Hii Ni Fursa Ambayo Hupaswi kuichezea


Habari ya siku hii njema sana rafik yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo, na hakikisha kwamba ndani ya siku hii ya leo unaweka juhudi kubwa sana. Hakikisha kwamba haukwami rafiki yangu wala kurudi nyuma kwa sababu yoyote ile. Wewe ni mshindi, ishi kiushindi ndani ya siku hii ya leo.

Ndani siku yoyote ile huwa kuna vitu vidogo vidgo ambavyo huwa vinajitokeza.  Vitu hivi vinaweza  kuwa vimeletwa kwetu tuvisimamie, au labda vinaweza kuwa pia tumekutana navyo kwenye kazi zetu ila vinapaswa kufanyika ili sisi tuweze kusonga mbele na hatimaye kuweza kufika kwenye kilele cha mafanikio.
Na mara nyingi sana watu huwa wanadharau vitu vya namna hii hapa. Kwa mfano mtu anaangalia kwamba yeye ni msomi sasa, kuanza kujishughulisha na kazi ndogo katika ofisi ambayo ina kipato kidogo, kwake hilo anona kwamba ni kuigiza.
Mwanafunzi anataka ahitimu chuo, papo hapo ameajiriwa kwenye kazi kubwa inayolipa mshahara mkubwa sana na amepata dereva wa kumwendesha.
Lakini ukiwambia juu ya kazi ndogo ambayo inapatikana katika kampuni fulani, basi hata hajali. Na pengine akiipata ile kazi haifanyi kwa  kiwango cha juu sana kuonesha kwamba kweli kazi hii imefanywa na mtu. Anagusa gusa tu ilimradi aonekane kwamba ile kazi ameifanya. Hivyo  haunganishi nguvu, muda na mwelekeo wake kuakikisha kwamba anafanya kazi kwa ubora wa hali ya juu sana.

Rafiki yangu hili ni kosa kubwa sana ambalo unaweza kufanya maishani. Kosa hili ni kudharau kazi hizi ndogo ndogo. Kila mara unapopata nafasi ya kufanya kazi ndogo, basi hakikisha kwamba unazifanya kwa uzuri na kwa kuweka uwezo wako wote hapo kiasi kwamba mtu atakapokuja kuitazama ile kazi, basi ajue kwamba hapa kuna mtu amefanya hii kazi.

Soma Zaidi:  Vitu Vitano Vyenye Thamani Kubwa Zaidi Hapa Duniani

Usidharau vitu vidogo hata siku moja, maana ni vitu vidogo ambavyo huchangia kutengeneza vitu vikubwa sana kwenye maisha. Hivyo usidharau vitu vidogo vidogo hata siku moja. Kama umeajiriwa, ifanye kazi yako vizuri sana kiasi kwamba kila mtu aionaye aifurahie hiyo kazi yako.
Kazi ndogo ndizo huonesha uwezo wako wa kufanya kazi kubwa.

Nilipokuwa nikiangaza katika kurasa za Biblia ndipo nilipokutana na jambo la kwamba mtu anayetimiza wajibu mdogo, hatimaye anazawadiwa kitu kikubwa zaidi ya hicho. Katika kitabu cha Mathayo imeandikwa hivi
Vema mtumwa mwema na mwaminifu, ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi, ingia katika furaha ya Bwana wako.
Hivyo rafiki yangu nazidi kukusisitizia kwamba hata siku moja usidharau jambo dogo ambalo wewe unapaswa kulisimamia. Iwe ni la kwako binafsi au la mtu mwingine amekuweka ulisimamie. Lisimamie vizuri sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X