Hii Ndio Kozi Inayofundishwa Katika Vyuo Vyote


katika zama za sasa hivi dunia imebahatika kuwa na vyuo vingi sana. vyuo hivi vinazidi kuja katika mifumo mbali mbali ukiwemo mfumo wa kwenda moja kwa moja vyuoni au mfumo wa kusoma kwa njia maarufu sana ya mtandao ambayo kwa sasa imeshamiri sana katika dunia hii.
ukifuatilia vyuo vyote hapa duniani vina kitu kimoja ambacho kinaviunganisha kwa pamoja. vyuo hivi hata havijatofautiana wala havina mifumo tofauti tofauti. ingawa kile kinachofundishwa katika chuo kimoja hutofautiana na kile kinachofundishwa chuo kingine. kila chuo kina mwonekano wake ila kitu kimoja tu kinaunganisha vyuo vyote,. Na hii ni kozi inayounganisha vyuo hivi. Nimegundua kwamba kozi hii ni muhimu sana kwa wanachuo wote na wanapaswa kuifaulu. kama kozi hii watashindwa kuifaulu wakiwa chuoni basi itakuwa vigumu kwa wanachuo hawa kuweza kushinda katika hali ya kawaida katika mtaa.  Hata hivyo mbali na kwamba kozi hii kuwa inafundishwa katika vyuo vyote vya hapa duniani haikuzuii wewe ambaye hujaenda chuo kuisoma kozi hii hapo hapo nyumbani kwako. kama utafaulu vyema kozi hii basi wewe utakuwa umefaulu vyema katika maisha ya kiujumla na utafanya vizuri sana. yaani kiufupi ni kwamba utatoka sifuri na kwenda kileleni muda sio mrefu. 


kozi yenyewe ambayo inafundishwa vyuo vyote hapa duniani ni muda. kila chuo kinafundisha umuhimu wa muda ingawa wakufunzi, hawasemi kwa wanafunzi wao moja kwa moja kwamba sasa mnajifunza juu ya umuhimu wa muda. lakini kwa kuwa kuna mpangilioo maalumu ambao kila chuo umeweka kwa ajili ya wanafunzi wake ndio maana tunaona kwamba wanafunzi wanapokuwa chuoni wanaufuata ule mpangilio wa ratiba unaoendana na chuo husika. Kila chuo huwa kina ratiba ambayo wanafunzi wake wanapaswa kuhakikisha kwamba wanaifuata hasa pale wanapokuwa chuoni kwa ajili ya kujifunza. Kama mwanafunzi wa chuo atahakikisha amefuata ratiba ya chuo husika kwa muhura unaohusika na bila kukosa basi huyo mwanafunzi atakuwa amekuwa mhitimu mzuri wa somo zuri juu ya muda ambalo wakufunzi wa chuo hufundisha kwa wanafunzi wake bila ya kuwaambia kwamba sasa tunawafundisha juu ya somo hili la muhimu sana.

ubora wa wa somo hili sio lazima lifundishwe katika chuo kikuu peke yake. ubora ni kwamba somo hili linaweza kufundishwa katika sehemu yoyoyte ile katika dunia hii ambamo tunaishi. Yaani kiufupi ni kwamba kama wewe utaweza kuhakikisha umepangilia ratiba zako za kila siku na kuhakikisha kwamba umefuata ratiba yako ya kila siku katika kufanya kazi zako za kukutoa sifuri kuhakikisha kwamba unaelekea kileleni basi wewe utakuwa katika hali nzuri sana ya kulifaulu somo hili la muda.

kazi ya kufanya dsiku hii ya leo.
1. hakikisha unapangilia ratiba yako ya siku hii ya leo na kuifuata.
2. hakikisha kwamba haupotezi muda wako kwa vitu ambavyo wewe binafsi unaona kwamba havikujengi.
3. usiruhusu muda wako kuibiwa na mtu yeyote siku hii ya leo.




Tukutane siku nyingine kwenye makala ya kuelimisha na kuhamasisha kama haya.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X