TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-118 Tatizo unakamuliwa na muda



Haijalishi unaishi katika sehemu gani hapa ulimwenguni, kitu kikubwa ambacho kinakuunganisha wewe hapo na watu wengine wote ambao umewahi kukutana nao na wale ambao hujawahi kukutana nao maishani mwako ni kwamba nyote mnakuwa na masaa 24. Basi! Hiki ni kiunganishi kikubwa sana ambacho kinakuunganisha wewe hapo na watu wengine wote. Hakuna mtu mwenye muda zaidi ya mtu mwingine na hakuna mtu mwenye muda kidogo ya mtu mwingine. Binadamu wote wana muda sawa. Nafikiri mtu aliyesema kwamba binadamu wote ni sawa moja kati ya vitu ambavyo alikuwa akiangalia ilikuwa  ni muda. Maana hakuna binadamu ambaye amewahi kuwa na muda mwingi zaidi ya mwenzake na hakuna mtu ambaye amewahi kuwa na muda kidogo zaidi ya mwingine. Yaani watu wote wanakuwa na muda sawa sawia. Mbali na ukweli huu kwamba watu wote tunakuwa na muda sawa, bado kunakuwa na tofauti kwenye matumizi ya muda. Wakati wapo ambao wanautumia muda ule ule ambao watu wote wanao kuhakikisha kwamba wanaweza kufanikiwa na kupiga hatua kubwa sana, wapo wanaoutumia muda huo huo kujirudisha nyuma na kujiangusha.

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwa nini kuna baadhi ya watu wamefanikiwa na kuweza kutengeneza utajiri  mkubwa sana wakati huo huo kuna watu wanalia? Ingawa ukweli ni kwamba watu wale wale wanakuwa  wametokea kwenye mazingira yale yale lakini bado watu hao sio sawa katika suala la ukuzaji wa vipaji vyao na mafanikio . Linapokuja suala zima la muda huhitaji kupiga mazoezi ya mgambo, bali unapasawa kuhakikisha kwamba unautumia muda wako kadri ya uwezo wako. Utumie muda sio muda ukutumie wewe na kukwambia wewe unapaswa kwenda wapi. Ikumbukwe kwamba muda ni moja kati ya rasilimali tatu ambazo kila binadamu anazo bure kabisa. Na ni rasilimali ambazo wewe hapo unaweza kuanza nazo katika kuhakikisha kwamba unaanza safari yako. rasilimali nyingine ni akili na nguvu (MAELEZO ZAIDI JUU YA RASILIMALI HIZI YAPO KWENYE KITABU CHA TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA). Ili kuweza kukuza ubunifu na vipaji vilivyo ndani yako suala zima la matumizi ya muda wako ni muhimu sana. tena muda unahitaji kuutumia kwa nidhamu ya juu sana kama ambavyo unatumia pesa yako kwa nidhamu.  Usiutumie muda wako kufanya kila kitu. Bali hakikisha kwamba unautummia muda wako kufanya kazi za msingi sana ambazo zinaboresha na kukuza ubunifu wako. Watu wengi sana wanalalamika haswa wanapokuwa wameajiriwa kwamba wao hawana muda wa kuwatosha kuweza kuendeleza ubunifu na vipaji ambavo wanavyo. Hivyo  ndani ya msaa 24 ya kila siku wanachokifahamu ni kwamba wao wanaenda kazini kwa bosi na kufanya kazi ya ajira. Hakuna kazi nyingine ambayo wanaifahamu. Jambo hili hapa si jambo la kuunga mkono hata kidogo, kwa sababu kuna watu wanapoteza ubunifu na hawatoi kile ambacho wanacho kwa sababu tu ya uzembe. Kama ambavyo nimesema hapo awali ni kwamba hakuna mtu mwenye muda mwingi zaidi ya mtu mwingine. Hivyo suala hili liko hivi na litabaki kuwa hivi hivi kwa siku nyingi sana. kitu kikubwa sana ni kuhakikisha kwamba muda uliopo unatumiwa vizuri kwa viwango vya hali ya juu sana. na hapa ndipo unapaswa kupunguza kazi au shughuli ambazo si za lazima ndani yako ambazo hazikuruhusu wewe hapo kuweza kuendeleza na kuibua ubunifu ulio ndani yako rafiki yangu. Chukulia mfano wa mfanyakazi ambaye anaenda kazini asubuhi saa moja na jioni saa kumi kutakiwa kutoka kazini. Mtu huyo huyo analalamika kwamba hana  muda wa kutosha, je hii ni kweli. Unakwenda wapi muda huu wa kuanzia saa kumi na dakika moja mpaka anapoeda kulala. Tena ukija kufuatilia Utagundua kwamba hata yeye halali mapema, utakuta kwamba analala saa saba na pengine saa nane za usiku. Sasa  ndani ya muda huu mwingine anakuwa wapi na anakuwa anafanya nini? Kumbe hapa ndipo  utagundua kwamba matumizi ya muda wake sio ya ukomavu, bali anatumia muda wake kizembe sana. Yaani unakuta kwamba anakuwa na muda wa kwenda kupiga soga na rafiki zake, mara anakuwa na muda wa kuongea na simu kwa zaidi ya masaa matatu. Wakati huo huo anakaa chini na kuangalia tamthiliya za Kikolea mpaka saa saba au saa nane. Hivi kweli mtu akikwambia kwamba hana muda utamwabiaje?  Basi unapaswa kuhakikisha kwamba unaepukana na mtego huu mbaya ambao unaweza kujiingiza katikati ya safari yako. Na ili uweze kuodokana na mtego huu basi unapaswa kuhakikisha kamba unaamua kufanya mazoezi ya kukuongezea wewe thamani maishani mwako. Kiukweli ni kwamba wewe upo zaidi ya ulivyo sasa hivi. Na kama huo ni ukweli usiopingika basi huna budi kuhakikisha unakuwa wewe mweneyewe haswa kwa kutumia muda wako ambao unao ndani ya masaa 24 ya kila siku. Hakuna sifa hata chembe ya wewe hapo kuzembea kutumia muda wako ambao unao ndani ya masaa 24 ya kila siku.  Utumie muda wa sasa hivi kwa manufaa ya kesho

