Utumie muda wako wa safari vizuri



Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za SONGA MBELE karibu sana katika makala ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadilisha mtazamo wako na mwelekeo wako kiujumla na kukufanya kuwa mtu mpya kabisa. Kitu ambacho kitakusogeza sana karibu sana na mafanikio.

Kujifunza kila siku ni njia nzuri ya kukufanya uzidi kusonga mbele kila siku, kutojifunza sasa hivi ni sawa na kuamua kufa kimawazo huku ukiwa unasubiri kuzikwa mbeleni. Sisi tushaamua kuwa wa kujifunza na sasa tunazidi kusonga mbele kila siku. Karibu sana rafiki yangu.
Tukirudi kwenye mada yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza muda wetu wa safari vizuri. Badala ya kuamua kuupoteza.

Kama kila siku

unasafiri kwa saa moja kuelekea kazini baada ya mwaka mmoja utakuwa umepoteza takribani wiki kumi na moja za kazi. Ukiangalia saa moja kwa siku linaonekana dogo sana lakini ni muda wa kutosha ambao kama utaamua kuutumia vizuri leo utakuja wa manufaa sana hapo mbeleni.

Kuna njia nzuri ambayo unaweza kuutumia vizuri muda wako wa safari, ambayo ni kusikiliiza kitabu kilichosomwa.

Njia hii itakufanya ufike kazini mwako ukiwa mwenye furaha na amani badala ya kufika umechoka. Njia hii itakusaidia sana kuutumia vizuri muda wako wa kazi vizuri badala ya kuutumia kusikiliza habari hasi au  habari ambazo hazielimishi  (habari hasi) au  kutofanya chochote kabisa juu ya muda huu.
Kama utajijengea utaratibu huu wa kusikiliza kitabu kimoja kilichosomwa kila siku. Na kama utatumia saa moja kila siku kufikia kazini ina maana utakuwa una uwezo wa kusikiliza vitabu viwili kila wiki ambavyo ni sawa na vitabu nane kwa mwezi
Nakuhakikishia kwamba utabaki kuwa ulivyo kama ulivyo sasa.

 Utumie muda wako sasa vizuri.
Sikiliza vitabu vilivyosomwa sasa bila kuchoka.
Unaweza sasa kusikiliza vitabu vinavyohusu, uongozi, ujasiliamali, uwekezaji, umuhimu wa muda, jinsi ya kuitumia akili yako kwa usahihi. Anza sasa kuutumia vizuri muda wako vizuri, changamkia fursa.

 Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X