Hii Ndio Siku Mpya Unayopaswa Kuishi


Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Ni msemo wa kiswahili. Kuna watu ni maarufu sana wa kuwaza yaliyopita. yaani wanasahau ya leo (sasa) kuwa ndio yenye umuhimu mkubwa sana kuliko hata yale wanayowaza.

Leo ni siku nyingine mpya.
Leo haijawahi kutokea.

Najua hapa utaanza kuniambia “jana nilikunywa chai kama leo”
Ndio uko sahihi Jana ulikunywa chai! Lakini swali la msingi chai ya jana ni sawa na ya leo? Je, bado ni chai ileile? Je,kiasi cha chai ulichokunywa jana ni sawa na cha leo?
Na kitafunwa je?

Unaona sasa,, leo ni tofauti sana. Mimi mwenywe makala niliyoandika jana ni tofauti na ya leo.

Soma zaidi;kona ya songambele; jinsi ya kufanya kazi kubwa kwa nguvu kidogo

Kumbe hakikisha unaishi leo maana leo ni zawadi kubwa sana.
Ona fursa katika kila Kitu.

Naipenda sana siku a leo maana ni siku ambayo haijawahi kutokea maishani mwangu.

Moja kati ya vitu vinavyofanya watu wasiishi leo ni
1. Kufanya kwa mazoea.
Kuna watu umekaa nao kwa kipindi sasa umewazoea Sana. Unawaona wa kawaida sana. Hata ukikutana nao leo hii, hujishughulishi kuona kwao somo unalojifunza kwa siku KUTOKA kwao.
Unaishia kuwaambia, nilikuwa nakuheshimu lakini sasa…
Acha mazoea. Godius Rweyongeza wa jana sio wa leo. Anaweza kuwa Mpya au amezeeka zaidi ( kama hajifunzi)

2. Kubeba makosa ya jana na kuyaleta leo.
Hapa, unapoteza muda. Ndio maana tulilala ili tuamke tukiwa wapya na kufanya mapya. Ukilala ni sawa na kufa. Ukifa ukafufuka hauendelezi ubaya, unaanza kwa motisha Mpya. Jifunze kwa Yesu. Alipokufa na kufufuka hakuanza kuwasaka maadui zake. Alianza na mambo mapya. Aliendeleza mazuri.

Soma zaidi;  kosa kubwa unalopaswa kuepuka

3. Uzembe wa kufikiri.
Watu wamezoea kila kitu kumezeshwa. Kila kitu kuambiwa fanya hivi. Sasa unapofika wakati hakuna wa kukumezesha. Ndipo tunaanza kusikia bongo bahati mbaya.
Leo ni  bahati mbaya sana, na vitu vingine kama hivyo.

Ili uweze kuofurahia sana siku ya leo achana na nayo hapo niliyokuambia

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X