USIOGOPE KUSHINDWA


 
Kushindwa ni moja ya jambo ambalo lipo katika njia ya kuelekea katika mfanikio. Bila shaka utakuwa umesikia mara nyingi sana maneno kama wewe ni mshindi, umezaliwa mshindi, na maneno mengine mengi sana. Haya maneno yapo sahihi kwa asilimia kubwa sana. Ila mbali na kwamba kweli wewe umezaliwa mshindi na umezaliwa kushinda bado katika njia ya mfanikio kuna kitu kinaitwa kushindwa. Ila leo hii nakwambia kwamba usiogpe kushindwa kwa sababu tu kushindwa ni njia ya wewe kuelekea katika mafanikio. Kushindwa ni njia nzuri ya wewe kujifunza kile ambacho hapo awali ulikuwa hujui. Kushindwa ni somo ambalo maisha yanapata kukufunza na huwezi kujifunza sehemu nyingine tofauti na na kulikuta katika njia ya kufanya. Hivyo kupende sana kushindwa.
 
KWANI NIKIOGOPA KUSHINDWA ITAKUWAJE?
 
Bila shaka utakaa chini na kuanza kujiuliza, je nikiogopa kushindwa mambo yangu yatakuwaje? Jibu la haraka ni kwamba pale utakapoogopa kushindwa maana yake utaogopa kufanya. Na kama hutafanya basi utabaki jinsi ulivyo. Na katika hali ya kawaida ni kwamba ukiamua kubaki jinsi ulivyo maana yake ni kwamba unajipoteza, kwa sababu hata dunia yenyewe tu huwa haibaki jinsi ilivyo. Yaani huwa inabadilika kila wakati kwa kujizungusha kwenye mhimili wake. Lakini pia kila wakati huwa inalizunguka jua. Kwa hiyo hakikisha kwamba unachukua na kamwe,kamwe usiogope hata chembe ya kushindwa.
 
SOMA ZAIDI;Haya Ndio Maneno Yanatumiwa Na Watu Linapokuja Suala La Pesa
 
 KWA NINI SASA SIPASWI KUOGOPA KUSHINDWA?
 
Hupaswi kuogopa kushindwa kwa sababu kama umejiwekea lengo na lazima kuna siku litakuja kutimia tu. Siku zote malengo makubwa huwa hayatimii kwa siku moja. Yaani kama wewe una ndoto kubwa sana, ndio kusema kwamba haziwezi kutimia ndani ya siku moja, zitachukua muda. Kuna wakati mambo yataenda vizuri sana, kuna wakati utakutana na miinuko lakini pia kuna wakati kuna wakati utaingia katika makorongo. Haya yote ni sehemu yako ya wewe kuendea mafanikio. Hizi ni ngazi za kupanda na kutoka sehemu moja na kwenda sehemu inayofuata.

 

Namalizia kwa maneno mawili yanayosemakwamba USIOGOPE KUSHINDWA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X