KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.馃し馃徑鈥嶁檪馃し馃徑鈥嶁檪


馃し

Ikifika mwishoni mwa mwaka wowote, huwa napenda sana mchaka mchaka ambao huwa unakuwepo. Watu wengi huwa wanauzungumzia mwaka mpya kutokea kila kona. Mitandao ote ya kijamii huwa inajaa jumbe mbali mbali za kuuaga na kuupokea mwaka Mpya. Nyimbo mbali mbali huwa zinaimbwa kuashiria mwisho wa mwaka na ujio wa mwaka Mpya. Maandalizi mbali mbali huwa yanafanyika nyumbani (maandalizi ya chakula, mavazi, matembezi, kutaja ila machache). Vyombo vya habari huwa havipo nyuma. Bali na vyenyewe huwa huwa vinaupamba mwaka unaokuja kwa mbwembwe nyingi sana. Vyombo hivi pia hushirikiana na mashirika na makampuni mbali mbali kutangaza ofa mbali mbali za makampuni hayo hivyo kuwafanya watu wazidi kufurahia maisha.

Kila ukiongea na mtu katika kipindi hiki, basi, utasikia habari za mipango mikubwa ambayo anapanga kufanya mwaka unaofuata. Kila MTU huwa ana mipango mikubwa (Haijalishi ameandika au hajaandika)

Mwaka Mpya
Siku ya mwaka Mpya, ni siku ambayo huanza kwa mbwembwe kubwa sana. Watu wengi hujitolea kufanya kazi siku hiyo. Utasikia wengine wanasema 鈥渓eo lazima nikapande miti.” Wengine watasema 鈥測aani Mimi siwezi kukosa kufanya kazi walau kidogo siku ya mwaka Mpya.”
Hali hii ya motisha, kuchapa kazi na kujituma ambayo huwa inajitokeza tarehe moja huwa inanipa matumaini ya kwamba kufikia mwishoni mwa mwaka huu nitakuwa naishi na watu wengi waliopiga hatua na pengine  mamilionea wapya

Tarehe 10 Januari
Kufikia tarehe kumi basi watu tayari wameanza kupoteza ile motisha ya kufanya kwa bidii, kujituma na kupangilia maisha yao

Watu wengi wanaoweka malengo yao January huwa hawakumbuki hata karatasi walipoyaandika kufikia mwishoni mwa mwaka. ni maneno ya Joseph C. Musharika. Mwandishi wa Kitabu cha _From Victim To Victor_. Hii inawahusisha watu binafsi, makampuni, mashirika na hata serikali.
Sasa Mimi nashangaa. Nashangaa sana kiasi kwamba nasukumwa kuuliza ipo wapi motisha ya januari mosi?
Kwa nini watu wamepoteza Malengo na wengine hawakumbuki hata walipoyaweka Malengo yao?
Je, wewe Malengo yako uliyoanza kuyatekeleza January 1 yako wapi?

Hapa kuna mambo matano ambayo yatakufanya usipoteze mwelekeo wa malengo yako januari mpaka disemba.

1. Panga kama vile utaishi milele, ishi kama vile utakufa kesho
Andika Malengo yako ya miaka 1/2/3/5/10/25.
Watu wengi wanaamini katika msemo unaosema leo ni leo asemaye kesho ni mwongo hali hii imewafanya watu wengi kusitasita kuweka mipango yao ya muda mrefu. Hivyo kuamini kwamba kila wanachopata sasa ni kwa ajili ya sasa na kesho itajipa yenyewe. Hali hii itakunyima motisha ya kusonga mbele na kufanya mambo makubwa.

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa napenda sana kusikiliza redio. Kila siku SAA kumi na mbili ilikuwa lazima  nisikilize DW habari za ulimwengu. Siku moja wakati nasikiliza habari hii. Walitangaza kwamba kufikia mwaka 2050 kuna viumbe watakuwa wamepotea na kutoweka kwenye uso wa dunia.

