KONA YA SONGA MBELE: Nani Anakujua?


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala zako pedwa ambazo hukujia kila siku ya jumapili. Karibu sana katika makala haya ya siku hii ya leo, ambapo tunaeanda kuangalia ni nani anakujua katika biashara yako?
Mara nyingi mtu anapokuwa na wazo la biashara, ana kuwa tayari anaona kwamba wazo lake litamfanya kuwa tajiri ndani ya muda mfupi. Wazo lake la biashara linamfanya anakuwa na motisha kubwa sana ya kufanya makubwa, kiasi kwamba anakuwa hashikiki. Pesa anakuwa anaziona nje nje tu!  Lakini kuwa na wazo la biashara na kuwa biashara yenyewe ni vitu viwili tofauti. Biashara kama biashara ina kanuni zake ambazo zinaiongoza ili kukua na hatimaye iweze kufikia hatua kubwa sana. Leo hii tunaenda kuangalia jambo moja la muhimu sana ambalo unalihitaji kuhakikisha kwamba biashara yako imekua na kuwa bora zaidi.
soma zaidi: KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini
Na ili biashara yako ikue iwe bora zaidi inahitaji kuuza. Biashara bila ya kuuza itafikia hatua kwamba biashara yako itakosa mzunguko mzuri wa pesa na hatimaye itaanguka. Kuwa na wazo la biashara tu haitoshi kukufanya wewe kuwa bora. Au kuwa na bidhaa bora ambayo haifahamiki kwa watu haitoshi tu kukufanya wewe kuingiza kipato katika akakunti yako. Lakini watu ambao wananunua bidhaa yako ndio wenye uwezo wa kuufanya wewe uweze kuuza kwa kiwango cha hali ya ajuu sana.
Na watu ambao wananunua bidhaa yako ni wale ambao wanakujua. Kama watu hawakujui basi ndio kusema kwamba hawawezi kuja kwako kwa ajili kununua bidhaa yako.lazima watu wakujue wewe ni nani na uko wapi ndipo waje kwako wa ajil ya kununua bidhaa ambayo wewe hapo unayo.
Na ili watu wakujue maana yake unapaaswa kuhakikisha kwamba unajitangaza kila siku kila sehemu na kwa kila mtu. Usichooke kujitangaza kila kunapokucha. Kumbuka kwamba biashara yako ni matangazo, bila matangazo hakuna biashara. Matangazo ndiyo yatakufanya wewe kufahamika kwa watu wengi zaidi.
Linapokuja suala zima la matangazo huwa napenda sana kutumia mfano wa makampuni makubwa sana ambayo tunayo hapa nchini lakini kila siku huwa hayaachi kujitangaza. Miongoni mwa makampuni ambayo tunayo hapa nchini na hayachi kabisa kujitangaza japo unaweza kuona kwamba yamefika mbali sana ni Vodacom, cocacola, TIGO, CRDB na mengine mengi sana.
Kila unapoongelea makampuni haya basi jua kwamba asilimia kubwa ya waetu wanayafahamu. Lakini habari njema ni kwamba makampuni haya hayajawahi kuacha kujitangaza hata siku moja. Kampuni kama ya cocacola ina zaidi yamiaka 130 lakin kila sikku lazima ukutane, usikie au kuona tangazo lao. Kila mtu kutoka katika kila kona ya dunia anawajua. Kwa nchi yetu hapa TANZANIA wameenea hadi kijijini. Wameenda hadi mitaa ambayo wewe hapo hujawahi kufika, lakini bado hawaaachi kujitangaza. Sasa kitu gani kinakuzuia wewe hapo kujitangaza.
Kwa hiyo unapaswa kuhakikisha kwamba unajitangaza kwa watu kila siku. Hakikisha kwamba kila unapoenda kila mtu ambaye unakutana naye anajua wewe ni nani? Na una nini? Tangaza bidhaa yako mpaka  Yule ambaye aliye mbali na wewe ajue na aisikie kama vile imemgusa mwilini mwake. Kama ambayo watu wa cocacola wanapotangaza kwamba onja msisimko na wewe unajisikia kana kwamba unauonja kweli hata kama hauna soda. Na muda mwingine baada ya kuona tangazo au baada ya kusikia mtu akimwaga cocacola kwenye glasi huku ikitoa mlio wake, basi na wewe utakimbia kkununua moja ili na wewe uonje msisimko. Hii yote ni nguvu ya tangazo ambal o wewe umelisikia. Hivyo hakikisha kwamba unajitangaza, na kujitangaza. Isipite siku bila ya awewe kuhakikisha kwamba umejitangaza kwa watu mbali mblli ilii wakujue na mwisho wa siku utaaweza kufikia hatua kubwa sana.

Utamtangazia nani bidhaa yako siku hii ya leo? Kazi ni kwako!
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X