Kitu Kimoja Kinachozidi Kukurudisha Nyuma


Habari ya siku hii ya leo. Leo ikiwa ni tarehe18/10/2017. Imani yangu sasa umeianza siku yako kwa namna ambayo ni ya tofauti kabisa. Namna ya kukujenga na kukupa nguvu. Umeianza kwa kusoma malengo yako

Leo hii naenda kukushirikisha kitu kimoja ambacho kinazidi kukurudisha nyuma kila kukicha. Kitu hiki kimekuwa kinakurudisha byuma na kitazidi kukurudisha nyuma kama hautabadilika na kuchukua hatua sasa. Kitu hiki umekikaribisha na kukifanya kuwa sehemu ya maisha yako ingawa sio kweli kwamba kitu hiki ni sehemu ya maisha yako.

Je, kitu hiki ni kipi?
Kitu chenyewe ni kukubali kila kitu unachoambiwa.
 Maisha yako unazidi kuyarudisha nyuma kila siku, kila wiki, na kila mwezi kwa sababu tu unakubali kile ambacho kila mtu anakwambia. Yaani wewe kufikiri kwako imekuwa kazi. Umeamua kuwaachia watu wengine njia hii ya kufikiri na kuangalia kila kitu kutokea katika kila kuona na mwisho wa siku kuja na majibu yako.

Yawezekana wewe ni miongoni mwa watu wanaofuatilia mambo ya siasa kila siku. Yaani wewe kazi kubwa sana unayoifanya ni kuenda na upepo kila siku. Leo wanasiasa wakija wanasema hiki na wewe umoo! Tayari umekubali kile walichosema.
Kesho wanageuza kauli yao ya jana bado na wewe unakubali kwamba bado wapo sahihi.
Kesho kutwa wakibadilika na wewe bado unabadilika.

Soma zaidi; Vitu Nane Vya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara

Kwani wewe kinyonga?
Yaani wewe kila rangi inayokuja pembeni mwako unajitahidi kubadilika ili uweze kuendana nayo. Ukikutana na rangi ya kijani unabadilika na kuwa kijani,
Ukikutana na rangi nyeusi basi na wewe unakuwa mweusi,
Ukikutana na rangi nyeupe na wewe unabadilika na kuwa mweupe!!!

Huu sasa ndio muda wako wa kubadilika na kuanza kuviangalia vitu kwa jicho la tofauti. Kuwa na utatatibu wa kufikiri na kutoa maoni pamoja na kuamua wewe kama wewe.

Usitake kuendana na ule usemi wa kwamba bendera siku zote hufuata upepo. Wewe sio bendera. Ya bendera yaachie bendera lakini maisha maisha yako usiyape upepo. Kuwa na msimamo, kuwa na uamuzi ambao unajua kwamba uamuzi huu kwa hakika unazidi kunifanya kuwa mtu mwenye nguvu, uelewa na huku ndio msimamo wangu.

Kama umepanga leo kwamba utafanya kitu fulani, usiache kufanya kwa sababu tu fulani kakwambia twende sehemu fulani. Yaani unabadilisha ratiba yako kwa sababu zisizo na maana. Sababu ambazo hata hazikujengi.

Chukulia mfano leo hii umepanga kusoma Kitabu SAA kumi za jioni na rafiki yako jioni hiyo ya SAA kumi anakuja na kukwambia twende kuangalia mechi ya simba na yanga. Utafanyaje?

Hatua ya kufanya siku hii ya leo.
1. Hakikisha unakuwa na msimamo katika kile ambacho unafanya. Usikubali kuyumbishwa na mtu, au watu.

2. Anza kufikiri wewe kama wewe? Usiruhusu watu kufikiri kwa niaba yako.

3. Jiulize kama hiki kinachofanyika hivi kwa sasa kikibadilishwa kitafanyikaje?

4. Je, kikianza kufanyika kutokea sehemu nyingine kitakuwaje? Usikubali watu wengine wafikiri kwa niaba yako na wewe uwe mtu wa kumeza kila wanachosema

Ulikuwa na mimi,
Kocha Godius Rweyongeza

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X