDREW CERNEGIE

Pili, kujituma na kufanya kile ambacho umepanga kufanya bila kujalli kitu gani kinatokea

Tatu, kwenda hatua ya ziada

Nne, kuwa na mtu ambaye unamwangalia. Mtu ambaye amewahi kufanya kitu kama cha kwako na sasa hivi ameshafikia kwenye viwango vikubwa.

Tano, kuwa tayari kujifunza vitu vipya na kuchukua hatua mpya hata kama zinaogopesha

 

3. Nenda mbali kadri unavyoweza. ukifika huko, utaweza kuona mbali zaidi.

Ukiendelea kukaa na watu wale wale kila siku. Na kufanya vitu vilevile kila siku, ni wazi kwamba utapata matokeo yale yake kila siku. Ila kama unataka kubadili maisha yako sasa hivi anza kuchukua hatua na hakikisha kwamba unaenda mbali. Ukifika huko ni lazima utaona mbali na utaanza safari nyingine ya kuelekea huko.  Kwa mfano sasa hivi, kuna rafiki zako ambao unawafamu na hao rafiki zako wana watu wengine ambao wanawafahamu na wanaweza kukuunganisha nao.

Kwa hiyo unaweza kujikuta kwamba kadri unavyokutana na mtu mmoja leo hii, kesho anakuunganisha na mtu mwingine. Na wewe unaweza kufanya kitu kama hiki kiwe ni sehemu ya maisha yako. Yaani ukaamua kwamba, kila rafiki yako anakuunganisha na mtu mmoja wa maana ambaye pia anafanya kitu kama chako au ambaye anaweza kuwa msaada kwa kile ambacho unafanya au ambaye anaweza kuwa mteja wako. Hili linawezekana.

 

4. Ugwiji ni asilimia 99 ya hamasa na asilimia 1 ni kipaji

Nimekuwa nikisoma historia ya watu ambao kwenye dunia ya leo hii tunawaita magwiji. Watu kama Thomas Edison, watu kama Abert Einstein, watu kama Steve Jobs, Wright Brothers na wengine wengi. nimegundua kitu kimoja kutoka kwa hawa watu. na kitu hiki ni kwamba watu hawa hawakuwa magwiji kama ambavyo dunia ya leo inawatazama. Badala yake ni kwamba hawa walikuwa watu kama wewe hapo ili waliokuwa na maono ya kufika mbali.

Hawa kukubali kuyumbishwa na mtu.

Hawakukubali kukatishwa tamaa na kitu chocchote.

Hawa kurudi nyuma kwa namna yoyote ile.

Waliamua kwamba lazima tusongembele bila kujali nini kinatokea.

Hiki ni kitu ambacho na wewe pia unakihitaji.

 

Kwa hiyo kila siku ukiamka, jihamasishe kwamba unaenda kufanya vitu vikubwa. Moja ya kitu ambacho kinawatofautisha watu ambao wamefanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa ni kwamba watu waliofanikiwa wanafanya kitu ambacho wamepanga kufanya hata kama hawajisikii kufanya hivyo. Wakati watu ambao hawajafanikiwa  wakijisikia tu kama kuchoka basi kwao huo ndio mwisho wa kila kitu. Hakuna kitu cha ziada ambacho wanaweza kufanya. Kuanzia leo hii anza kujenga tabia ya kujihamasisha kila unapoamka asubuhi, mchana na jioni. Jihamasishe kwa kusoma vitabu, jihamasishe kwa kusikiiliza vitabu ambavyo vimesomwa, jihamasishe kwa kuangalia video za watu ambao wamefanikiwa na vitu vingine vya aina hii hii.

 

5. Gramu moja ya mazoezi ni bora kuliko kilo moja ya nadharia John Jacob Astor

Rafiki yangu, ni muhimu kufanyia kazi yale ambayo unajifunza kila siku kwa kuyaweka kwenye matendo. Ujue tupo kwenye ulimwengu ambapo watu wanaujua ukweli ila wanashindwa kuuweka kwenye vitendo. Unaweza kukuta kwamba mtu anaamka asubuhi na kufungua runinga na kuwaangalia watu ambao wanafanya mazoezi. Wakati anawaangalia watu hao akaanza kuwahukumu. Utamsikia akisema, huyu anazembea. Au yule hawezi, utasikia akisema huyu hajui kuruka n.k. lakini yeye anasema hivyo akiwa amekaa kwenye kochi. Ukisema kwamba aende na yeye akafanye mazoezi kama wanavyofanya basi utashangaa kuona kwamba huyu ambaye alikuwa anasema maneno yote hayo kumbe yeye mwenyewe hawezi kufanya mazoezi. Hiki ndicho kitu ambacho unapaswa kuepukana nacho. NDIO maana Jacob Astor anatwambia kwamba gramu moja ya mazoezi ni bora zaidi kuliko Kilo moja ya nadharia.

Ni wazi kwamba kama unahitaji kuwa dereva mzuri unahitaji kujifunza kitu kuhusu uendeshaji kwa kupitia vitabu lakini huwezi kuwa dereva mzuri kwa kusoma vitabu. Hii ndio kusema kwamba utapaswa kukaa kwenye kiti cha dereva na kuendesha gari.

