Hili Ni Jambo Linaloendelea kukuweka Hapo Ulipo.


Vitu vyote duniani havibaki kama vilivyo Bali vinabadilika kadri ya mazingira na maeneo. Binadamu pia hajaachwa nyuma katika mabadiliko haya. Na ni mtu ambaye anabadilika kila siku katika utendaji, ukuaji na kufikiri.
Hii ni sheria ya asili yaani kama ambavyo mti unapandwa ukiwa mbegu vivyo hivyo binadamu anahitaji kubadilika hili kuendana na mazingira.

Mabadiliko yana changamoto zake lakini bado huitaji kuyakataa bali unahitaji kuyapokea hili yaweze kukusaidia.

Wakati mti unakua ukikosa mwanga basi hausemi sasa ndio mwisho Wangu wa ukuaji. Bali mti hutafuta mwanga ulipo ili uweze kuendelea kukua na kweli hatimaye mti hukua. Kama mti unaweza kufanya hivi kwa nini wewe usiweze kufanya hivi.

Au mtoto akianza kukua na kuanza kutembea huwa anaanguka kila akijaribu, lakini bado haachi, hatimaye huweza kukua na kutembea. Lakini haishii hapo, mtoto pia huweza kukimbia, na pengine kushiriki mashindano makubwa kama Olympic na kushinda.
Je, kama angeamua kuacha kutembea siku ya kwanza baada ya kuanguka angeweza kushiriki mashindano makubwa kama haya?

Sasa kwa nini wewe ukikutana na vikwazo vidogo unaacha? Kwa nini unaogopa na kukata tamaa?

Haya ndio mambo ambavyo yanakuzuia.

1. Hutaki kulipa gharama?
Najua unashangaa gharama gani napaswa kulipa? Ndio ni gharama ya Kile ambacho unapaswa kufanya. Tukienda hotelini tunakula kwanza na baadae tunalipa. Lakini katika maisha unalipa kwanza na baadae unakula.
Ukienda shuleni unasoma, unanunua vitabu, unalipa ada na kununua daftari hili upate elimu itakayokusaidia kufanya kazi. Hapo umelipa gharama.
Utakapoanza kulipwa kwa kutumia ujuzi wako ambao umejifunza kwa kulipa gharama basi tunasema umekula.

Mkulima akienda kulima shambani amatoa hela ya vibarua anatoa hela ya pembejeo na kuhakikisha amefanya umwagiliaji wa kutosha mpaka wakati wa kuvuna. ( hapo tunasema analipa gharama). Baadae anapopeleka mazao sokoni kuuza hapo ndipo tunaposema anakula.

2. Hauna malengo.
Kuna utafiti ulifanywa nchini marekani kwa wanafunzi wa chuo kikuu na kugundua kwamba asilimia 97.7 ya wanachuo ( wahitimu) hawakuwa na malengo. Huku asilimia 2.3 tu ndio ilikuwa na malengo.
Kuna mambo mawili ambavyo huwafanya watu wasiweke malengo.

💧uoga
Uoga huu unatokana na mambo Yale ambayo sisi huwa tunaingiza kichwani. Ukiingiza mambo chanya huleta matokeo chanya na ukiingiza  mambo basi basi lazima utegemee matokeo basi ambavyo yanaweza kujitokeza kwa mfumo wa uoga.
Baadhi ya mambo basi ambavyo yanaweza kupelekea uoga ni kama.

  1. Kusikiliza taarifa ya  habari kwenye redio au TV asubuhi au muda wowote.Mara nyingi habari hizi huwa ni hasi lakini pia husababisha kuianza siku yetu kwa mtazamo ambao ni hasi. Hutufanya tuione dunia kama sehemu ambavyo haifai mtu kuishi.

