TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-137 Tatizo hutaki kujidogosha


Kuna mwendeshaji mmoja wa baiskeli aliyekuwa anapita mahali na baiskeli yake. Alipofika eneo husika aliona kwamba kulikuwa kuna wanajeshi ambao walikuwa wanajaribu kuondoa kisiki bila mafanikio. Nyuma ya wale wanajeshi alikuwepo mtu mmoja aliyakuwa amesimama tu! Yule mwendesha baiskeli alimwulilza, inakuwaje rafiki yangu, mbona wewe huwasaidii watu hawa wakati unaona kwamba wanahangaika kuondoa kisiki”. Yule mtu aliyekuwa amesimama akasema kwamba mimi ni kamanda wa kikosi hivyo kazi yangu ni kutoa amri na hawa kuteleleza. Basi alichokifanya  yule mwendesha basiskeli ili kuwa ni kuweka baiskeli yake pembeni na kuanza kuwasaidia wale watu waliokuwa wakikiondoa kisiki. Alipojiunga mwendesha baiskeli uondoaji wa kisiki ukawa rahisi sana na kikondolewa muda huo huo. Yule mwendesha baiskeli akageuka na kumwona yule kamanda bado amesimama. Akamwambia kwamba siku nyingine wanajeshi wako wakikwama basi mwite mkuu wa majeshi awasaidie. Baada ya hapo mwendesha baiskeli akaondoka. Baada ya muda kidogo ndipo wanajeshi na yule kamanda walikuja kugundua kwamba yule mtu aliyewasaidia kuondoa kisiki alikuwa ni GEORGE WASHINGTON, ambaye ni mkuu wa majeshi wa nchi hiyo.
Somo la kibwagizo hiki kifupi li wazi sana.
#1. Kuna nyakati unapaswa kujidogosha na kuchapa kazi, bila kujali cheo chako. Yaani hapa achana na ule kwamba mimi ndio mimi.
#2. Sio kila sehemu unapoenda uanze kujitapa kwamba mimi ni mtu fulani, mnanionaje. Ila vitendo vina uwezo wa kuongea zaidi ya wewe unavyoongea.
#3. Sio mpaka uambiwe saidia ndipo uanze, ila ukiona kwamba kuna uhitaji basi cha kufanya saidia hapo dunia itakulipa tu!
#4. Kiongozi mzuri sio yule anayenyoosha kidole na kuwaambia watu fanya hiki na acha kile, kiongozi mzuri ni yule ambaye anafanya kazi na kuwa mtari wa mbele na kuwaacha watu wamfuate nyuma yake.
Hayo ndio machache ambayo nimeona nikushirikishe rafiki yangu wa karibu sana kwa siku hii ya leo. Tukutane kesho.
Jipatie kitabu chochote kile kwa bei ya shilingi 10,000/- leo ili upewe kitabu kingine kimoja cha ziada bure.
Yaani ukinunua kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI au TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA  kwa bei tajwa hapo juu utapewa zawadi ya kitabu kinngine kimoja cha ziada cha NYUMA YA USHINDI. Lipia pesa kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA, baada ya hapo nitumie ujumbe wenye email yako ili nikutumie kitabu ambacho utakuwa umenunua.
Kama tayari una vitabu vyangu vyote viwili ila unahitaji kupata zawadi hii ya kitabu cha NYUMA YA USHINDI basi cha kufanya, jiunge nami ndani HAZINA YETU TANZANIA, ambapo utapata vitabu zaidi vya Kiswahili vya kujisomea bure kwa miezi mitatu mfululizo. Yaani mwezi wa tatu utapata kitabu, mwezi wa nne kingine, mwezi wa tano utapata kitabu kingine na wa sita nao. Kujiunga na hazina yetu Tanzania unalipia ada ndogo ya  mwaka mzima ambayo ni 20,000 TU! Pesa yote itumwe kupitia nambari ya simu 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.

Kitabu cha zawadi kitatumwa rasmi tarehe 4 machi. Ila mwisho wa wewe kujiunga na kuwa kwenye orodha hii ni tarehe 1 machi. Karibu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X