Kuna vitu ambavyo unaweza kuvinunua sokoni, na kuna vitu huwezi hata siku moja kuvinunua sokoni. Kuna vitu ambavyo upatikanaji wake unakuwa mgumu wakati vitu vingine upatikanaji wake wake ni kawaida.
Wakati vitu Vingine vunakubitaji use na pesa,, ili uvipate vitu vingine vinahitaji juhudi Yako tu ili viweze kuwepo. Vinahitaji pia muda wako ili uvipate.
Kuna ujuzi hapa ambao wewe hapo hauna. Na unazidi kupoteza muda mwingi sana kwa sababu tu ya kutokuwa na na ujuzi huu. Haujali kwamba muda ni raslimali Yako ya muhimu sana ambavyo unayo hivyo hupaswi kuuchezea, bado hauweki juhudi yoyote ile ili kuhakikisha kwamba umeutafuta ujuzi huu. Ndio ujuzi huu ni kuwa na mpangilio. Inalipa sana ukiwa na mpangilio na unajua kitu gani ni cha wapi, na kinapaswa kufanyika wapi?
Linapokuja kwenye suala la mpangilio huwa napenda kutolea mfano wa mpishi wa hoteli au mgahawa, hasa ukimwangalia muda wa chakula ukiwa unakaribia.
Huwa anafanya vitu vyake kwa mpangilio. Kila kitu ambacho huwa anagusa huwa kina maana huwa kimepangiliwa. Huwa anajua kwa nini amegusa kiungo fulani, na kila hatua ambayo Huwa anapiga huwa ina sababu zake. Hawezi kuchukua kiungo cha kachumbari na kukiweka kwenye mboga za majani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila kitu kimepangiliwa na kina sababu.
Na wewe unapaswa kuwa na mpangilio na kujua kitu gani unapaswa kufanya na kwa nini? Sio kila hatua ambayo utapiga inakufaa bali unapaswa kupiga hatua chache na za muhimu sana.
Mpangilio ni kitu ambacho kimekuwepo tangu kuumbwa kwa dunia.
Dunia imekuwepo kutokana na kwamba kuna mpangilio.
Wewe upo hapo kwa sababu tu kwamba kuna mpangilio mkubwa sana unafanyika ndani Yako. Chakula unachokula kinapangiliwa na kuwekwa vizuri sana ndani Yako mpaka kinakupa nguvu kubwa sana wewe. Ni kutokana na nguvu hii wewe unaweza kufanya vitu vingine vikafanikiwa. Nguvu hii imetokana na mpangilio.
Inalipa sana kuwa na mpangilio na kufanya kazi Zako kwa namna ambayo ina mwelekeo mzuri.
1. Hatua ya kufanya siku ya leo. Hakikisha kwamba unapangilia ratiba yako ya siku hii ya leo. Pangilia ratiba Yako ya wiki, pangilia ratiba Yako ya mwezi.
2. Usifanye kazi au kitu chochote ambacho hakijapangiliwa kwenye ratiba Yako.
3. Usiruhusu mtu kuingilia ratiba yako ya siku husika
Tukutane kileleni.
Na,
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com.