Imethibitishwa. Mbinu Za Kitabibu Zinafaa Kutumika Katika Maisha Ya Kawaida Ya Kila Siku


Hongera sana rafiki kwa kuiona siku hii ya leo. Ikiwa ni tarehe 29 August
Ukienda hospitali unaumwa utataja tatizo lako kwa mtaalamu wa Afya. Mtaalamu huyu wa Afya kwa kutumia ubobezi wake atakupima au atakusikiliza tu na kisha kutoa dawa. 
Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa afya wa hospitalini ila kwa leo napenda tuyajue haya mawili ambayo yamethibitika kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.
Kinapatikana kwa sh. 10,000/-
KWANZA, mtaalam wa Afya atakupa dawa kulingana na ugonjwa wako. Haijalishi unaipenda au huipendi. Haijalishi unampenda yeye au humpendi yeye. Ile dawa unapaswa kuitumia. 
Sasa kwenye maisha ya kila siku. Imethibitika kwamba ukweli wa jambo fulani ukitolewa. Haijalishi unaupenda au huupendi. Haijalishi unampenda aliyeutoa au hupendi aliyeutoa ukweli unabaki kuwa ukweli tu. Na huna budi kuufuata. Hivyo jitahidi kuanzia leo kuuchukua ukweli na kuufanyia kazi bila kujali umetolewa na mtu aliye juu ya wewe au aliyechini. Ukweli unabaki kuwa ukweli siku zote.
Mfano wa ukweli ambao utapaswa kuukubali ni huu hapa.
Huwezi kutatua matatizo kwa namna ile ile ya kufikiri iliyosababisha matatizo.
Huwezi kuondoka kwenye madeni kama utaendelea na fikra zilezile ulizokuwa nazo wakati wa kukopa. Huu ni ukweli. Na hivyo utapaswa kuchukua hatua za tofauti ili uweze kuondokana na madeni.
Kama fikra zako zilikuwa kwamba madeni katika maisha hayaepukiki, basi sasa unapaswa kufahamu kwamba madeni ni utumwa. Ukianza kuyaona madeni kama utumwa ujue kwamba umetokea kuona vitu kwa namna ya tofauti ambayo ulikuwa hujaitumia hapo awali.
PILI; Mtaalamu wa afya akishagundua kwamba una ugonjwa fulani atakupa dawa ambazo utazitumia kwa maelekezo yake. Anaweza kukupa maelekezo kwamba utumie hizo dawa mara tatu kwa siku. Au utumie dawa hizo mara mbili kwa siku. Kama kweli upo makini na afya yako basi utafuata maelekezo ya daktari bila kipingamizi ili uweze kupona.
Sasa imethibitishwa kwamba kuna dozi unahitaji ili uweze kufanya mambo ya tofauti.
1. Dozi ya kusoma vitabu mara tatu kwa siku. Kama kwa siku unaweza kupata muda wa kula mara tatu mfululizo bila kuacha sasa unashindwa nini kusoma vitabu mara tatu mfululizo. Soma vitabu asubuhi, mchana na jioni kama vile umepewa dozi kutoka kwa mtaalamu wa afya.
2. Fuata maelekezo mpaka upone. Hakuna daktari anayekwambia tumiatumia hii dozi ukijisikia kupona achana nayo. Sharti ni kwamba dozi lazima iishe. Vivyo hivyo kwako. Ukitaka kupata matokeo ya tofauti sharti lazima ukubali kulipa gharama na kuvumilia mpaka mwisho.
Hizo ndizo mbinu za kitabibu zilizothibitishwa kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.  
KUMBUKA: utapaswa kuupokea ukweli kama ulivyo na kuufanyia kazi, lakini pia utapaswa kufanyia ukweli huo mwanzo mpaka mwisho. 
Jiunge nami kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRICA ili tuambizane ukweli na kuchukua hatua kila siku.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X