Kama Utashindwa ni juu yako Na kama Utashinda Ni Juu Yako


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu

Mara nyingi likitokea kosa lolote mtu atamtafuta mtu wa kulalamikia.

Hivi ulishawahi kugundua kwamba ukimunyooshea mtu kidole kimoja vitatu vinakuelekea wewe na kimoja kitaelekea juu kama ishara ya ushahidi.

Hii ni kuonesha kwamba wewe ndiwe unayechangia asilimia 75℅ ya makosa yako na changamoto zako  zinazojitokeza, na mwingine unayemunyooshea kidole anachangia asilimia 25% ya makosa. Kumbe hata kama angetimiza wajibu wake bado kosa au kikwazo hicho kingetokea kwa sababu wewe kama mhusika unachangia asilimia 75 ya makosa yote.

Je unahitaji mabadiliko wewe kama wewe?
Je mnahitaji mabadiliko kama kikundi?

Sasa ni muda wa kuacha kuwa na matamanio na kuanza kufanya.

Soma zaidi hapa; Je, wewe una matamanio au ndoto?

Kitu kizuri kitakachokufanya ufike unapotaka  ni nidhamu juu ya kile unachofanya
Nidhamu ni mtaji nambari moja ambao unapawa kulipa kwa ajili ya mabadiliko na matukio mazuri ya baadae.

George Washnton anasema

Nidhamu ni roho ya jeshi na hulifanya jeshi kushinda au kushindwa

Nidhamu ni njia ya  kuelekea mafanikio

Nidhamu ni njia ya kukuletea mabadiliko
Nidhamu ni kukubali kwamba wewe ni mhusika mkuu kwa kila kitu maishani mwako.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X