Aina Hii Ya Kimbelembele Inaruhusiwa Kwa Kiwango Kikubwa


Steve Jobs alikuwa mvumbuzi ambaye ameishi kwenye zama hizi zetu. Mtu huyu (Steve Jobs) kwa kipindi cha maisha yake amevumbua vitu ambavyo vimebadili maisha ya watu na mwonrkano wa dunia nzima.

Mwaka 1984, Steve Jobs alikuja na aina na kompyuta inayojulikana kama Macintosh. Aina hii ya kompyuta ilibadili kabisa hali ya hewa kwenye tathnia ya mawasiliano.

Hakuishia hapo mwaka 2001 mvumbuzi huyu alikuja na IPAD. Mwaka 2007 alikuja na kifaa kinachojulikana kama iPhone.

Vifaa hivi vyote vilibadili mwonekano na mwenendo mzima sekta ya mawasiliano.

 Kuna aina ya kiherehere ambayo mvumbuzi huyu alikuwa nayo, na aina hii kiherere ndio imefanya agundue vitu ambavyo ni bora kwa nyakati zote. Aina hii ya kiherehere ni nzuri sana kiasi kwamba na wewe utapaswa kuwa nayo.
Aina hii ya kiherehere ni ya kutengeneza miundombinu ya miaka mitano mbele na kuitoa leo.
Yaani kitu ambacho ungekipata miaka mitano na zaidi kutoka sasa yeye alikuwa anakifanyia kazi na kukitoa leo hii. Jambo hili linajidhihirisha pale alipozindua kompyuta aina ya WORKSTATION mwaka 1989, baada ya uzinduzi huo mwandishi alimwuliza kwa nini unacheleweaha usambazaji wa kompyuta, Jobs alisema, “kiukweli sio kwamba ninachelewesha kifaa hiki bali ninakiwahisha kabla ya wakati wake. Kimetangulia kwa miaka mitano”.

Vivyo hivyo kwa mwaka 2007 alipokuwa anazindua iPhone. Alisema kifaa hicho amekiwahisha miaka mitano kabla. Maana yake makampuni mengine mpaka yaje kufikia viwango hivyo itawachukua miaka mitano mbeleni.

Sasa na wewe unapaswa kuwa na aina hii ya kiherehere.

Soma vitu ambavyo watu wengine watakuja kuanza kuvisoma miaka mitano ijayo.

Toa huduma ambayo  itakuwa mbele kwa viwango kuliko mtu mwingine.

Andika kitabu ambacho itawachukua wengine miaka mitano kukikamilisha.

Kila kitu kifanye kwa viwango vya huu kiasi kwamba kiwe miaka mitano mbele kuliko wengine

Soma Zaidi; Ukisikia Fulani Ni Kiongozi Basi Jua Anafanya Hivi

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X