Suala ambalo huwa linajitokeza katika kutumia muda ni pale mwili wako unapokwambia kwamba , acha kuutesa sana mwili wako maana raha ni sasa hivi, hiyo sauti si ya kusikiliza. Nmegundua kwamba watu walioweza kufikia  hatua kubwa sana katika kutumia vipaji vyao sio watu ambao wanajizuia. Sio watu wanapenda raha za muda mfupi sana, bali ni watu ambao wanahakikisha kwamba wanautumia muda wao kwa viwango vya hali ya juu sana kuelekea kule ambapo wao wanataka.

SWALI LA KUJIULIZA KILA SIKU.
Kumbuka kwamba unapasawa kuishi ndani ya siku mpya kama vile hiyo ndiyo siku pekee ambayo unayo hapa duniani. Hivyo kila siku unapoamka asubuhi swali la muhimu sana ambalo unahitaji kujiuliza ni je, nitautumia muda wangu wa siku hii ya leo kufanya kitu gani? Kuna citu vingi sana ambavyo unaweza kufanya ndani ya siku yako. lakini sio vyote vyenye umuhimu kwako kwa ajili ya maendeleo na mafanikio yako. hivyo chagua vitu vichache sana ambavyo vinakuwa na mchago mkubwa sana.  moja kati ya vitu ambavyo hupaswi kusahau ndani ya siku yako ni kuendeleza kipaji chako. Hiki ni kitu cha msingi sana ambacho hupaswi kuacha na kufumbia macho. Usiruhusu mtu akuingilie katika matumizi ya muda wako wa kila siku. Na kiukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuuigilia muda wako. Wewe peke yako t ndio mwenye uwezo mkubwa sana wa kuweza kuuingilia muda wako. Unaweza kuruhusu muda wako uingiliwe na watu au ukaamua kuutumia vizuri. Sasa je, unafanyaje leo katika kuhakikisha kwamba unautumia muda wako ambao unao ndani ya siku hii ya leo?

