KONA YA SONGA MBELE; Hii Ndio Kauli Ambayo Inadidimiza Ubunifu Hapa Harani Afrika.



Moja kati ya bara lenye wingi wa rasilimali ni afrika. Ila kwa kuwa watu hawajajengwa katika msingi wa kuhakikisha kwamba wanaziona rasilimali basi wanatumia muda mwingi sana kuhakikisha kwamba wanalalamika kila siku, kila wakati. Hali hii inazidi kupoteza ubunifu wa vijana wetu wa kiafrika. Kuna vitu vingi sana vinavyofanya waafrika wasiweze kuzitumia  rasilimali zao ambazo zimewazunguka kama ambavyo nimeeleza kwenye kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-1. 

SOMA ZAIDI; Kona Ya Songa Mbele; Nani Anakujua?


Ila  kwa leo hii ninaenda kuzungumzia kitu ambacho kinaitwa kauli.
Miongoni ambayo nimewahi kuisikia sana hapa barani afrika tangu nimezaliwa nni kauli inayosema “babu zetu walikuwa wanafanya hivi”.  Kauli hii watu wanapenda kuitumia sana.  Yaani watu wanataka waige na kufanya kila kitu kama ambavyo kilikuwa kikifanywa na baba na babu zetu. Ukijaribu kufanya kinyume utasikia maneno yanaanza kupita, babu yako alifanya hivi, baba yako naye akafanya hivi. Sasa wewe kijana wa juzi juzi tu ndio unataka kubadili kila kitu. Yaani wewe unataka kusema kwamba una akili zaidi ya baba na babu yako.  Hakika maneno kama hayo hapo hayawezi kuendeleza ubunifu ulio ndani ya vichwa vya waafrika.
Hatuwezi kuijenga afrika mpya kwa kufanya vitu vile vile kama vilivyokuwa vikifanywa na mababu wetu. Hatuwezi kuwa na afrika huru kama hatutaruhusu ubunifu na ugwiji ulio ndani ya kila mtu kuonekana kwa nje?

SOMA ZAIDI; Mambo Matano Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Jambo Lolote

SASA NIFANYEJE KAMA HALI KAMA HII HAPA ITAJITOKEZA?
Kwa kuwa hali hii inajitokeza kila siku, kila wakati katika mazingira yetu. Basi lazima tuwe na mbinu mbadala. Lazima tuwe na uwezo wa kufanya makubwa yaliyo ndani yetu na kuhakikisha kwamba hatuzuiwi na kauli hizi ambazo zinatolewa na watu. 
Kwa sababu hiyo unapasawa kujua haswa wewe unataka kufanya nini.  Ni bora ukajua ni wapi unataka kwenda na kwa nini? Ukafahamu kwa nini unataka kuwa mbunifu na kitu gani ambacho unataka kuweka muda wako kubuni. 
SOMA ZAIDI; Hili Ndilo Duka Lenye Kila Kitu

Baada ya hapo nenda kaweke juhudi yako na nguvu katika kuhakikisha kwamba jambo hili linakamilika. Wacha watu waongee. Maneno ambayo watu wanaongea, vitendo ambavyo watu wanafanya,vione kama fursa ya kwako kuzidi kusonga mbele na kufanya zaidi. 
Ukiona mtu anakwambia umekosea kwa sababu babu zetu walikuwa wanafanya hivi na wewe unafanya tofauti. Jua kwaba mtu Yule kafungwa kifikra, hivyo hakikisha kwamba na wewe haufugwi kifikra. Badala yake unakuwa na mtazamo ambao uko bora sana katika kuhakikisaha kwamba unasonga mbele. Mtazamo ambao utakutoa hapo ulipo kwenda hatua ya ziada.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X