NI MARUFUKU KUKATA TAMAA


Mtu mmoja amewahi kusema kwamba hapa duniani kila mtu ana kazi yake. Kuna watu kazi yao ni kukatisha tamaa. Kwa hiyo ukiona mtu anakukatisha tamaa, jua yupo kazini. Na wewe endelea na kazi yako.
Ila cha msingi ni kwamba, kazi za watu wengine zisikukwamishe wala kukuzuia kusonga mbele.

Nakumbuka siku ya kwanza nilipoandika makala na kuiweka kwenye blogu, nilimshirikisha rafiki yangu ushindi mkubwa niliokuwa nimepata. Kwangu ulikuwa ni ushindi usio wa kitoto. Ila yeye alicheka sana. Na huyu ni mtu nikikuwa namtegemea sana kwa ushauri (kipindi hicho yupo Chuo kikuu mwaka wa nne, mimi ndio kwanza chuo kikuu nakisikia tu😀). Alisema kwamba, kuandika kunahitaji uzoefu. Na ili uanzishe blogu unapaswa walau kuwa na makala zisizopungua thelathini (30). Hiki ni kiwango cha chini sana kwake. Kipindi kile sikuwa hata na makala kumi, na wala sikujua kesho nitaandika nini. Ila niliamua nitaandika kila siku makala moja moja hata kwa kuibia kwa watu.😀😀

Kweli bhana. Unadishi sio lelemama. Kuna siku nilikuwa nakosa cha kuandika natafsiri makala za kiingereza kwa kiswahili😀😀😀 (hapa unapaswa kucheka kidogo).

Ila baada ya  mwezi nilianza kuwa fundi. Leo hii ndio nimekuja kukumbuka kwamba mwanzoni nilikuwa natafsiri makala za kiingereza kwa kiswahili.

🔥Kesho kwenye blogu ya SONGA MBELE itakuwa na makala 600. Laiti ningeacha kuandika siku ya kwanza, ushindi huu mkubwa nisingeufikia hata kidogo.

Kona nyingine ya kukatisha tamaa nikikutana nayo wakati naendelea kuandika.Huwa nina tabia ya kuongea malengo yangu ambayo nitayafanyia kazi. Sasa siku hiyo nikawa naelezea jinsi nitakavyoandika kitabu.

Dada mmoja alicheka sana. Alisema, “hivi wewe unataka kuandika kitabu kama nani? Vitabu wanaandika akina Ben Carson ambao wamefanya mambo ya kuonekana kwa jamii. Sasa wewe utaandika nini?”

Najua nilimpa maelezo mengi ya kwa nini napaswa kuandika kitabu ila hakunielewa. Maneno hayo niseme ukweli yalikuwa kama teke la punda vile. Yalinifanya niache kuandika muda fulani hivi. Nikaanza kuusubiri ubenikasoni😀😀.
Ila baadae nikaamua tu nitaandika. Nilisema, “mimi sio Ben Carson wala Mimi sio maarufu, lakini kile ninachojua kinaweza kuwa msaada kwa watu hata wachache. Nina sababu ya kuandika na nitaandika”. Sikuendelea kuusubiri ubenikasoni.

Leo hii nikiangalia nyuma kidogo na kuona yaliyokea. Najiuliza hivi kwa mfano ningemua kuacha kuandika kabisa tangu siku ile dada yule alivyonikatisha tamaa
🔥Je, ni lini ningekuja kuandika kwenye gazeti (MWANANCHI)?

🔥je, ni lini ningeandikwa kwenye gazeti (THE CITIZEN)

🔥Je, ni lini ningealikwa maredioni na kwenye TV, kuongea (Sua FM, Abood FM na abood TV).

🔥Je, ni lini ningetoa vitabu. (Mpaka sasa hivi  nimeandika Vitabu vitano)

🔥Je, ni lini ningepata nafasi ya kushirikiana na watu ambao nimekuwa nikiwasikiliza kwenye maredio na TV. Watu ambao wamegusa maisha ya watu? Watu ambao ninawakubali.

Kumbe ukweli ni kwamba sipaswi kuwa Ben Carson ili kuandika kitabu. Ninahitaji kuwa Godius Rweyongeza ili kuandika kitabu.

Nakusalimu tu rafiki yangu. Naomba nikutakie siku njema na bora sana.

# *UsisubiriUweBenCarson*
# *AnzaKuwaWewe*
#Makala600KwenyeBloguMoja
# *SongambeleBlog*


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X