Kama Tatizo Ni Nyota Ya Kwako Imeenda Wapi?


Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi hii ya kipekee sana. Zawadi ya maisha.
Moja kati ya vitu vinavyoongelewa sana na watu ni nyota. Mtu akifanikiwa wanasema ni nyota. Asipofanikiwa pia wanasema ni nyota. Mtu akijenga mahusiano mazuri wanasema ni nyota. Lakini pia mahusiano yake yakiwa mabaya wanasema ni nyota. 
Imefikia hatua sasa watu wamesahau misingi muhimu sana ya maisha maana kila kitu sasa kinaelekezwa kwa nyota. Wanafunzi hawasomi tena, wakishindwa wanasema nyota zao mbaya. Watu hawajishughulishi na kazi na matokeo ya uzembe yako wazi kabisa. Yaani njaa, umasikini na maisha mabovu. Ila bado wanasema ni nyota zao ni mbaya. 
Akionekana mtu anafanya vizuri katika sekta fulani labda muziki, biashara, uigizaji, uchoraji, utangazaji n.k basi wanasema mtu huyu nyota yake ni nzuri. Au nyota yake inamurika.
Inashangaza sana, maana imefikia hatua sasa hata ile misingi ya kazi watu wameisahau. Wanasahau ule usemi unaosema kwamba asiyefanya kazi asile. Wanasahau kwamba Nyuma ya ushindi Kuna kushindwa, kuanguka, kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Haya yote yanawekwa pembeni na suala na nyota ndilo linawekwa mbele. 
Sasa swali langu kwako ni hili? Kama tatizo ni nyota, ya kwako imeenda wapi? Nani amekunyang’anya nyota yako? 
Kiukweli watu wanapozungumzia nyota, basi wanakuwa wanamaanisha bahati. Ndio maana utasikia watu wakisema maneno kama haya “unamwona fulani alivyofanikiwa, aligusa na mambo yote yakajipanga”.  
Kama Kuna watu wameweza kungarisha nyota zao kwa nini wewe usingarishe ya kwako? Wao wana nini ambacho wewe huna.
Leo hii napenda ufahamu hizi njia muhimu za kungariaha nyota zao

1. TENGENEZA TIMU YA WATU WANAOKUFAHAMU.
Asilimia kubwa wanaosema, fulani ana nyota huwa wanasingizia kwa sababu eti yeye ana idadi ya watu wengi wanaomfahamu (connection). Lakini cha kushangaza na wao huwa hawatumii muda wao kuongeza mzunguko wao wa watu muhimu sana. Na hivyo kuishia kulalamika tu bila kusonga mbele. Sasa, rafiki yangu napenda ufahamu kwamba jumuiya ya watu inatengenezwa. Robin Sharma aliwahi kusema hivi “ulizaliwa peke yako ishi kiasi kwamba utakapokufa, utaacha jumuiya ya watu nyuma yako”. Kwa mantiki hii Robin Sharma alitaka tutengeneze mahusiano bora. Tuishi na watu vizuri lakini pia tusiishie kuwa na mahusiano na watu wale wale kila mwaka. Bali tuongeze idadi ya watu wanaotufahamu kila iitwayo leo. Ni kwa jinsi tutakuwa tunangarisha nyota yetu.
Hata katika biashara, mtu huwa unamuuzia mtu ambaye anakufahamu. Kwa hiyo anza kutafuta kufahamika kwanza. Hakikisha kila siku unaongeza mtu mmoja kwenye mzunguko wako.
Kwa kumalizia hapa napenda ufahamu kanuni hii, idadi ya watu unaowahamu ipo sambamba na mafanikio utakayopata.
2. KUJARIBU HATUA MPYA
Watu wasiofanikiwa ni waoga siku zote kuchukua hatua. Wanakuwa na malengo makubwa sana ndani yao. Ila hawayaoneshi katika matendo yao. Kila siku wasema “ningekuwa na hiki ningefanya kile”. Ila hali ni tofauti kwa wale wanaowasema kwamba wana nyota nzuri. Wao wanachukua hatua bila uoga. Hawako tayari kufa na kitu ndani yao. Watu hawa wanaosemekana kwamba wana nyota wanaishi kwa kanuni inayosema, “ kitu kilicho ndani yangu sio changu, Bali cha jamii”. Wanajua kwamba wakiwa na mziki ndani yao huo mziki sio wa kwao kwa maana huo mziki upo kuwaburudisha watu wengine. Na kweli wanapoutoa mziki basi jamii inaupokea kwa mikono miwili. Kinachofuata ni wao kuzidi kung’aa zaidi.
Soma Zaidi; Huyu Ni Mtu Ambaye Hashikiki Kwenye Karne Hii Ya 21
3. KUISAIDIA JAMII
Kuna kanuni muhimu sana ambayo watu wenye nyota wanaitumia, wanasema hivi “unaweza kupata chochote unachohitaji kama utaisadia jamii kupata inachohitaji”.
Chukulia mfano wa mimiliki wa gari. Huyu ni mtu ambaye anafahamu kwamba akileta gari kwenye jamii na kutatua tatizo LA usafiri kwa kurahisha mfumo wa usafiri, basi jamii itamlipa na yeye apata chochote anachohitaji.
4. MWIZI WA KWANZA NYOTA NI WEWE
Kama nyota zinaibwa, basi mwizi wa kwanza ni wewe. Na mwizi pekee ni wewe. Hakuna mtu ambaye amkukata mikono, miguu au viungo vyako ili usitimize ndoto zako. Hata kama amefsnya hivyo ila bado una rasilimali muhimu sana ambayo ni akili. Kama hutumii akili yako basis jua kwamba nyota yako unaziba, unaififisha na kuipoteza. Usifanye hivyo. Usijiibie nyota yako. Badala yake ipige msasa ili ionekane iking’aa kila wakati.
Ipige msass kwa kuwa mtu wa vitendo zaidi ya maneno. Ipige msasa kwa kutimiza majukumu yako ya kila siku bila kuacha.
Ipige msasa kwa kusoma vitabu vunavyoelismisha zaidi ili uwe na maarifa zaidi kila siku. 
Je, mpaka sasa bado unaona nyota yako imeibiwa?
Kwa nini
Na ni kaiiba. 
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X