KONA YA SONGA MBELE; Hivi Ni Vitu Vinavyotafutwa Kwa Wanachuo Wanaotafuta Ajira


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Karibu sana katika makala hii ya siku hii ya leo tujifunze kitu kipya. Maana bila kujifunza kitu kipya tutaangamia. Maarifa siku hizi yana mwisho kikomo. Kama hutatafuta Maarifa mapya, basi jua kwamba unajifungia na kujifungia fursa njema sana ambazo zingekujia.

Sasa karibuni kwenye makala ya siku hii ya leo.

Kumekuwa na wimbi la vijana wanaomaliza vyuo vikuu kumaliza chuo na kwenda kuhangaika kutafuta wakizunguka na vyeti katika kila kona.

Vijana hawa wanajinadi kwamba wao wamehitimu chuo kikuu wakiwa wamegraduate na GPA ya juu sana.

Soma zaidi; Hii Ni Maana Mbaya Ya Mwanachuo Kuwahi Kutolewa

Hahahah,, nacheka sio kwamba nafurahi ila kwa sababu kuna kitu ambacho kinanisikitisha hapa.

Hivi wewe ambaye unazunguka na vyeti hujui kwamba chuo uliposoma wewe kuna watu ambao wamesoma chuo hicho hicho kama cha kwako, na wao wana degree kama ya kwako? Darasa lile lile la kwako? Mmekaa wote darasani?
Sasa kwa nini uajiriwe wewe na sio huyu mwenzako?

Chukulia kwamba mmesoma darasani wanafunzi 100. Kwa nini uajiriwe wewe na sio Huyo Rafiki Yako?

Rafiki yangu kama bado una mtazamo huu wa kwamba uajiriwe kwa sababu tu cheti chako kina GPA kubwa, umepotea. (Ndio umepotea, badilisha mtazamo).

Juzi nikikuwa naongea na Rafiki yangu EDIUS KATAMUGORA (mwandishi wa Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio). Akawa ananiambia kwamba wanafunzi wanaohitimu vyuoni kwa mwaka laki nane. Na wanaopata Ajira sio zaidi ya lelfu themanini. Sasa hawa wengine wako wapi? Je ni kweli kwamba hawana vigezo vya kuajiriwa?

Hahahah! Sio kwamba nacheka ila, naomba sasa tuendelee kuwa wote mpaka mwisho. Kama unaona nakukatisha tamaa, bora uache kusoma kabisa maana yanayokuja yatakukatisha tamaa zaidi.

Ajirani hakuna MTU ambaye yuko interested na cheti chako??? Ndio. Hakuna hata mmoja? Wala hakuna MTU ambaye atakuajiri eti kwa sababu hauna kazi. Yaani kwa sababu hauna kitu cha kukuingizia kipato basi yeye akupe sehemu ya wewe kujiegesha kama wengi wanavyosema ili upate kipato. Hakuna!!

Hakuna mtu utakayemwendea kwa kutaja matatizo yako akakusikiliza? Hayupo! Kama unahisi nadanganya, basi wewe sasa hivi chukua Cheti chako hicho chenye GPA ya 5, nenda ukitaja matatizo yako uone ni wangapi ambao watakusikiza. Wakikusikiliza na kukuajiri, basi wewe nipigie simu ili niiondoe makala hii mtandaoni na niifutilie kabisa kwenye uso wa dunia.

Sasa basi haya hapa ni mambo muhimu sana kwako kijana wa chuo unayehangaika na kuzunguka na vyeti?
1.  Kumekuwa na kasumba ya kwamba kila MTU anayeingia ajirani anataka kuiba au kumwibia yule alimwajiri?? Anataka amuvune yule aliyemajiri. Ndugu yangu kama mawazo yako ndio hayo jua kwamba unajiaandaa kupoteza.

Siku hizi wanaajiriwa watu wenye asili (nature) ya ujasiliamali tu, basi. MTU ambaye hama ujasiriamali ndani yake, atakuwa anafikria kuiba, kuchukua kila kitu kutoka kwenye biashra.

