Huu Ndio Mfumo Bora Utakaokuwezesha Wewe Kutimiza Malengo Yako. mfumo huu haujawahi kufeli hata kidogo


 HIVI IMEWAHI KUKUTOKEA, ukiwa kwenye chumba ambapo kuna  kelele nyingi za watu na unaongea na marafiki ila ghafla ukasikia sehemu mtu anataja jina lako. Yaani watu waliokuwa pembeni kidogo wanaonge mwanzoni na ulikuwa hujawasikia wanachoongea muda wote, ila zamu hii tu mtu kataja jina lako, basi masikio yako yameshanasa kila kitu. Hivi ni kitu gani ambacho huwa kinakufanya usikie sauti ya jina lako kwa haraka kiasi hicho wakati maongezi yaliyokuwa yanaendela kabla ya hapo hukuyasikia.

 

Hiki kitu kitaalamu kinajulikana kama RETICULAR ACTIVATING SYSTEM (RAS). Huu ni mfumo wa ubongo wako wa kupokea kile ambacho unataka kwa wakati husika. Yaani kwa mfumo huu ubongo wako unakuwezesha kusikia ambacho unataka kusikia, au kuona ambacho unasikia, kusoma ambacho unataka n.k.

mfumo huu unazuia wewe kuona vitu ambavyo hujavipa kipaumbele kwenye ubongo na kukuwezesha kuona vile vitu ambavyo umevipa kipaumbele kwenye ubongo wako.

Mfumo huu unakuzuia kusikia vitu ambavyo hujavipa kipaumbele na kukuwezesha kusikia vitu ambavyo umevipa kipeumbele peke yake.  

 

Sasa kwa nini ninaandika haya yote. Huu mfumo una kitu gani cha kukusaidia kwenye maisha ya kila siku? Hili hapa linaweza kuwa ni swali ambalo unajiuliza.

Huu ni mfumo bora, ambao ningependa uanze kuutumia kwa manufaa kuanzia siku hii ya leo. Utaweza kuutumia mfumo huu kwa manufaa endapo utaweka malengo yako siku ya leo. Ukishaweka malengo yako utaanza kuyafanyia kazi huku ukihakikisha kwamba unayasoma kwa kuyarudia si chini ya mara kwa siku. Lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha kwamba ubongo wako unajua nini unataka, ili sasa kwa kutumia mfumo wa reticular activating system uweze kukuonesha vitu ambavyo umelenga kulingana na lengo lako na kukuepusha vile ambavyo hutaki kulingana na lengo lako.

 

Kama bado hujanielewa vizuri, hapa ngoja tu nikupe mfano wa kawaida.

 Sasa hivi ni kikwambia kwamba toka nje uanze kuangalia magari ya rangi nyekundu. Utasahangaa kuona mengi kuliko ambavyo umewahi kuyaona siku yoyote. Sio kwamba magari haya hayakuwepo hapo kabla. Yalikuwepo siku zote ila kwa sababu ubongo wako haukuwa umeweka nguvu huko ulikuwa unapuuzia kwa kutumia mfumo huu  huu wa reticular activating system.

 

Ndio maana unatakiwa kuhakikisha kwamba umeandika malengo yako ili mfumo huu uweze kukuletea matokeao sahihi na kukuonesha vile vitu ambavyo wewe unataka kufikia kwenye malengo yako.

 

Wazazi pia wanautumia mfumo huu. Unaweza kukuta kwamba mama anasinzia huku kukiwa  na watu wanaopiga kelele za hapa na pale. Lakini pale ambapo mtoto anatoa mlio kidogo tu, usingizi wote unaisha anaamka kumwona mtoto wake. Huu ndio mfumo wenyewe unakuwa unafanya kazi.

 

Kuna kitu kimoja ambacho siku ya leo nilipenda wewe ufanye. Na kitu hiki sio kingine bali kuhakikisha kwamba unaweka malengo.

Ukishaweka malengo hakikisha kwamba unaanza kuyasoma kila siku ili mfumo huu uanze kufanya kazi kwa ajili ya kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako.

Mfumo huu pia utakuonesha fursa ambazo hukutegemea kulingana na malengo ambayo umejiwekea.

 

Kwa maneno hayo rafiki yangu, nipende kukutakia siku njema sana. kila la kheri.

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


2 responses to “Huu Ndio Mfumo Bora Utakaokuwezesha Wewe Kutimiza Malengo Yako. mfumo huu haujawahi kufeli hata kidogo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X