Watu niliokuwa nao walianza kulalamika. Kila mtu alishangaa kuona ni kwa nini wanazungumzia mambo ya mwaka 2050 sasa. Wakati bado kuna muda mwingi sana. Rafiki yangu mmoja alithubutu kusema ni uong. Huku mwingine akisema wazungu wanapoteza sana muda.

Hali hii inaweza kukupa picha ni kwa jinsi gani watu hawataki kuangalia mbeleni. Ni kwa jinsi gani watu hawana mipango yako.

2. Andika malengo yako makubwa matano ( _the big five_ ).
Kila siku kuna mambo mengi sana ya kufanya. Kila wiki ina mchaka mchaka wake. Kila mwezi una raha na changamoto zake. Hakikisha unapoanza mwaka mpya unaandika mambo makubwa matano ambayo utayafanya ndani ya mwaka huo. Ndio mambo makubwa matano tu.
kama huwezi kuchukua muda kidogo kupanga utaupoteza mwaka mzima anasisitiza Godius Rweyongeza.

Swali
Sasa mbona leo ni mwezi wa 9? Ina maana nisubiri mpaka januari ndipo niandike mambo yangu makubwa matano?

Jibu
Hapana. Huhitaji kusubiri mpaka januari ili upangilie maisha yako. Siku zote wakati ni sasa, muda ni sasa na wewe anza sasa.

Mwaka mpya unaweza siku yoyote ile. Ndio maana mwaka wa serikali huanza julai 1. Makampuni mbali mbali huanza mwaka Mpya kwa nyakati tofauti tofauti. Wewe mwaka wako Mpya ni leo tarehe 7septemba 2017.

3. Soma Malengo yako makubwa matano
Jenga utaratibu wa kuamka kila siku asubuhi wakati dunia imelala. Jisomee malengo yako na pangikia siku yako.
Hakikisha kila asubuhi umesoma lengo lako LA sasa.
Baada ya hapo andika mambo 20 tofauti tofauti utakayoyafanya ili kuboresha lengo ndani ya siku hiyo.

4. Lengo moja tu linakutosha.
Hahah, najua hapa utakuwa umechanganyikiwa. Iweje Mimi niliyeandika uwe na malengo matano sasa nikwambie unahutaji lengo moja tu!

Ndio unahitaji lengo moja. Hii haimaniishi Malengo yako makubwa matano uyafute na kuyateketeza. Hasha! Ukifanya hivyo hutakuwa na tofauti na wale wanaoanza mwaka  kwa mbwembwe, lakini kujisahau na mwisho wa siku kupoteza walipoandika Malengo yao.

Unahitaji lengo kuu moja LA kushughulika nalo kwa wakati. Lengo moja tu LA kufanyia kazi kwa wakati. Hili ndilo lengo nambari moja. Kipaumbele chako cha sasa.
Kwa hiyo sasa kati ya Yale Malengo yako matano, chagua moja tu LA kufanyia kazi sasa. Ndio lengo moja tu.

5. Unaweka nini mfukoni mwako?
Hakikisha unatembea na malengo yako popote uendapo. Sasa naenda kukupa siri ambayo hujawahi kuipata sehemu yoyote. Siri hii nimeiandika mwishoni kwa ajili ya wavumilivu. Maana najua wengi wameishia njiani. Hata Yesu aliwahi kuwaambia mitume wake kwamba wavumilivu ndio watakaouona ufalme wa mbinguni. Hivyo wewe kwa kuwa tumesafiri pamoja na hukuona haja ya kuacha kusoma makala hii hata kama ndefu, chukua siri hii.

Mfuko wako wa kulia ufanye kuwa mfuko wa Malengo yako
Najua una vitu vingi vya kubeba. Ila mfuko wako wa kulia hakikisha unaufanya kuwa wa kubeba malengo yako. Unajua nini kitatokea? Kila utakapogusa mfukoni utashika Malengo yako na hivyo kukukumbusha kwamba unapaswa kufanya kitu fulani.

Wakati Wako Ni Sasa!

#Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni


2 responses to “KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.馃し馃徑鈥嶁檪馃し馃徑鈥嶁檪”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X