Hiki Ni Kiwango Cha Uharaka Kinachopendwa Sana Na Watu


 Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Imani yangu leo ni siku njema sana.

Dunia ya sasa hivi imekuwa ni dunia ya kasi sana. Kwa sasa watu wanapenda sana vitu vya kasi kuliko wanavyopenda kitu kingine chochote. Katika dunia ya sasa hivi kasi ni kitu ambacho kinaongelewa kila mahali. Ndio maana utasikia baadhi ya makampuni yakijinadi kwamba “4G ndio mpango mzima”. Wengine utawasikia wanasema hapa kasi tu, n.k

Hii ni kutokana na ukweli kwamba ulimwengu wa sasa ni wa haraka wala hauna huruma kwa mtu anayejikokota.

Ndio maana wewe ukifungua mtandao kama unagoogle kitu kikachelewa utaona mtandao unakuchelewesha sana. Unaweza hata kuacha kutafuta kitu ulihokuwa unatafuta kama, kitazidi kuchelewa.

Ingawa ulimwengu ni wa haraka lakini lazima tuwe na kipimo halisi kitakachoatuambia sasa umeenda kasi au umechelewa. Na kipimo hiki ni kimoja tu.

Pale mteja wako anapopata bidhaa na kuipata mkononi mwake hapo utakuwa umeenda kasi,
Lakini kama ataihitaji ikachelewa basi utakuwa haujaenda kasi, hilo tu.
Kwa hiyo kiufupi kipimo cha uharaka ni uwezo wako kuifikisha huduma yako kwa jamii ndani ya muda kinapohitajika.

Je, wewe bidhaa zako zinamfikia mteja wako muda gani baada ya yeye kuiomba.

Chagua kwenda kwa kasi rafiki.

Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X