Jambo Linalokuzia Kufikia Mafanikio.


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu

   Kadri unavyojitahidi kujikwamua ili uweze kupiga hatua kubwa sana ya mafanikio, yapo mambo yanayo jitokeza kukuzuia kufikia mafanikio yako. Mambo kadri tutakavyoona yana chanzo kikubwa ambacho wewe binafsi unaweza kukizuia na chanzo hiki ni wewe. Utagundua kwamba wewe ndiye mwenye uwezo wa kuzuia hiki kikwazo na kuamua kusonga mbele.

Kikwazo hiki ni kipi? 

UOGA
   Kila binadamu ana uoga fulani ndani yake. Tofauti huja kwa namna ambavyo sisi huwa tunashugulika na uoga wetu. Wapo wanaochukulia uoga kama sehemu ya maisha yao.
   Uoga unaweza kuwekwa katika makundi mengi sana. Ila makundi makubwa sana ni uoga wa kupoteza pesa au uoga wa kufanya kosa.
kinachozuia watu kusonga mbele ni uoga ulio akilini mwao ambao huwafanya wajiulize maswali mengi ambayo hayana tija. Itakuaje kama biashara itashindwa? Itakuaje kama nitakosa wateja? Itakuaje kama bei ya bidhaa itashuka?

Je nifanyeje kuondokana na uoga?
       Kuwa na washauri wanaokusaidia kule unapotaka kufika. Unapochagua washauri wachague wale ambao wamewahi kufanya jambo ambalo unataka kufanya. Usichague washauri kwa sababu umechagua, wengine wanaweza kukupoteza.
   
       Njia ya pili ambayo itakusaidia kuondoa uoga ni kujielimisha mwenyewe. Yapo mambo mengi sana ambayo unaweza kujielimisha mwenyewe kila siku. Unaweza kujielimisha mwenyewe kuhusu shughuli unayoifanya na  ujasiriamali. Hata kama hutaki kuwa mjasiriamali ebu jaribu kujielimisha mwenyewe kuhusu ujasiriamali, naamini utafaidika sana.  Unaweza kujielimiisha kwa kusoma vitabu kama Rich Dad Poor Dad, cha Robert Kiyosaki na vingine vingi.

Soma zaidi hapa: Vitabu vitatu vya kusoma kabla mwaka hujaisha.

Unaweza pia kujifunza kuhusu uongozi. Hii sio lazima unataka kuwa kiongozi au la! Kwa kuwa kila binadamu ni kiongozi kwa asili jifunze uongozi utafaidika sana. Utajua aina za watu lakini pia utaweza kuijua na kuisoma aklili ya mtu inahitaji nini katika mazingira gani.

Lengo kubwa sana la kujifunza ni kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kuondokana na uoga katika maisha yetu. Kwa kuangakia wengine wamewezaje kuthubutu na kuanza. Kama wengine waliweza kwa nini wewe usiweze.
Ebu achana na uoga wa kaka, dada, mjomba atasema nini kama nitafanya hiki. Huyu ndiye adui nambari moja wa mafanikio na uwezo wa kumzuia umo mikononi mwako. Amua sasa kumwondoa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X