ZAMA ZIMEBADILIKA-5


Moja kati ya usemi ambao kocha Makirita Amani amekuwa akiutumia ni usemi kwamba, tunaishi katika zama ambapo mtu wa kawaida  ana vyanzo vingi vya maarifa kuliko mfalme wa karne ya 15″. Usemi huu unasimama kama ulivyo bila hata kuhitaji miguu ya ziada kuubeba.

Kiwango ambacho binadamu amekuwa akipata maarifa  kimekuwa kikibadilika Kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kiwango hiki kimekuwa kikiongezeka kwa kasi sana haswa pale binadamu alipoanza kuweka vitu katika maandishi.

Na hili tunaweza tu kuliona kupitia kiwango cha maandishi ambayo yamekuwa yakitolewa Kila mwaka.
Kabla ya mwaka 1500 bara la Ulaya peke yake likikuwa linatoa vitabu 1000 kwa mwaka. Hii ina maana kwamba ingekuchukua karne nzima kupata vitabu vyenye uwezo wa kujaza maktaba moja tu.

Kufikia mwaka 1950 (baada ya karne NNE na nusu). Bara la ulaya tu lilikuwa na uwezo wa kuzalisha vitabu 120,000. Hii ndio kusema kwamba kile ambacho kilichukua karne kujaza maktaba, sasa kilikuwa kinachukua mwaka tu. Yaani haya ni mabadiliko makubwa sana.

Sasa cha kushangaza zaidi ni kwamba kufikia  katikati ya miaka 60, bara la Ulaya lilikuwa na uwezo wa kutoa vitabu 1000 kwa siku sawa na vitabu 360000 kwa mwaka .

Bila shaka mpaka hapo unajiuliza na takwimu zote hizo zinatupeleka wapi!
Ukweli ni kwamba kwa sasa mtu wa kawaida sana amezungukwa na vyanzo vyingi   vya taarifa kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa watu wengi kuchagua maeneo ya kuwekeza muda na nguvu zao.

Tofuti 1500 ambapo vitabu vilikuwa vinachapwa 1000 kwa mwaka. Kwenye zama hizi kiwango cha uchapaji wa vitabu kwa mwaka ni kikubwa sana.

Na vitabu hivi vinavyochapwa sio tu kwamba vinarudia kuandika kitu kile kile. Bali ni ugunduzi mpya ambao unazidi kutokea Kila siku. Na ugunduzi huu unasukuma lakini pia unaleta uhitaji wa vitabu vipya.

Tukiachana na suala la vitabu makala zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii kwa siku moja ni nyingi sana.
Video zinazowekwa you tube ni nyingi mno.

👉Video ambazo ungeweza kuziangalia kwa muda wa saa 60 zinawekwa you tube ndani ya kila dakika moja

👉Zaidi ya video bilioni nne zinaangaliwa kila siku

👉Zaidi ya watu milioni 800 hutembelea you tube kila mwezi

👉Zaidi ya saa bilioni 3 zinaangaliwa kila mwezi

👉70% ya watazamaji wa video za you tube wanatoka nje ya Marekani.

👉Video zenye urefu wa miaka 500 zinaangaliwa kila siku kupitia mtandao wa facebook

👉Zaidi ya video 700 zinashirikishwa kwa watu wengine kwenye mtandao wa twitter kila siku

Kwa hiyo mabadiliko ni makubwa sana ndani ya zama hizi. Na mabadiliko haya huwezi kuyakimbia .

Ila Unapaswa kuchagua aina ya taarifa unazoruhusu kupata kila siku.

Chagua aina ya maarifa yanayokufaa na yanayokusogeza kwenye kilele cha mafanikio

Chagua aina ya mitandao ya kutembelea. Hii inahusisha blogu za kusoma na you tube channel za kutembelea.

Kumbuka kwamba vyanzo vya Maarifa vinapokuwa vingi, kinakuwa ni chanzo cha kuwapoteza watu wengi zaidi. Maana ukweli wa wahenga wetu unaosema kwamba miluzi mingi humpoteza mbwa haujazeeka.

Imeandikwa na
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

*RASMI SASA:* kitabu cha ZAMA ZIMEBADILIKA, kitazinduliwa rasmi tarehe 15/4/2019 asubuhi na mapema sana!

Kitabu kitaanza kupatikana kwa soft copy kwanza.

Bei itatolewa baadae


One response to “ZAMA ZIMEBADILIKA-5”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X