Hili Ni Jambo Linalowafanya Watu Washindwe Maishani


Moja kati ya swali ambalo nimekuwa najiuliza ni swali la je, ni kweli watu hawajui kile wanachofanya au wanajua kiasi kwamba wanapuuzia? Je, ni kweli kwamba masikini hawajui mbinu za kutafuta pesa au wanazipuuzia?
Je, ni kweli watu wanaoumwa hawajui kanuni za afya au wanazipuuzia?

Unadhani jibu ni lipi? Jibu ni rahisi sana WATU WANAJUA KARBIA KILA KITU. Ila kupuuzia ndiko kunawakumba.

Katika ulimwengu wa sasa hivi, ukitaka kujua  kwamba watu wanajua kanuni fulani au hawajui basi wafuatilie mitandaoni.

Soma Zaidi:  Watanzania Acheni Utani, Tamthilia Hazijengi

Kila siku mitandaoni utakuta watu wanaweka status zenye maneno mazuri sana kuhusu kanuni fulani. Utakuta watu wanaandika mazoezi ni muhimu kwa afya yako.
Vitabu ni chanzo cha maarifa. Marafiki wabaya si watu wa kufuata,  nakadhalika nakadhalika.

Hii ni ishara tosha kwamba watu wanajua kanuni hizi. Ila sasa kuziishi hapo ndipo maajabu yalipolala. Ni wangapi wanaishi kile wanachokiandika.

Ni rahisi sana kusema kitu fulani lakini kukiweka katika matendo ndipo ulipo ugumu.

Rafiki yangu kama kuna eneo ambalo hufanyi vizuri jiulize ni kwa nini hufanyi vizuri katika eneo hilo?
Je, ni kwa sababu hujui kanuni au kwa sababu unajua sana hadi unapuuzia?

Ukinenepa jiulize ni kwa nini? Ni kwa sababu hujui kwamba kula chakula bora na kufanya mazoezi ni muhimu kwako? Au kwa sababu unajua sana hadi unapuuzia?

Tatizo la watu wengi sana wanapenda kubadilisha kitu fulani kwa kingine.  Na mara nyingi haifanyi kazi.

Wanapenda kunywa soda badala ya glasi nane za maji kila siku.

Unapenda kuangalia tv badala ya dak 20 za mazoezi kila siku.

Wanapenda kuiba pesa badala ya kutengeneza mifereji na kujenga thamani ya kuivuta pesa ije kwao.

Rafiki yangu,
Kama kuna kitu unaona kabisaa unashindwa, basi jiulize ni wapi wewe unakosea kafanyie kazi kile unachokijua badala kukaa unakijua huku ukikipuuzia.

Unajua kwamba kuweka malengo ni muhimu, sasa kwa nini huweki?

Unajua kufanya mazoezi ni muhimu na haufanyi?

Unajua kusoma vitabu ni muhimu, sasa unasubiri nini?

Fanyia kazi kila kitu chanya unachojua kinafanya kazi badala ya kuendekeza kitu hasi kwenye maisha yako.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza.
0755848391.
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X