KITABU NYUMA YA USHINDI;


habar, kitabu cha nyuma ya ushindi, kimezinduliwa rasimi tangu juzi, na mpaka sasa hivi  unaweza kukipata popote pale ulipo duniani. hapa nimekuwekea utangulizi wa kitabu cha NYUMA YA USHINDI
Mara nyingi sana inapozungumziwa historia ya watu waliofanikiwa kiuchumi, kimahusiano, kisiasa, kijamii n.k basi huwa inaoenekana ni ya kusisimua sana. Maana historia hii huwa inazungumziwa katika namna ambayo ni ya kusisimua. Mfano unaweza kukuta historia ya mtu kama Bill Gates inazungumziwa kwa namna hii, “aliacha chuo na kwenda kuanzisha kampuni ya Microsoft, sasa hivi ni bilionea”. Au mwingine anamzungumzia Mark Zuckerberg kwa namna kama hii, “alianzisha facebook, akiwa chuo, akaacha chuo na sasa hivi ni bilionea”. Ingawa kauli zote za watu hawa wawili ni kauli nzuri sana na sahihi. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu aliyeweza kufika hapo aliofika kwa siku moja. Sio kweli kwamba tu mara baada ya Mark Zuckerberg kuacha chuo aliibukia kuwa milioea na bilionea ndani ya siku chache. Kuna mchakato uliokuwa ukifanyika mpaka kufikia ushindi.Na mchakato huu ambao huwa unafanyika kabla ya ushindi au mafanikio kuonekana upo nyuma ya ushindi, au watu muda mwingine unaweza kusema kwamba NYUMA YA PAZIA. Kuna vitu ambavyo huwa havionekani na watu wengi sana huwa hawapendi kuviongelea. Vitu hivi huwa vinatokea nyuma ya PAZIA LA USHINDI. Sasa kitabu hiki hapa kimelenga kukuletea vitu hivyo ambavyo huwa vinatokea nyuma ya pazia la ushindi. Moja ya vitu hivi ambavyo huwa vinatokea nyuma ya ushindi ni kushindwa. Basi kitabu hiki ambacho ni kitabu cha kwanza kwenye mfululizo wa vitabu vya nyuma ya ushindi kimelenga kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha kwamba kinaeleza kitu kimoja ambacho huwa kinatokea nyuma ya ushindi yaani KUSHINDWA.
Imani yangu kwamba utafaidika na kitabu hiki ambacho kimendikwa kwa kutumia mifano ya kila aina ili kukujengea picha halisi ya kile ambacho huwa kinatokea nyuma ya ushindi.
Mwisho ninategemea uchukue hatua baada ya kusoma kitabu hiki, ili na wewe uweze kufika kule ambapo unataka kufika kwa kuiga na kujifunza kwa mifano ya watu walioshindwa! Naomba nimalizie kwa kusema kwamba NYUMA YA USHINDI  KUNA KUSHINDWA, KUSHINDWA, KUSHINDWA. Asante sana tukutane kileleni



2 responses to “KITABU NYUMA YA USHINDI;”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X