Hivi Ndivyo Mazoezi Yanaweza Kukufanya Ule Meza Moja Na Mfalme


Katika mazingira yetu ya sasa hivi wafalme sio watu  waliozoeleka sana kulinganisha na kipindi cha nyuma. Zamani kidogo ulikuwa unakuta kabila fulani lina mfalme wake ambaye watu wote wanamsikikiza na sauti yake iko juu kwenye masuala ya utawala. Lakini pia mfalme kama kiongozi alikuwa anapata vitu vyote vizuri. Yaani kwake nguo zilikuwa ni nguo bora sana kuliko mtu mwingine, chakula chake kilikuwa ni chakula bora sana, malazi yake yalikuwa ni ya kipekee sana. Sio hivyo tu hadi usafiri wake ulikuwa ni wa kipekee, ardhi ya mfalme ilikuwa ni ardhi yenye rutuba kweli kweli. Kwa mazingira ya sasa hivi mfalme ndio raisi wa nchi.

Lakini mwa mantiki ya makala hii mfalme sio raisi tu. Naomba nitoe maana ya mfalme kulingana na ujumbe wa leo. Mfalme ni mtu ambaye amefikia mafanikio makubwa iwe ni kiuchumi, kiuongozi, kiroho, kimahusiano, n.k
Mtu ambaye wewe ungependa kukutana naye au pengine umekuwa  na shauku ya kukutana naye kwa siku nyingi sana ila hutapata nafasi hiyo kutokana na utofauti uliopo kati yako na yeye kimafanikio.

Hawa ni watu ambao stori za kitaani huwa tunaishia kusema walikuwa na bahati. Pengine huwa tunasema walibahatika kurithi mali za mjomba, baba, shangazi au ndugu fulani. Au ni wale watu ambao wengine wanasema alikutana na jini likampenda basi likampa utajiri😀😀.
Na pengine wapuuzi wengine wanasema amejiunga freemason.

Je, kuna watu ambao umewahi kusema maneno kama haya juu yao. Je, kuna watu wa namna hii ambao ungependa kukutana nao ila hujui utawezaje?
Leo hii ninakuja kwako na namna rahisi sana ya kukuwezesha kukutana na watu hawa na pia mbinu hizi zitakuwezesha kuwa mmoja wao.

Moja anza kwa kujiuliza una nini? Ni kitu gani ambacho unaweza kuanza nacho kikakusogeza mbele. Je, una kisomo fulani? Au una kipaji fulani? Au utaalamu fulani?

Ukishajua kile ulichonacho kinachofuata ni wewe kuamua kuwa gwiji kwenye hicho kitu. Usihangaike na mengine. Ebu tuchukulie mfano umejikuta wewe una ujuzi na kisomo cha sheria. Basi unaamua kukomaa hadi kuwa gwiji wa sheria. Mpaka kieleweke. Hakikisha kama katika nchi hii wanatafuta wanasheria watatu mabingwa basi na wewe unakuwepo.
Sula hili halitakuchukua mwaka mmoja au miwili. Ni suala la muda mrefu. Kuanzia miaka saba mpaka kumi na tano!!!!!!!!!

Lakini ukiweza kutoboa hapa. Jua utakula meza moja na wafalme.
Kwanza utakuwa mtu ambaye anafutwa sana jambo ambalo litapelekea wewe kukipwa sana. Jambo ambalo litapelekea wewe kupata vizuri sana ambavyo ulikuwa unatamani (gari, nyumba, n.k)

Jambo hili halitawasili kwako kirahisi rahisi kama unavyofikiri, litahitaji kuwekeza katika kusoma. Litahitaji pia uwekeze katika kufanya mazoezi ya kitu hicho.

Ebu tuchukulie mfano wetu hapo juu. Umejikuta una kisomo cha sheria, basi utapaswa kufanya mazoezi ya masuala ya sheria kila iitwayo leo. Utahitaji kusoma sana vitabu vya sheria kuliko mtu mwingine aliyekuzunguka.
Kumbuka, ukitoa jasho jingi sana wakati wa mazoezi, utatoa damu kidogo wakati wa vita.
Yajayo yanafurahisha, je, upo tayari?

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


One response to “Hivi Ndivyo Mazoezi Yanaweza Kukufanya Ule Meza Moja Na Mfalme”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X