Hili Ni Eneo Muhimu Ambapo Unapaswa Kuelekeza Bajeti Yako Kwa Miezi Sita Ijayo


 

Rafiki yangu, bila shaka umewahi kusikia kuwa serikali imebadilisha bajeti yake na kuielekeza sehemu nyingine.  Na mara nyingi huwa unakuta kuwa hili linafanyika mara baada ya kutokea kitu fulani cha dharula ambacho hapo awali hakikuwa kwenye bajeti husika ya serikali.

 

Sasa leo hii ningependa na wewe ufanye kitu kama hiki hapa. Hiyo fedha ambayo umekuwa unaiwekeza kwenye maeneo ambayo si ya msingi, basi iwekeze sasa kwenye maeneo ambayo ni ya msingi.

Nimeona tuchukue kipindi cha miezi sita ijayo.  Kama utafuata ushauri wangu ambao nitakupa na ndani ya miezi sita, ukawa hujapata matokeo yoyote yale basi unaruhusiwa kuendelea na maisha yako

Sasa kwa miezi sita azimia kwamba hautatumia fedha kununua vitu ambavyo havikuongezei thamani badala yake utatumia fedha hiyo yote kununua vitabu.

Fedha yote ambayo ulikuwa unaitumia kununua magazerti, zamu hii iwekeze kwenye kununua vitabu. Visome hivyo vitabu kisha fanyia kazi kile ambacho waandishi wameandika kwenye kitabu. Kama  hutapata matokeo baada ya miezi sita endelea na maisha yako ya kila siku

 

Fedha yote ya sigara, iwekeze kwenye vitabu kwa miezi sita ijayo.

Kama ndani ya kipindi hiki hapa hutapata matokeo basi unaruhusiwa kuendelea na maisha yako.

Fedha yote ya bia  iwekeze kwenye vitabu kwa miezi sita ijayo. Fanyia kazi kile ambacho utasoma  kwenye vitabu kwa miezi sita ijayo. Kama hutapata amatokeo, basi unaruhusiwa kuendelea na maisha yako.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X