Kipaji Peke Yake hakitoshi: Vitu Vitano Unavyohitaji Ili Uweze Kutoboa


Kuna watu wanakaa wanafikiri kwamba wangezaliwa na aina fulani ya kipaji basi maisha yangewaendea sawa sawa kabisa.  Yaani kwamba wangefurahia mema ya nchi.

Sasa labda swali la kujiuliza ni Je, watu wote wenye vipaji wamefanikiwa sana?
Jibu la haraka ni hapana. Ndio maana Myles Munroe anasema sehemu tajiri hapa duniani ni makaburini. Huko ndipo kuna watu waliokufa na mawazo makubwa, watu waliokufa na vipaji vyao n.k

Kuwa na kipaji ni sehemu ndogo ya mafanikio. Kama ni asilimia basi hata haifiki hata asilimia moja. Kuna mambo mengine ambayo yanaendana na kipaji ambayo unapaswa kuyajua.

Soma Zaidi; TAFAKARI YA WIKI; Kipaji Ni Bei Rahisi Sana Kuliko Chumvi

1. KUANZA KUKITUMIA
Ukiwa na kipaji hata kama ni kizuri na bora kiasi gani, bila kukitumia rafiki yangu unajichimbia tu shimo.

Utaishia kujigamba, mnanionaje. Mimi ninaweza kitu fulani kumbe upo upo tu. Kuwa na kipaji haitoshi, anza kukitumia. Lamarck aliwahi kusema kwamba kiungo chohote kisipotumika basi kitakufa na kupotea vivyo hivyo kwa kipaji.

2. HAMASA
Wakati unatekeleza kipaji chako utakutana na changamoto na vikwazo vitakavyokuzuia wewe kusonga MBELE. Hapa utahitaji kujihamasisha.

Hamasa ndio itakufanya usonge mbele. Utapata hamasa kwa kusoma vitabu, kusikiliza Vitabu vilivyosomwa, kujihusisha na watu chanya.
Kipaji peke yake hakitoshi, hamasa ni muhimu.

3. Uvumilivu
Thomas Ediaona anafahamika kwa usemi wake maarufu kwamba mafanikio ni asilimia moja ya hamasa na asilimia 99 uvumilivu.
Utahitaji kuweka juhudi na kuvumilia ili kufikia mafanikio uyatakayo.
Kipaji peke yake hakitoshi uvumilivu unahitajika.

4. MAZOEZI
Unahitaji kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili uweze kukitumia vyema sana kipaji chako. Mchezaji wa mpira hata kama ana kipaji kiasi gani kwake mazoezi ni lazima. Na wewe unahitaji mazoezi makubwa tena ya kila siku.

SOMA ZAIDI; Jinsi Ya Kuunganisha Elimu Ya Shuleni Na Maisha Ya Kawaida

5. KIPE MUDA
Kama utaanza kufanyia kipaji chako leo basi usitegemee matokeo mazuri kuanzia kesho. Utahitaji kukipa muda kipaji kikue zaidi. Wataalam wanasema kwamba inachukua miaka saba mpaka kumi kwako kuanza kupata matokeo makubwa sana. Kwa hiyo usihofie kuweka juhudi mara kwa mara ili uweze kupata matokeo makubwa. Ni suala la muda tu kipaji chako kitaanza kuonekana

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


One response to “Kipaji Peke Yake hakitoshi: Vitu Vitano Unavyohitaji Ili Uweze Kutoboa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X