Vitu Viwili Vya Kushangaza Kuhusu Warren Buffet. Angekuwa Tanzania Watu Wangesema Ametoa Kafara Au Basi Watu Wangesingizia Majini


Katika bara la Afrika kuna tabia moja ya kipekee sana.
Tabia hii imejengwa kwenye msingi kwamba, anayemiliki kitu cha bei ghali basi yeye ndiye, anachukuliwa kama tajiri. Kwa mfano, kama wewe unamiliki nyumba ya bei ghali sana basi wewe ndiye mtu tajiri sana kuliko wote. Hiyo ndio imani ya waafrika walio wengi.
Kwa hiyo imani hiyo imepelekwa karbia kwenye kila kitu.  Anayemiliki simu ya bei ghali basi huyo ndiye tajiri. Anayevaa nguo za kisasa basi huyo ndiye tajiri na alipamba nyumba yake kwa maua ya kisasa basi huyo ndiye tajiri.
Lakini matajiri wamedhihirisha kuwa hilo sio kweli. Sio tu kwa maneno bali kwa kuyaishi. Na leo hii nisingependa niongelee matajiri wengi sana. Bali nimwongelee bilionea Warren Buffet. Kwa utajiri wake basi Tanzania anafaa kuitwa Trilionea. Lakini kuna vitu viwili vya kushangaza sana kuhusu Bilionea huyu. Na nina uhakika kwa vitu hivi vya kushangaza angekuwa Tanzania basi watu wengi wangesema ametoa Kafara. Wengine wangesema majini ndiyo yanamtuma na kauli nyingine ambazo wewe mwenyewe utakuwa unazijua.
Vitu hivi vya kushangaz akuhusu bilionea huyu ni kwamba

SOMA ZAIDI: Je, Shule Na Maisha Yanaendana?

1. ANAISHI KWENYE NYUMBA ALIYOIJENGA MWAKA 1958.
Kiukweli kwa pesa alizonazo. Ni wazi kwamba kama angekuwa mtu mwingine basi angekuwa anaishi kwa nyumba moja matata sana. Lakini yeye anaishi tu kwenye nyumba ya kawaida aliyonunua zaidi ya miaka 60 iliyopita. na nyumba ile anaipa thamani kubwa sana. Warren Buffet anasema kwamba hiyo nyumba anayoishi ni uwekezaji nambari tatu mkubwa kwake kuwahi kufanya. Kwa hiyo unaweza kuona ni kwa namna gani anaiheshimu sana.
Kuna funzo na somo kubwa sana hapa la kujifunza kwa kwake. usikimbizane na kila kila kitu. Kimbizana zaidi na vitu ambavyo vinaingiza fedha mfukoni mwako.
Pia tunajifunza kwamba tunapaswa kuheshimu uwekezaji ambao tunaufanya siku hii ya leo. Kama unaona wazi kwamba unawekeza kwenye anasa basi mwisho wa siku utakuja kujutia uwekezaji wako huo.
2. AMEANZA KUTUMIA IPHONE MWAKA HUU
Huwezi amini kusikia kwamba bilionea huyu alikuwa bado hajamiliki simu nzuri na kali kama Iphone. Ila mwaka huu ndio ameanza kutumia iphone baada ya simu yake ya zamani kuharibika. Buffet amekuwa anatumia simu ya kawaida sana kutoka kwenye kampuni ya SAMSUNG.  Simu hiyo ilikuwa na thamani ya dola 20 tu. sawa na elfu 44 za kitanzania.
Unaweza kushangaa, wakati watu wengine wanakimbizana kununua bei za bei kubwa sana mpaka milioni mbili na zaidi. Yeye ana simu ya elfu 44 tu.
Wakati mwingine mtu akipoteza simu yake kwa siku moja tu ndio anajiona kama vile amepoteza maisha. Ila yeye mwaka huu tu ndio amekuja kununua simu ya aina hii.
Kwenye hili tunajifunza kwamba
Usiwe mtu wa kutaka kuonekana una viwango wakati viwango vyenyewe huna. Hata kama una viwango, usikimbilie kujionesha kwa watu. Kila mtu yuko bize na maisha yako.
Tunajifunza pia kuwa na misimamo  na kutoendeshwa na hisia. Kuna vijana wengi wananunua simu bila kujua hata hizo simu wananunua za nini.  mtu ananuhnua simu ya milioni au zaidi, kisha anaitumia kwa kazi tatu tu. kupiga, kupoteza muda na kuchati. Wakati angeweza kufanya hayo yote kwa simu ya elfu 20 tu.

SOMA ZAIDI; Uwekezaji Huu Utakufanya Kuwa Mtu Mkuu Kwenye Hii Dunia

Nijibu SMS 1000? Au Nisome Kurasa 1000? Ipi Bora? Nifanye Ipi?

HITIMISHO
Siku ya leo napenda nihitimishe kwa kukuelekeza kanuni mbili muhimu sana kutoka kwa bilionea huyu. Kanuni ya kwanza ni kwamba, kamwe usipoteze fedha
Na kanuni ya pili ni kwamba usiisahau kanuni ya kwanza.
Binafsi rafiki yangu napenda nihitimishe kwa kusema kwamba, anza kujenga nidhanu ya kutumia vizuri pesa kidogo.  Inawezekana kwa siku sasa umekuwa unaomba upate utajiri. Lakini sasa kama huwezi kutumia vizuri fedha kidogo zinazopita mikononi mwako, basi niseme tu waziwazi kwamba, miaka itazidi kupita. Na siku moja utakuja kushangaa utajiri haupati. Siku hiyo ukijihoji vizuri utagundua kwamba utajiri huu ulishapita mikononi mwako, ila tatizo lako ni kwamba hukuwa makini kwenye matumizi ya fedha kidogo ambayo ulikuwa unazipata.
Nikutakie kila la kheri rafiki yangu.

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X