Nguzo Tano Za Masoko


Moja kati ya somo la muhimu sana ambalo mjasiliamali anahitaji kuhakikisha kwamba amelifahamu kwa undani na kujifunza somo hilo ni kuuza.  Maana mara nyingi sana watu huwa wanaweka nguvu nyingi sana katika kuhakikisha kwamba wameweza kuzalisha bidhaa mpya. Lakini hata kama utazalisha bidhaa mpya ambayo ni nzuri kiasi gani, bila kuiuza bidhaa hiyo basi jua kwamba kuna kitu ambacho utakuwa unakikosa.
Na ili uweze kuiuza bidhaa yako lazima kuwe na vitu ambavyo wewe hapo unavifahamu. Vitu ambavyo vitakujengea msingi na kukufanya uweze kuwa imara zaidi. Katika makala hay animzezungumzia ktu kinachoitwa nguzo tano ambazo unahitaji kuzifahamu ili uweze kuuza bidhaa zako vizuri. Nguzo hizi ni mwongozo kwa masoko yako. Nguzo hizi ni njia nzuri sana ya wewe hapo kuhakikisha kwamba unaweza kufikia kwenye mafanikio kibiashara.

#1. NGUZO YA KWANZA; BIDHAA
Ili uweze kuingia katika soko na kuuza lazima uwe na bidhaa. Kitu kikubwa sna ambacho kinauzwa katika soko lolote lile ni bidhaa. Bidhaa hii inaweza kuwa inashikika au kuonekana kwa macho kama vile kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Lakini pia bidhaa hii inawezekana ikawa haionekani kwa macho ila ipo. Mfano wa bidhaa ambazo hazionekani kwa macho ni huduma za ushauri. Ushauri juu ya masula ya kijasiliamali, ushauri juu ya masuala ya kiafya na kadhalika. Hizi zote ni aina za bidhaa ispokuwa ni kwamba zinatofautiana kwa ufanano wake. Je wewe unayo bidhaa ya kupeleka sokoni?
#2. NGUZO YA PILI; BEI
Hata kama bidhaa yako ni bora sana kiasi gani lakini kama itakuwa na bei ya  juu sana itachukua muda kwa bidhaa yako kusambaa na kuwafikia walengwa wako. Hivyo hakikisha kwamba unapokuwa na bidhaa yako unahakikisha kwamba umeweka bei ambayo inaendana na wateja wako.
#3. NGUZO YA TATU; SEHEMU
Hakikisha kwamba wateja wako wanajua wewe hapo uko maeneo gani. Kiasi kwamba wakitaka kuja kwako wajue ni wapi wanafikia. Kwa zama za sasa huitaji kuwa umepanga au unamailiki nyumba kubwa sana. Simu yako inakutosha wewe hapo kutengeneza sehemu yako katika mtandao  ambapo watu watakuwa wanakuja na kukuta bidhaa yako. Je wewe watu wakitaka kujawatakukuta wapi?
#4. NGUZO YA NNE; MATANGAZO
Bila sha ka umewahi kusikia kwamba biashara ni matangazo.  Hivyo na wewe unapaswa kuhakikisha kwamba unajitangaza kila siku . Iga mfano wa makampuni ya simu. Kuna baadhi ya makampuni ambayo yameenea katika maeno mengi sana hapa nchini. Lakini cha kushangaza ni kwamba makapuni yale bado yanazidi kujitangaza kila siku. Hivyo na wewe unapaswa kuhakikisha kwamba unajitangaza kila siku. Hakikisha kwamba kila mtu ambaye anapita katika mazingiara yako anajua kwamba wewe hapo ni nani na una huduma gani ambayo anaweza kuipata kutoka kwako.
#5. NGUZO YA TAJNO: WATU
Watu ni muhimu sana katika biashara yako. Kuna watu ambao wanaweza kuwa sehemu ya biashara kutokana na jinsi ambavyo wanauza bidhaa yako, jinsi wanavyoitangaza bidhaa yako na jinsi ambavyo wanawapokea wateja wako. Hivyo unapaswa kuhakikisha kwanza unakuwa na timu sahihi ya watu ambao wamekuzunguka. Lakini pia unapaswa kuhakikisha kwamba unatafuta watu wapya kila siku. Watu wa kununua bidhaa zako, watu wa kuwekeza na watu ambao kwa namna moja au nyingine watakusaidia wewe hapo kuweza kufikia ndoto zako kubwa za kimafanikio katika biashara.

Hizo ndizo nguzo tano muhimu sana ambazo unahitaji kuhakikisha kwamba umezifahamu wakati unafanya mauzo ya bidhaa zako.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


One response to “Nguzo Tano Za Masoko”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X