Unahitaji Hiki Kabla Ya Kufanya Hicho Hapo


Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi ya siku hii ya leo. Kwa hakika leo ni siku njema sana ambayo unapaswa kuitumia.

Kumbuka kwamba utakumbukwa kwa yale uliyoyafanya na kuyamaliza sio kwa yale uliyojaribu kufanya. Hivyo hakikisha leo. Unafanya kweli kweli ulichopanga kufanya.

Kuna siri moja ambayo imejificha na ninaona watu wengi bado hawajaijua siri hii. Na siri hii sio nyingine bali kujiandaa.

Mara nyingi sana kabla ya tukio fulani huwa yanatangulia maandalizi.
Kwa mfano kama kuna sherehe ya kitaifa, huwezi kukurupuka tu siku ya mwisho na kuitisha sherehe. Unapaswa kuwa na maandalizi ya kutosha. Unawatumia watu kadi za mwaliko mapema.

 Kama kutakuwa na waongeaji unawaandaa mapema ili waandae kitu cha maana.
Na penngine kama kuna harambee, unasema kabisa. Hii yote sio tu kwamba inafanyika ilimradi imefanyika. Bali ina maana yake.

Vivyo hivyo kama unahitaji chakula, lazima uanze kukifanyia maandalizi bila kuchelewa. Sio tu unakaa na kusubiri njaa inapokuwa imekuuma ndipo unakuja kustuka kwamba sasa hapa kinahitajika chakula.

Kwa hiyo mandalizi ni muhimu sana. Ndio maana Abraham Lincoln aliwahi kusema kwamba, ukinipa masaa sita ya kukata mti, nitatumia masaa manne kunoa shoka.
Hapa alitakab kutuonesha umuhimu wa kujiandaa kabla ya kufanya kitu kikubwa. Ebu na wewe anza kujenga utaratibu wa kujiandaa kuanzia leo hii.

Kujiandaa hakumaanishi kwamba usiwe unafanya kazi. Bali kwamba upate muda wa kukaa chini na kupangilia mambo yako.
Upate muda wa kukaa chini na kupangilia wiki yako, mwezi na mwaka. Na haya ndio maandalizi menyewe. Huhitaji masaa manne kama anavyosema Abraham Lincoln, lakini walau utahitaji dakika kadhaa, pengine wiki, mwezi na hata miaka kulingana na ukubwa wa jambo ambalo unataka kulifanya.

Yajayo yanafurahisha, je, upo tayari kujiandaa??

Kaa chini  leo uangalie mpango wako. Ugawe katika vipengele mbali mbali. Jiulize je, hapa ninahitaji kujiandaa kwa kufanya nini??

Soma Zaidi; Kutoka Sifuri Mpaka Ubilionea (Mbinu Kumi Zitakazokuinua Mpaka Ubilionea)

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X