Maeneo Matatu Unayoweza Kuwekeza Kama Hauna Pesa/Mtaji


Moja kati ya vilio vya watu wengi linapokuja suala la kuazisha biashara, basi ni kilio cha MTAJI. Utasikia watu wanasema, ningependa kuanzisha biashara fulani ila mtaji.
Ningependa kuwekeza sehemu fulani ila mtaji sina.

Kitabu Hiki Kipo Kwa Ajili Yako
Tsh.5,000/-

Kama wewe kilio chako kimekuwa hiki kwa siku sasa, naomba nikwambie kwamba kuna maeneo matatu ambayo unaweza kuwekeza kwa sasa hata kama hauna mtaji. Na maeneo haya ni kama yafuatayo:

1. Wekeza kwenye maarifa.
Hii sehemu ya kwanza kabisa unayoweza kuwekeza kwa sasa hata kama hauna senti. Hapa kinachohitajika ni wewe kujua aina gani ya maarifa ambayo unayahitaji. Ukiwekeza huku, hutakuja kuhangaika hata pale utakapopata pesa.
Hakikisha unapata maarifa juu ya elimu ya pesa.
Pata maarifa juu biashara unapenda kuifanya
Pata maarifa juu ya uuzaji
Pata maarifa juu ya uongozi.
Huhitaji kuwa na mtaji mkubwa ili upate haya yote. Unatakiwa kuwa tayari, tu inatosha.

2. WEKEZA KATIKA MAHUSIANO
Jifunze kuwasiliana na watu. Maana hata ukianzisha biashara bado, utapaswa kuwa mtu wa watu, utahitaji kuwasiliana na kuwasilisha kile ulichonacho. hivyo jambo hili hapa linakuhitaji kwa sasa uanze kuwekeza kwenye mahusiano na watu.
Jifunze lugha ya mwili inavyofanya kazi. Jifunze unavyoweza kuwasilisha kitu kwa watu na kikakubaliwa.

3. WEKEZA KWENYE MUDA
Huhitaji kuwa na pesa za kutosha ndio uanze kwenda na wakati. Muda ulio nao sasa hivi ni hazina kubwa sana ambayo haitakuja kujirudia siku zijazo. Ukipita ndio umepita. Anza kuitumia kila sekunde ijayo mbele yako kwa umakini wa hali ya juu sana. Ishi kila sekunde kama vile ndio sekunde yako ya mwisho wewe kuwepo hapa duniani. Na tenda unachofanya kama vile utaishi milele.

Soma Zaidi: Vitu Nane (08) Vya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara

Soma Zaidi: Hii Ni Njia Rahisi Ya Kuhairisha Unachopanga

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X