Liwezekanalo Leo Lisingoje Kesho


Kama ungekuwa siku moja ya kuishi duniani ambayo ni leo ungefanya nini?
Ni kitu gani ungefanya kumalizia muda wako wa mwisho wa kuishi hapa duniani?

Bila shaka kama ungekutana na watu ungeongea nao vizuri.
Kama  kuna mtu umemkosea basi ungemwomba msamaha lakini pia kusamehe waliokukosea.
Kama ni kazi basi ungehakikisha unaifanya vizuri.
Yaani kiujumla kila kitu kingefanyika vizuru sana.

Kumbe mambo hayo sio tu ya kusubiri kufanya siku utakapoambiwa leo ni siku ya mwisho ambayo ni ngumu kutokea ukaambiwa hivyo.

Hivyo cha kufanya kama kuna jambo ambalo linapaswa kufanyika leo. Basi wewe lifanye kwa kutumia maneno ya wahenga kwamba *liwezekanalo leo lisingoje kesho*

Steve Jobs mwazilishi wa kampuni ya Apple aliwahi kusema “kwa muda wa miaka 33 uliyopita, kila asubuhi nimejitazama kwenye kioo nabkujiuliza: ‘_kama leo ingekuwa siku yangu ya mwisho kwenye maisha yangu ningetaka kufanya jambo ambalo niko karibu kufanya? Kila mara jibu langu limekuwa hapana katika siku nyingi kwenye mstari, najua lazima nibadili kitu fulani’_”

Je, kila unalolifanya unajiuliza swali alilojiuliza Steve Jobs?

Kusita sita na kuahirisha ni maadui wa kuitumia fursa ya leo.

Kuna mtu alisema “kusitasita ni chanzo cha matatizo yangu niliyonayo leo. Hata hivyo sijui maana ya kusita sita nitaangalia kesho kwenye kamusi.” Mtu huyo alikuwa bado na tatizo la kusitasita.
Kumbe wewe achana na kusita sita zitumie fursa za leo.
Yaani tumia kanuni ya liwezekanalo leo lisingoje kesho.

Gene Brown alisema “Fursa za leo zinafuta kushindwa kwa jana.”  maana mpaka sasa huwezi kurudi mwanzo na kuanza upya lakini unaweza kuanzia hapo ulipo na kutengeneza mwisho mpya.
Anza kwa kufanya ambacho unaona kinawezekana leo bila kusitasita na kuhairisha.

www.songambeleblog.blogspot.com

Na
Coach Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.comcom


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X