Hivi Mbwembwe Za Mwaka Mpya Maana Yake Nini?


Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya leo.  Ikiwa ni tarehe 03 ya mwaka mpya 2019.
Leo kwa pamoja napenda tutafakari swali libalosema, hivi mbwembwe za mwaka mpya maana yake nini?

 Siku ya mwisho ya mwaka watu huwa wanakaa kusubiri mwaka mpya. Wapo ambao huwa wanaenda kwenye mikusanyiko mbalimbali kama kanisani au viwanja maalumu. Wengine huwa wanakaa kwenye familia zao kwenye vikundivikundi. Ila lengo la watu hawa wote huwa ni kushangilia na kushereherekea mwaka mpya unaoanza.

 Sasa swali langu ambalo najiuliza mbwebwe hizi za kusherehekea mwaka mpya maana yake nini?

Hivi kitu gani huwa kinawafanya watu washangilie?
Je, ni kwa sababu wanaukaribia uzee?
Au kwa sababu wametimiza ndoto kwa mwaka unaoisha?
Au kwa sababu hawakutimiza ndoto na hivyo wanafurahia uzembe wao?

Kiukweli hili kwangu ni swali la kutafakairisha sana.

Rafiki yangu, najua mpaka sasa haitajiki mtu kukwambia kwamba kinachobadilika ndani ya mwaka mpya ni tarehe ila vitu vingine vinabaki vilivyo isipokuwa wewe ubadilike.

Hivyo hakikisha unapokuja kushangilia mwaka mwingine unashangilia huku ukiwa na sababu kubwa sana.
Sababu kama
1. Kutimiza malengo yako
2. Kufanya mabadiliko makubwa sana maishani.
3. Kuboresha huduma katika biashara au huduma unazotoa
4. Kufungua biashara n.k

Hizi ndizo sababu zinazoweza kukufanya uahangilie ila sio unashangilia tu ilimradi umeshangilia.

Soma Zaidi; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-95, tatizo unasubiria mwaka mpya

Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio ndani ya 2019


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X