Soma zaidi; wiki Wiki Moja Bila Habari

  • #USHAURI (I) Epuka sana kusikiliza habari muda wa asubuhi maana mara nyingi unachokiingiza akilini mwako asubuhi (saa moja) baada ya kuamka. Huwa kina nguvu kubwa sana na kinaweza kukuonesha ni aina gani ya siku  ambayo unaenda kuwa nayo.
  • USHAURI (II) Ingiza habari chanya kila uamkapo asubuhi kutoka kwenye vyanzao chanya. Hapa nitaambatanisha baadhi ya vyanzo hivyo. Vyanzo hivyo ni kama vitabu vinavyoelimisha na kuhamasisha, blogu kama SONGA MBELE, BIDEISM, AMKA AMKA MTANZANIA, GEOFREY MWAKATIKAHuku utapata habari chanya zitakazokusaidia kuianza siku yako kwa  ubora wa hali ya juu sana.
KUMBUKA; (i) uko ulivyo kwa sababu ya Kile ambacho unafikria.
(ii) wewe ndiwe dereva wa maisha yako. Amua sasa maisha gani ambayo ungependa kuishi, amua mafanikio gani ungependa kufikia.
  1. Aina ya marafiki ulionao
  2. Niliwahi kuandika makala tenye kichwa cha NIAMBIE RAFIKI ZAKO NIKWAMBIE TABIA YAKO Tabia yako ni wastani wa watu sita waliokuzunguka. Kwa hiyo kama umezungukwa na marafiki wenye mtazamo chanya juu ya maisha basi utakuwa kwenye mwelekeo bora wa maisha.
Marafiki wengine wanaweza kukurudisha nyuma kiutendaji. Ukiwashirikisha mada, au kitu fulani chenye umuhimu basi watakataa Kile ambacho umewaambia na kukutolea mifano ya watu wengi walioshindwa kwenye jambo hilo ambalo unafanya.
  • #USHAURI (I) Chagua marafiki ambao unaendana nao kwa tabia, kwa kufikiri na kiutendaji. Wapunguze marafiki ambao wanakurudisha nyuma nakukuzuia kusonga mbele.
  • USHAURI (II) Tafuta watu waliofikia mafanikio na uwaunganishe kwenye mzunguko wako kwa kuwa na washauri kuhusu kile ambacho unafanya. Hwa ndio watakaokusaidia kufika unapotaka.
KUMBUKA (I) uache urafiki ubaki kwa ajili ya urafiki na wewe Fanya kazi na watu wanaojua kufanya kazi

💧 Malengo
Je, malengo yanafanya kazi?
Malengo ni muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya maisha.
Huwa napendwazalushajizi uliofanywa na nchi ya JAPANI baada ya kuweka malengo. Malengo yaliifanya Japani ikue kiuchumi.

1950 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja katika uzalushaji wa nguo ndani ya miaka 10. Hivyo walianza uzalishaji. Na kweli lengo lao lilifikiwa kama ambavyo walikuwa wamepanga.

Miaka ya 1960 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja wa vifaa vya chuma ndani ya miaka kumi.
Na kweli ndani ya miaka kumi Japani ilikuwa inaongoza kwenye uzalishaji wa bidhaa za Chuma.

Miaka ya 1970 Japani iliweka lengo la kuwa mzalishaji nambari moja wa bidhaa zitokanazo na wanyama ndani ya miaka 10.
Kweli ndani ya miaka kumi Japani waliweza kuwa wazalishaji nambari moja wa bidhaa zitokanazo na chuma. Na kweli waliweza
Nenda kaweke malengo.
Malengo tanafanya kazi.

Miaka ya 1980 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja la kuwa wazalishaji nambari moja wa vifaa vya umeme ndani ya miaka kumi (10). Kweli baada ya miaka hiyo waliweza, unajua kwa nini?
Sababu ni kwamba malengo yanafaya kazi.
Tatizo watu wanapoteza muda mwingi

Kupanga na kukaa kwenye vikao vya sherehe badala ya kupanga kuhusu ndoa yenyewe.

Wanatumia muda mwingi kupanga jinsi ya kupata kazi badala ya kupanga jinsi ya kutoa huduma kwa watu.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X