UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-4 (Kupanda Na Kushuka Kwa Thamani Ya Pesa-2)


Utajiri wa Mataifa

Ukurasa 47-50

Kupanda na kushuka kwa thamani ya pesa.

Imani yangu kwamba unaendelea kufuatilia kwa umakini chambuzi hizi hapa, tangu tumeanza mpaka hapa tulipo. Bado tunazidi kusonga mbele mpaka kieleweke.

Soma Zaidi:  THE WEALTH OF NATIONS-3 (kupanda na kushuka kwa thamani ya pesa)

“Kupanda na kushuka kwa thamani ya pesa hufuata kanuni zile zile zinazosababisha kupanda na kushuka kwa bidhaa za kawaida”.

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwa nini huwa kuna kipindi bei ya nyanya huwa inapanda sana, na kuna kipindi huwa inashuka sana.

Yaani kuna wakati unaweza kwenda sokoni ukakuta kwamba nyanya🍅🍅 mbili ni mia tano.
Kipindi kingine ukaenda sokoni ukakuta rundo🍅🍅🍅🍅 la nyanya la mia tano haliwezi kubebwa na mtoto👧 wa miaka mitano😂😂😂

Kwa nini?

Inasemekana kadri kitu kinavyokuwa kinapatikana kwa wingi sana, thamani yake hushuka.
Hili pia halijaacha nyuma suala zima la pesa.
Upatikanaji wake pia unaweza kuifanya ipande au ishuke thamani.

Kama kwa siku sasa umekuwa unajiuliza ni kitu gani kinafanya pesa ipande na kushuka, thamani. Naamini utakuwa unazidi kupata mwanga zaidi kila siku.
Jana tuliona sababu mbili zinasosababisha kupanda na kushuka. Leo tumeongezea moja. kesho tutaendelea pia.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X