Huyu Ni Mtu Ambaye Lazima Utamwambia Hapana


Kila siku huwa ni fursa mpya. Fursa kuanzia watu tunaokutana nao. Watu tunaoongea nao, vitu tunavyofanya n.k

Sasa fursa hizi huwa zinategemea ni kwa jinsi gani ambavyo mtu anaenda kuzitumia.

Moja ya fursa ambayo inajitokeza ndani ya siku katika maongezi ni kukubali au kukataa. Kusema ndio au Hapana.

Kuna watu wanafikiri kwamba haya ni maneno mawili ambayo huwa hayatumiki kwa wakati mmoja. Yaani kwamba likitumika moja jingine halitumiki. Ikitumika Ndio basi Hapana haitumiki kabisa.

Ila sasa cha kushangaza ni kwamba maneno haya yanatumika yote kwa pamoja. Ukisema ndio kwa mtu unakuwa unajiiambia wewe HAPANA. Na ukisema HAPANA kwa mtu wewe unakuwa unajiambia ndio. Iko hivyo.

Ebu chukulia mtu anakuja na kukwambia kwamba anataka umsaidie kazi zake kwa muda kidogo na wewe unakubali ukisema ndio.
Hii ndio kusema kwamba kukubali kwako kumsaidia ni kujiambia Hapana mwenyewe. Maana kazi zako zitakwama na ratiba yako itahairishwa. Hivyo rafiki unapoamua kutumia maneno haya. Amua kweli kuyatumia kwa manufaa yako zaidi. Usitumie maneno haya mwisho wa siku ukajikuta unajutia. Asante sana,

Soma Zaidi: Neno Hili Litakufanya Upendwe Na Watu, Na Neno Hili Litakufanya Uchukiwe Na Watu

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X