Hiki Ni Kitu Ambacho Dunia Haipungukiwi


Sio kitu cha ajabu kusikia watu wanasema kwamba kuna uhaba wa maji. Au uhaba wa chakula. Wengine utawasikia wakisema kuna uhaba wa walimu katika shule, wilaya au mkoa fulani. Cha ajabu zaidi ni kwamba kuna malalamishi ya uhaba  wa viongozi bora.

 Lakini ushawahi kujiuliza ni kitu gani ambacho hakina uhaba? Yaani uapatikanaji wake upo kwa wingi kila siku.
Kama hujawahi kujiuliza swali kama hili hapa basi naomba nikwambie kitu hiki hapa.
Kitu chenyewe kipo, na sio kingine bali Fursa. Fursa hazijawahi kuwa haba. Kila siku kuna fursa mpya. Kila unapoenda unakutana na fursa, kila unayekutana naye ni fursa. Yaani kila muda kuna fursa juu ya fursa.

Yaani kiufupi ni kwamba, fursa ni kama magari ya daladala. Likikupita hili linakuja jingine na kukubeba.  Kwa hiyo huba haja ya kukimbizana na kusema fursa imekupita. Hakuna kitu kama hicho.

Jua kwamba kila siku unazo fursa, kila sehemu unazo fursa. Na kila uendapo ni fursa.
Zitumie fursa hizi hapa. Maana siku zote fursa zipo.

Kitu cha msingi ni wewe kujua unahitaji nini katika maisha yako. Ukishajua hili basi sina shaka kuna baadhi ya vitu ambavyo wanaviita fursa havitakuhangaisha, maana wewe unajua ni wapi unaenda na kwa nini.

Huhitaji kukimbizana na kila fursa bila kujipanga. Kuwa makini jua ni wapi unaenda na kwa nini. Weka juhudi kufika kule.

Asante sana,


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X