Vivyo hivyo kwenye masuala mazima ya ujasiliamali na biashara. Unaweza kujifunza kuhusu biashara kwa kupitia vitabu. Lakini huwezi kuwa mfanyabiashara bora kwa kusoma vitabu. Nenda nje, kafanye mazoezi. Inawezekana.

 

6. Mafanikio na kushindwa ni vitu ambavyo vinaambatana Nicolas Tesla

Kuna watu ambao huwa wanajitahidi kuukwepa ukweli huu hapa. Nimeandika kitabu kizima ambacho nakiita NYUMA YA USHINDI kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa.  Inawezekana ukawa huelewi ukweli huu, ila iko hivi. Watu wengi wanapenda kupata mafanikio. Lakini sasa dunia lazima ikupime ione kwamba wewe unayehitaji  mafanikio unayahitaji kweli au unahadaa. Na moja ya kipimo hicho ni kushindwa. Ukiweza kuinuka baada ya kushindwa na kuanguka, basi wewe unakuwa kwenye njia bora. Thomas Edison amewahi kunukuliwa akisema kwamba, siku zote nimekuwwa nikiogopa mafanikio ambayo huwa yanapatika mara moja bila kushindwa. Kwa nini? kwa sababu kushindwa sio kitu kibaya bali kupo ili kukuimarisha wewe na kukufanya uweze kusonga mbele. Maana kushindwa kunakufanya wewe ukue zaidi badala ya kukudidimia kama ambavyo watu wengi wanafikiri.

 

7. Ukifunga mikono yako muda wote, hakuna kitu kizuri ambacho kinaweza kutokea. Lakini mkono ambao umenguliwa umebarikiwa maana unapokea  kadri unavyotoa kwa wingi

Linapokuja suala la kutoa watu wengi hufikiri kwamba kutoa ni lazima iwe ni pesa peke yake. Lakini unaweza kutoa pesa, muda wako nguvu zako, akili n.k.  Ni ukweli kwamba dunia huwa inawapa zaidi wale watu ambao wanakuwa tayari kutoa kwanza. Wajasiliamali huwa wanatoa fedha zao kuanzisha kitu. Kwa kufanya hivi wanakuwa wametoa na ndio baadae huja kulipwa kwa kupata watu wa kununua bidhaa zao. Ila kama mtu hayupo tayari kutoa basi ni ukweli kwamba mtu huyu hata kupokea kwake kutakuwa ni kugumu.

 

Zig ziglar hili ameliweka wazi pale ambapo anasema kwamba, unaweza kupata kile ambacho unataka kama utakuwa tayari kuwasaidia watu kupata kile ambacho wao wanataka.

Kama ni mwanafunzi lazima awe tayari kutoa fedha kwenda shuleni kusoma miaka 15 mpaka 20 kabla ya kupata cheti cha kuingia kwenye soko la ajira

Kama ni mkulima lazima awe tayari kujitoa kulima, kupanda, kumwagilia, kupalilia kabla ya kupata mavuno.

Kwa kufanya hivyo wote wanakuwa wanatoa kitu ili waweze kupata kitu. Kama huwezi kutoa kitu basi ni wazi kwamba hutapata. Nadhani wahenga wetu waliliweka wazi hili pale waliposema kwamba asiyepoteza haokoti.

 

Rafiki yangu, leo niliona wazi nikuteletee masomo haya muhimu sana kutoka kwa wajasiliamali ambao wamefanikiwa kwa viwango vikubwa kwenye hii dunia. Kama ambavyo unaona tumejifunza masomo saba kutoka kwa hawa wajasiliamali na wagunduzi wa karne ya 19. Nina uhakika kuna kitu kikubwa sana ambacho wewe mwenyewe unaenda kufanyia kazi mara moja.  Napenda tu nikukumbushe kwamba gramu moja ya kufanya mazoezi ni bora kuliko kilo nadharia. Gramu moja ya kuchukua hatua ni bora kuliko kilo ya kubweteka.

Kama bado hujaSUBSCRIBE kwenye youtube channel yetu, unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza HAPA ili uendendee kufuatiia masomo yetu ambayo tunayatoa hukoo.

Pia usisahau kujiuinga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu kwa KUBONYEZA HAPA

https://www.youtube.com/channel/UCRGDR3d_Pt-TeRxSlF3ORzQ?view_as=subscriber

 

MAKALA NYINGINE ZINAZOENDANA NA HII HAPA: 

MASOMO SABA (07) YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WAJASILIAMALI WAKUBWA

 VITU VITANO VINAVYOFANYA WATU WAUE NDOTO ZAO NA HIVYO KUSHINDWA KUZIFIKIA

 NI KOSA KUJUA KITU KISHA UKAJIFICHA NA KITU HICHO

VITU SITA (06)  AMBAVYO UTAPASWA KUFANYA MAISHANI MWAKO

Rafiki yangu umekuwa na mimi GODIUS RWEYONGEZA

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X