Ubongo Ni Bustani


Habari za leo rafiki yangu na msomaji wa makala kutoka SONGA MBELE BLOG. Matumaini yangu unaendelea vyema na hatua kuelekea mafanikio ndani ya mwaka wetu huu mpya wa 2017. Karibu sana katika makala ya leo, ili tuendelee kujifunza maana hakuna sherehe kwa mwanamafanikio katika kujifunza. Kujifunza kunakufanya unakuwa kijana hata kama una miaka themanini (80) lakini pia kutojifunza kuna kufanya mzee hata kama una miaka ishirini (20). Amua sasa unataka kuwa wapi kwenye kundi la wazee au kundi la vijana. Ila kwa kuwa wewe ushaamua na upo unasoma hapa basi wewe umeamua kuwa kwenye kundi letu la vijana karibu sana.

Ubongo wa binadamu  unaweza kufananiswa na bustani ambayo unaweza kuamua kuilima au kuacha. Lakini uikiamua kuilima au kuacha bado inaleta matokeo.  Kama hakuna chochote ulichopanda kwenye bustani basi  magugu yataota. Lakini pia kama ambavyo mkulima huitunza bustani kwa kulima, kumwagiilia  kupalilia,  na kuondoa magugu waharibifu, vivyo hivyo wewe unahitaji kuupalilia ubongo wako, kuumwagilia lakini pia kupanda mbegu zilizo bora, kwa kuondoa magugu.

Ubongo wako ni bustani ambayo unaweza kuipalilia na kupanda kilicho bora ndani yake
Anza sasa.

Utaulima, utaupanda utapalilia kwa kuweka kilicho bora katika akili yako, ukiweka kilicho bora klitaleta matokeo bora na ukiweka kibaya kitaleta matokeo mabaya.
Maana matendo yako huendana na kile unachopenda. Kama utaingiza kile cha kukufikisha kwenye mafanikio  basi tutakuona ukielekea mafanikio (tutakuona kileleni) na kama utaingiza kinachokurudisha nyuma tutaona katika mwonekano wa nje matokeo yake. Matokeo ya nje yanatokana na kile ullichokiweka katika akili yako.
Amua leo kuulisha ubongo wako kile kilicho bora kama unataka kupata matokeo yaliyo bora. Ulime vizuri upande mbegu zilizo bora na zimwagilie ili ziweze kuota. Hakikisha unaondoa magugu yote yanayojitokeza
Kulima ubongo wako ni sawa na kuanza kuutumia ubongo wako kwa ajili ya manufaaa yako ya sasa na baadae
Kuupanda ubongo wako ni sawa na kuamuka kuvutia tabia fulani kwako, tabia ambazo unazihitaji kwenye maisha yako
Kuumwagilia ni kufanya kile unachopenda kila siku kama sehemu ya malengo yako. Kufanya kile ambacho kinakupeleka kwenye ndoto yako ambayo unapenda kuikamilisha. Kifanye kila siku ili kujijengea utaratibu wa kufanya hivyo. Anza sasa muda ni sasa.
Itakuchukua siku 21 tu na wewe utakuwa umeweza  kukifankya na kuendana na na tabia hizo. Kumbe kama utajisikia kama kutokufanya basi jiambie ni siku 21 tu baada ya hapo nitaacha.

Kuondoa magugu ni kuondoa vijitabia vyote vinavyokufanya urudi nyuma.    Vijitabia ambavyo vinakufanya uogope kuendelea na kazi.   Lisha ubongo wako na kitu killichobora, lisha ubongo na vitu ambavyo vitakufikishisha kwenye matokeo bora. Kwa kufanya utakuwa unajivutia tabia fulani ambazo unaziipenda.                     



    Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X