Acha Kulalamika, Anza Kuishi


Acha kulalamika kwamba hauna muda wa kutosha kwa ajili ya wewe kufanya mambo fulani. Acha kulalamika kwamba kuna watu wanatumia uchawi kufikia mafanikio.
Acha kulalamika kwamba wewe umezaliwa kwenye familia maskini
Acha kulalamika kwamba serikali haijafanya kitu kwa ajili yako.

Chukua hatua hakuna kitu ambacho hakipo ndani ya uwezo wako, hakuna ambacho huwezi kukifanya wewe tena ukakifa ya kwa ubora zaidi.

Kama ni suala la muda unao wa kutosha yaani kwa wiki unayo Massa 168. Sawa na masaa 24 kila siku. Ukilala masaa nane, ukafanya kazi masaa nane, Je masaa mengine nane unayatumia kufanya nini?

Masaa haya ni sawa na masaa 240 kila mwezi ambavyo ni sawa na masaa 2880 kwa mwaka. Sasa haya masaa yote unayatumia kufanya nini? Kumbe tatizo sio muda, tatizo ni wewe.

Ila.kama unaamini kwamba kuna watu watumia uchawi kwa ajili ya kufikia mafanikio naweza kusema kwamba upo sahihi. Ndio wapo watu ambao wanatumiawanatumia uchawi fulani, na uchawi wenyewe ni kufuata kanuni.

Ukizijua kanuni za kitu fulani utaishi mmaishayenye furaha sana.
Kanuni zipo ili kurahisisha maisha. Hivyo kama unazijua kanuni huitaji kutumia nguvu kubwa sana katika kufanya kitu fulani.

Ukijua kwamba gari linahitaji mafuta kwa ajili ya kuanza safari yake basi hutaangaika  kutafuta kitu cha kuweka ili gari lianze safari..
Hutajiuliza kama unapaswa kuweka juisi au maji.
Kwa sababu kanuni inafahamika kwamba lazima uweke mafuta ili gari lianze safari.

Hivyohivyo kwa watu waliofanikiwa. Hawa watu wamezijua kanuni na kuzifuata. Huu ndio uchawi ambao wanatumia.
Jifunze kanuni za kila kitu urahisishe maisha.
Jifunze kanuni za Biashara.
Jifunze kanuni za Kilimo
Jifunze kanuni za mahusiano
Jifunze kanuni za michezo husika.

Utaishi maisha yenye furaha, utaishi maisha yenye furaha na watu watakuita mchawi.

Mpaka hapo naaminu utakuwa umeachana na suala zima la kulalamika
Wewe umezaliwa kusababisha mabadiliko
Kuna kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako ambacho wewe ukikifanya kinakutofautisha wewe na wayu wengine, kama ambavyo una mwonekano wa tofauti. Utumie upekee wako kufanya mambo ya pekee. Fanya mambo madoho aka ipekee hili uwe wa pekee.

Usianze kusema serikali imekufanyia nini Bali angalia unataka kuifanyia nini serikali.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X