IJUE KANUNI YA MBEGU NA JINSI YA KUITUMIA


Rafiki kila kitu unachokiona kimejengwa chini ya misingi na kanuni fulani. Kitu hiki kikifuata kanuni hiyo sio tu huweza kuwa bora zaidi bali pia huwasaidia wengine kupata zaidi au kuboresha mazingira zaidi.

Mbegu hizi tunazoziona pia zipo chini ya kanuni maalumu ambayo hutumika kwa manufaa.

Kanuni ya mbegu ni kwamba, mbegu lazima ife ili kuzalisha zaidi. Ndio maana siku zote tunaona kwamba mbegu inawekwa udongoni na kupoteza uwezo wako wa awali, ila kwa kufanya hivi inatoa mbegu zaidi. Ndio maana mtu akipanda punje moja havuni punje moja tena. Bali anavuna matunda yenye punje nyingi sana.

Sasa kanuni hii tunawezaje kuitumia kwenye maisha? Je, ni kwamba tutapaswa kufa kwanza ili tufanye makubwa sana?
Hapana. Hapa kikubwa ni kwamba tutapaswa kuwa tayari kuwekeza kidogo kile tulichonacho ili tupate kikubwa zaidi. Kuwekeza ni sawa na kuua kitu, ila unawekeza ili uweze kupata zaidi.

Hapa  kuna maeneo sita ambayo unaweza kuwekeza mara moja
1. Wekeza katika wewe. Wekeza kwako kwa kutafuta kuwa mtu bora zaidi ya ulivyokuwa jana. Ifanye iwe ya kipekee zaidi ya ilivyokuwa jana.

2. Wekeza katika maeneo ambayo yatakuza kipaji chako zaidi ya kilivyo sasa.

3. Wekeza katika maeneo ambayo utakuza  kipato chako.

4. Wekeza katika kufanya maisha ya watu yawe bora zaidi.

5. Wekeza katika kutatua matatizo ya watu unaokutana nao au jamii yako.

6. Wekeza katika kuitumia siku ya leo vizuri maana leo ndio siku pekee ambayo ipo mikononi mwako. Usianze kufikiria utapata siku nyingine. Leo ni leo esho huwa haiji.

Hongera sana kwa kujifunza kanuni ya mbegu na jinsi ya kuitumia.

SOMA ZAIDI: IJUE KANUNI YA CHUMVI NA JINSI YA KUITUMIA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X