TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-120 Tatizo hujajua vitabu vya msingi vya kusoma


Kusoma na kujifunza kunaweza kukufanya kuwa jinsi unavyotaka. Kunaweza kumgeuza mtumwa kuwa kiongozi, kunaweza kumwinua kilaza kuwa gwiji, kunaweza kumnyayua aliyelala na kumsimamisha. Mbali na ukweli huo hapo ni watu wachache sana ambao huwa wanachukua hatua kuhakikisha kwamba wanaweza kusoma na kujifunza ili kuweza kuchukua hatua madhubuti za kuwafikisha kule ambako wanataka.
Leo hii uko kama ulivyo, lakini hautaendelea kuwa jinsi ulivyo miaka kumi ijayo kama utakuwa mtu wa kujifunza na kuongeza maarifa. Maarifa haya yapo na yanapitikana kwa njia mbali mbali. moja ya njia ambayo inafanya maarifa yaendelee kupatikana ni njia ya vitabu. Kitabu kimoja tu kina uwezo wa kukubadili na kukufanya wewe kuwa wewe, siku zote za maisha yako. hivyo njia nzuri ya kuishi maisha ambayo unayataka kuyaishi ni kuhakikisha kwamba unajifunza kutoka kwenye vitabu. Kuna vitabu vingi sana vya kusoma katika dunia hii hapa lakini pia wewe hapo unakuwa na uhuru wa wewe kuchagua ni aina gani ya kitabu usome na ni aina gani ya vitabu haupaswi kusoma. Vitabu vipo vingi sana hapa duniani. Kwa leo hii ningekushauri usome vitabu hivi viwili ambavyo vitabadili mwelekeo mzima wa maisha yako. vitabu hivi ni;

#1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
Hiki ni kitabu bora kabisa kwa karne hii ya 21. Mwandishi wa kitabu hiki (ambaye ndiye mimi hapa GODIUS RWEYONGEZA). Amekuwa akijiuliza kwa siku nyingi sana maswalil mengi sana kama haya hapa,
Kwa nini katika jamii moja kuna watu waliofanikiwa na watu ambao wana maisha ya chini?
Inakuwaje kuna baadhi ya watu wenye mahusiano mazuri na wengine mahusiano yao yanalega lega?
Kwa nini baadhi ya watu wana uwezo wa hali ya juuu sana kuingia kwenye kundi la watu na kuanzisha mahusiano na mtu yeyote wakati huo huo kuna watu hata wanaogopa kuonekana mbele ya watu?
Inakauwaje katika jamii majina ya baadhi ya watu yakiongelewa kila mtu anajua kitu gani kinaongelewa na wengine ukiongelea majina yao hata hakuna mtu ambaye anayewafahamu?
Katika kujibu maswali haya na mengine mengi kama ambavyo yameainishwa ndani ya kurasa za kitabu, basi mwandishi amekukandalia kitabu ambacho unaweza kukisoma ukiwa nyumbani kwako kitandani kabisa umelala. Unachohitaji ni kuwa na simu jaja (smartphone) au kipakatio (kompyuta). Hilo tu. Hapo utaweza kusoma na kujifunza mambo ya msingi sana ambayo yamo ndani ya kurasa za KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
#2. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA
Kitabu cha pili ambacho unahitaji kuhakikisha kwamba unakisoma kwa umakini wa hali ya juu sana ni kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.   Ndani ya kurasa za kitabu utakutana na mtazamo mpya kabisa wa kuyatazama mambo ambayo yanaendelea katika dunia hii.
Hiii ni kutokana na jinsi ambavyo watu wamekuwa wakipokea na kuvichukulia vitu. Mfano kwa siku sasa kumekuwepo na msimamo wa baadhi ya watu kwamba umasikini ambao umeenea katika bara la Afrika chanzo chake ni wakoloni wa kizungu. Watu wanaosema hivi wanaendelea kwa kusema kwamba rasilimali zilizoibiwa kipindi kile, ikiwa ni pamoja na watu waliochukuliwa kama watumwa, madini, wanyamapori, kutaja ila vichache ndivyo vingeweza kulifanya bara la Afrika tajiri. Kadri ya watu hawa, RASILIMALI ZILIZOPOTEA KIPINDI KILE NI CHANZO CHA UMASIKINI  KWAO. Hata hivyo ndani ya kurasa za kitabu hiki utapata mtazamo wa tofauti. Ambapo mwandishi moja kwa moja anasema hivi “TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.
Sasa kama TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA, tatizo ni nini?
Ndani ya kurasa za kitabu hiki hapa mwandishi ameelezea vitu zaidi ya 50 ambavyo ukivibadilisha wewe hapo, basi maisha yatabadilika.
Je, nitavipataje vitabu hivyo?
Sasa unaweza kujipatia vitabu vyote hapo kwa bei ya zawadi, kwa vitabu vyote viwili. Yaani unaweza kuvipata kwa bei ya zawadi ambayo ni 14,000 badala ya 20,000.  Pesa hiyo utailipia kupitia nambari ifuatayo, 0755848391 Jina GODIUS RWEYONGEZA.
Bei ya kitabu kimoja kimoja ni  #KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI ni 8,000 badala ya 10,000  na TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ni 6,000 badala ya 10,000.
Kama unahitaji kitabu kimojawapo unaaweza pia kulipia kupitia nambari hiyo hiyo hapo juu.
Baada ya kulipia nitumie ujumbe wa njia ambayo ungependa mimi nikutumie vitabu hivi. Ambapo unaweza kuchagua njia mojawapo kati ya hizi hapa, email, wasapu au telegram. Kitabu kitakufikia muda mfupi sana baada ya wewe kutuma pesa. Na vitabu vyote ni SOFT COPY.
 karibu sana.

NDIMI, GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X