Hivi Ndivyo Unaweza Kusoma Kitabu Kwa Wiki Moja (Mbinu Nne Za Uhakika)


Habari ya siku hii njema sana ya Leo rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo na ya kipekee sana kuwahi kutokea katika dunia hii.

Siku hii ya leo naomba tuangalie ni kwa jinsi gani unaweza kusoma kitabu kwa wiki moja.

Moja kati ya changamoto ambayo watu kwa sasa wanayo ni kutosoma. Kila Mara unapoongea na watu watakuambia kwamba hawana muda wa kuwatosha kusoma vitabu. Wengine watasema usomaji wa vitabu sio hobby na hivyo hawawezi kujishughulisha na usomaji.

Ila ukweli ni kwamba kusoma kitabu ni jambo la muhimu sana kwa MTU yeyote ambaye anaishi katika dunia hii na haswa katika zama hizi ambazo dunia ina badilika kila siku.

Hapa hauna jinsi isipokuwa kuhakikisha unakaa chini unachukua kitabu na kusoma.

Lakini pia kwa mtu ambaye ameajiriwa au ameajiajiri. Ili uweze kuongeza kipato chako Mara mbili basi utapaswa kusoma vitabu mara tatu zaidi ili maarifa ya kufanya kazi yako kwa ubora wa hali ya juu yaongezeke.

Sasa bila shaka mpaka hapo utakuwa unajiuliza nawezaje kusoma kitabu kwa wiki ili niweze kuongeza ujuzi wangu kwa kiwango cha juu na kuwa na Maarifa ya kutosha.
Basi hapa ninakuja na mbinu zifuatazo ambazo zitakusaidia.

Soma Zaidi; A NOTE FROM SONGAMBELE; Mitandao Ya Kijamii

1. Chagua aina ya kitabu ambayo unahitaji kusoma.
Katika dunia hii kuna aina nyingi sana za vitabu. Huwezi kusoma kila kitabu. Ila unaweza kusoma vitabu vinavyoendana na uwanja wako wa kazi au uwanja unaoufurahia kuufuatilia. Mfano Mimi uwanja ninaoufutilia ni uwanja wa biashara na ujasiliamali. Hivyo nawekeza nguvu kubwa sana katika kuhakikisha kwamba kila siku ninasoma kitabu kinachohusu biashara, ujasiliamali au uwekezaji.

Na kwa kuwa mimi kikazi ni mtaalamu wa kilimo basi pia na huku lazima niwekeze muda kuhakikisha nasoma vitabu vya aina hii.

NB; Vitabu ambavyo huhitaji kuacha kwenye kusoma ni vitabu vya maendeleo binafsi. Hata kama utasema hauna vitabu vya kusoma basi hakikisha kwamba unasoma vitabu vya maendeleo binafsi. Vitabu hivi vinaweza kuwa vinahusu malengo, vipaji,n.k

Soma Zaidi; KITABU; NYUMA YA USHINDI

2. Chukua kitabu kimoja cha kuanza nacho
Baada ya kuchagua aina ya vitabu ambavyo sasa unahitaji kusoma, baada ya hapo chagua kitabu kimoja tu ambacho utaanza nacho.
Je, tayari umekichagua.
Kitafute hiki kwanza. Kama hapa  unapata shida basi wasiliana na mimi Mara moja ili nikwambie wapi utaweza kukipata kitabu chako.

3. Anza kukisoma mara moja.
Haitoshi tu wewe kuchagua kitabu na kutulia. Sasa baada ya hapo nini?
Endelea kusoma kitabu hiki. Tenga muda maalumu hata dakika kumi za kusoma.kitabu hiki kila siku. Ila Itapendeza zaidi kama utakuwa na muda ambao ni kati ya nusu SAA na SAA zima.

Na SAA hili utaweza kulipata kama utaweza kuamka mapema kila siku.

4. ENDELEA KUSOMA
Haitoshi tu wewe kuanza kusoma kitabu na kuacha, bali hakikisha unakianza na kukifikisha mwisho. Usiishie tu kuanza kusoma kitabu. Kimalize.

Kama utaweza kusoma hivi kila siku kitabu chako na kukiwekea nguvu kwa zaidi ya nusu SAA. Nina hakika ndani ya muda huo unaweza kusoma kurasa zisizopungua kumi na tano.
Sasa hapo napiga hesabu kurasa kumi na tano kila siku ni sawa na kurasa 105. Hiki ni sawa na kitabu cha kawaida chenye kurasa 100.

Hapa utakuwa umefanya kazi njema sana rafiki yangu. Ebu anza kulifanyia kazi suala hili hapa bila kuhairisha.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
(Songambele)
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

KUPATA KITABU CHA TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X