UWANJA NI WAKO
Wachezaji wa mpira wa miguu wakiingia kiwanjani, huwa wana muda wa dakika 90 za kufanya mabadiliko. Ndani ya masaa hayo huwa wanaweza kuutumia muda huo vizuri sana kuhakikisha kwamba wanaweza kufunga timu pinzani. Binafsi mimi sio shabiki wa timu za mpira. Ila niliwahi kuwa shabiki wa timu ya yanga kwa siku za nyuma. Kipindi  hicho nikifuatilia mpira, kama timu ilikuwa inafunga timu pinzani dakika za mwanzoni basi timu hiyo ilikuwa inasemekana kwamba inaweza kufanya vizuri maana watakuwa wamewawatoa wapinzani wao kwenye mchezo. Japo sio kweli kwamba siku zote timu za mpira hufunga mwanzoni , kuna siku na nyakati timu huwa zinaacheza mpaka dakika ya 89 bila kufungana. Ndani ya kipindi ambacho kunakuwa hakuna timu iliyoweza kuona lango la timu pinzani huwa hakuna hata mchezaji mmoja ambaye huwa anaacha kucheza kwa sababu tu hawajafunga, bali kila mchezajji huwa anahakikisha kwamba anautumia muda wote wa yeye kuwa uwanjani vizuri.  Kumbe na wewe haupaswi kusema kwamba nitatumia muda kidogo sana kuendeleza kipaji changu na baada ya hapo nitaendelea na tabia zangu. Wala usiseme kwamba nitafanya kwa siku kidogo baada ya hapo nitaacha. Hasha, sio kweli. Ukiachia dakika ya 20 dakika sabini unakuwa unamwachia nani? Kumbe unatakiwa kuhakikisha kwamba unautumia muda wako vizuri kila siku. Na unapaswa kuutumia haswa, pale unapokuwa umepanga kufanya jambo fulani. Ikumbukwe  kwamba sio magoli yote hufungwa ndani ya dakika ya kumi za mwanzoni. Kuna magoli huwa yanafungwa ndani ya dakika moja ya mwisho, na mengine huwa yanafungwa ndani ya sekunde  moja ya mwisho. Lakini ni magoli ambayo huwa yana umuhimu mkubwa sana na huwa yanaipatia timu ushindi wa hali ya juu sana. kama ni kombe la dunia timu itahesabika mshindi kwa sababu tu imeweza kufunga goli moja na la kipekee, ndani ya dakika ya 90. Goli hilo moja tu litaipa timu ushindi na heshima ya hali ya juu  sana. dunia nzima itakaa na kuweza kusema kwamba timu hii  ni bingwa kwa sababut tu imeweza kufunga goli ndani ya dakika 90.
Ninachojaribu kuelezea na kusisitiza hapa kwa kutoa mifano yote hii ya kimichezo ni vitu viwili ni
1.     Usiache kufanya na kutimiza ndoto yako ya kiubunifu na kuinua kipaji chako dakika za mwanzo. Hakikisha unaendelea kwa sababu ushndi kuna wakati huwa unachelewa kufika ila huwa ukifika basi jua kwamba umefika. Na tofauti ya muda kidogo sana huwa inaleta matokeo makubwa sana maishani.
Katika maisha baadhi ya watu walioacha kufanya vitu wameacha muda kidogo kabla ya wao kuweza kufikia hatua waliyokuwa wanakusudia na wameisubiri kwa siku nyingi sana.
Endelea kupiga hatua mpaka kieleweke.
2.     Muda wako ni muhimu sana ukautumia vizuri, masaa 24 hayajengwi kwa matofali, bali masaa 24 yanajengwa kwa sekunde moja.
3.     Ukitaka kujua umuhimu wa sekunde moja muulize mchezaji wa timu ya mpira ambayo imefunga dakika za mwanzo na wamekuja kufungwa dakika ya 90.
Umekuwa nami,
GOIUS RWEYONGEZA
($onga mbele)
Tuwasiliane,
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

Sasa unaweza kujipatia vitabu  vyangu vyote kwa bei  yz zawadi. Hahahah! Hii inaitwa ya kwako tu! Unaweza kupata vitabu hivi hapa kwa shilingi 14,000/- badala ya 20.000/- cha kufanya,  lipia kupitia nambari  0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo nitumie ujumbe wa kuniambia ni njia gani ambayo ungependa mimi hapa nikutumie vitabu. Vitabu vunatumwa kwa njia ya email wasapu au telegram. Karibu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X