Hapo ndipo utakuta waajiri wanataka kuwaajiri watu ambao wana tabia ya kijasiriamali. Watu ambao wanajua nini wanapaswa kufanya. Watu ambao wapo tayari kubuni na kuna na mawazo mapya.

Watu wenye asili ya ujasiriamali, wapo tayari kufanya kazi na kufanikisha majukumu yao bila hata ya kusimamiwa. Sasa wewe leo hii unalia kwamba hauna ajira, kesho unapata ajira, unazembea na unasubiri bosi wako aje aanze kukusimamia. Rafiki yangu, unajipoteza.

Kama wewe unazunguka na cheti anza kujifunza ujasiriamali, hata kama unataka  kuajiriwa. Kuwa na ile asili ya kijasiliamali itakusaidia kuiona dunia kwa namna ya tofauti. Ajira yako utaiendea kwa namna ya tofauti, utahakikisha kwamba unajitofautisha mwenyewe, la sivyo utakufa.
SIKU HIZI HABARI YA MJINI NI UJASIRIAMALI, HATA KAMA UNATAKA KUAJIRIWA!!!!

moja ya swali ambalo utaulizwa wakati wa usaili ni kuwa umewahi kufeli kwenye kitu chochote maishani mwako? Unajua kwa nini utaulizwa hili swali, kwa sababu kama umewahi kufeli maana yake kuna kitu cha maana ulikuwa unafanya. ila kama hujawahi kufanya kitu maana  yake hujawahi kufeli na huna sifa ya kijasiriamali. Loooo!

SOMA ZAIDI: Mjasiriamali ni nani

2. Badala ya kuzunguka mtaani unatembea na vyeti, anza kuzunguka mtaani ukionesha ujuzi wako. Zunguka  mtaani ukionesha kipaji chako. Dunia inaweza kukulipa zaidi ukiwa na kipaji chako, kuliko inavyoweza kukulipa ukiwa umeajiriwa.  tafuta kipaji chako na anza kukifanyia kazi. Kama hujui kipaji chako ni kipi, basi wewe nitumie ujumbe wasapu sasa hivi nikusaidie kugundua kipaji chako.

USIZUNGUKE NA VYETI, ZUNGUKA NA KIPAJI, NA UJUZI.

DUNIA INALIPA KIPAJI SIO KARATASI HIYO ULIYOISHIKIKIA MKONONI UNAIITA CHETI.

Afu wewe huoni kwamba kuzunguka mtaani kila siku na cheti ni kupoteza muda, na kadri unavyozidi kuzunguka ndivyo unavyozidi kudhoofusha hadhi yako, yaani unakuwa OUTDATED. Ile mikogo Yako ya chuo inazidi kupotea. Chukua hatua.

3. Jitofautishe mwenyewe au kufa. Ndio namaanisha kujitofautisha mwenyewe la sivyo utakufa.
Kama darasani mmesoma wanafunzi zaidi 100 na nyote mnategemea ajira, mnategemea nani atakuja kuwaajiri? Lakini wewe unawwza kuamua kufanya kitu kinachoendana na ujuzi wako ambao umehifunza chuoni. Kile ulichojigunza chuoni ni mtaji tosha kwako kutoka hapo ulipo. Fikria ni kwa namna gani unaweza kuutumia ujuzi wako wa chuoni kuanzosha kitu cha tofauti. Nagalia ni kwa namna gani ujuzi wa chuoni unawza kuutumia kutoa huduma kwa watu na angalia ni kwa namna gani wewe unaweza kuwa mtu wa msaada hapa duniani!

Huuuu! Sasa navuta pumzi maana nimekuwa nikiongea kwa muda mrefu.

SOMA ZAIDI:Kama Unataka Mali: Maeneo Matano Unapoweza Kupata Mali Halali…

Je, una ndoto kubwa za kufanyia kazi maishani mwako?

kamajibu lako ni ndio, basi hakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kitabu hiki cha kipekee ni mwongozo unaopaswa kuwa nao wakati unafanyia kazi ndoto zako. Kupata kitabu hiki wasilina nami kwa 0755848391


One response to “KONA YA SONGA MBELE; Hivi Ni Vitu Vinavyotafutwa Kwa Wanachuo Wanaotafuta Ajira”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X