Je Wewe Ni Kiongozi Au Mfuasi?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blog ya SONGA MBELE imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuelekea mafanikio. Karibu sana katika makala ya leo.Uongozi ni sanaa ya ushawishi na kuhamasisha watu kufanya zaidi ya kile amabacho wamewahi kufikria katika harakati za kufikia mafanikio

Hii siku zote haina chochote cha kufanya na haiendani na hadhi yako. Wala hii haiendani na mamlaka  au ukubwa wowote.

Wewe sio kiongozi kwa sababu kuna watu wanakuja kwako kuleta kesi wala wewe sio kiongozi kwa sababu kuna kiasi fulani kikubwa cha mshahara unalipwa.

Kiongozi mzuri hushawishi watu kufanya vizuri na kufikia mafanikio. Joh Quincy Adams aliwahi kusema “If your actions insipire others to dream more do more and become more you are a leader”
Kama matendo yako yanawahamasisha watu kufanya zaidi wewe ni kiongozi.

Hii haikuhitaji uwe na watu na watu wanakuja kwako kwako kuleta kesi. Hii inaweza kufanywa na mkulima , mwalimu bodaboda au yeyote. Siku zote nimekuwa nawaambia watu kwamba kila mtu ni kiongizi tangu kuzaliwa kwake. Kama wewe unaweza kuamka asubuhi na kupangikia mipango yako jinsi itavyoonda na kujiwwkea ratiba nzuri na kuifuata basi wewe ni kiongozi. Kama wewe hauna mtazamo wa kushawishi watu kufanya vizuri zaidi katika shughuli zao basi wewe ni mfuasi.
Hata kama utakuwa na cheo cha uongozi watu hawataweza kukufuata kwa sababu wanaona matendo yako hayaendani na kile unachosema.

Kiongozi wa ngazi ya juu ambaye muda wote amejifungia hataki kuongea na watu wala hataki kuwa karibu na watu basi huyo sio kiongozi ni mfuasi.

Lakini swali la msingi la kujiuliza
Je wewe ni kiongozi au mfuasi?
Ili kujua kama wewe ni kiongozi  unahitaji kujiuliza mwenyewe maswali yafuatayo na kuyapatia ufumbuzi fikria kwa umakini utakapokuwa unajibu kila swali.

Je unafanya kazi kwa mazoea au kwa viwango?
Mfuasi hufanya kazi aliyopangiwa tu , amemaliza. Haijalishi yuko vizuri kiasi gani katika kazi ile ila yeye anachojalai ni kuangalia kama amefanya kazi alioyopaswa kufanya na ameimaliza baasi. Kwa upande mwingine kiongozi huwa hazuiwi na na kanuni na taratibu za kazi ambapo huwa yuko huru kufikria ni kwa jinsi gani anaweza kuiboresha kazi hivyo na kuifanya kuwa bora zaidi. Viongozi huona wajibu wao ni kuongeza thamani katika kile ambacho wanafanya na huiongeza pale wanapopata nafasi.

Soma zaid hapa; Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo

Unajiamini?
 Wafuasi huona watu wenye vipaji na mafanikio kama tishio kwao. Viongozi huona hiyo kama fursa na kuichukua kama raslimali. Viongozi siku zote hujisikia kusaidia  na watatafuta msaada popote pale wanapoweza kuutafuta. Kiukweli viongozi ni viungo muhimu sana wa timu ya mpira miguu.
Hawaogopi kusema kwamba wanahitaji watu wengine ili waweze kufanikiwa.

Soma zaidi hapa; Hii Ndiyo Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo

Je unaona nini?
Wafuasi huona vikwazo na kushindwa katika kazi wazifanyazo. Viongozi huona fursa katika kila kitu. Mambo yanapokwenda vibaya viongozi hawatulii na kuanza kuwazia matatizo yaliyojitokeza bali viongozi hutafuta suluhu.

Je uko tayari kubadilika?
Wafuasi wanatafuta sehemu ambayo ni salama na hawataki kubadilika siku zote. Wanaona mabadiliko kama usumbufu. Viongozi ni watu wanaopenda kuona mambo yanabadilika kila siku. Lakini huwa hawasiti kuuliza kipi kinafuata?.

Je unafanya maamuzi gani?
Wafuasi siku zote huwa wanaogopa kuanza kwa kuogopa kwamba watafanya kitu kibaya. Hawana uhakika kama wao ni watu sahihi. Viongozi hawaogopi kuanzisha kitu kipya hata kama hawana uhakika kama kitaleta mafanikio au la!

Je uko tayari kulaumiwa?
Makosa yanapotokea wagu wa kwanza kulaumu ni wafuasi.
Kwa upande wa pili wa shilingi viongozi wako tayari kulaumiwa kwa matendo yao.
Hawaogopi kwamba kufanya kosa kutawashusha hadhi.  Wanajua kwamba wakiyafanyia kazi malalamiko yao basi watakuwa wameoiga hatua.

Je wewe ni mnyenyekevu?
Wafuasi huwa ni watu wa majigambo hasa pale anapofanya kitu fulani vizuri sana. Wanalazimisha watu kufanya kazi ambazo zinapaswa kufanywa na wao.  Viongozi ni wanyenyekevu hata kama kafikia mafanikio makubwa kiasi gani lakini bado huwa wanasongambele bila kujigamba. Kiongozi akiona kitu fulani anaweza kukifanya basi huwa halazimishi mtu kukifanya, bali atakifanya mwenyewe.

Je una hamasa kutoka ndani?
Wafuasi siku zote wanahamasishwa na vitu kutoka nje kama kupandishwa cheo na kupandishiwa mshahara.
Viongozi hawafanyi kazi kwa sababu ya mshahara au vyeo. Wana hamasa ya kufanikiwa na ndivyo walivyo. Viongozi wa kweli wanasongambele hata kama hawalipwi.

Je staa wa maisha yako ni nani?
Wafuasi huangalia ni kitu gani wanaweza kufikia binafsi na huchukia watu wengine wanapofikia mafanikio. Wanatmia muda mwingi kufuatilia nani anatoka na nani na wanafanya nini? Na mahusiano yao yakoje?
Fulani amevaaje?  Na je kaposti nini kwenye mtandao ya kijamii.?
Viongozi wanatumia muda mwingi kujitafakari wao wenyewe.  Kujiuliza je, mipango yao ya siku imetimia? Je ni wapi warekejebishe?  Wanahitaji nini ili kufikia mafanikio?

Soma zaidi hapa; Hili Ni Kosa Ambalo Watumiaji Wengi Wa   Kijamii Hufanya


Je upo tayari kujifunza?
Wafuasi sio watu wa kujifunza mambo mapya.  Akimaliza shule anajua amemaliza kila kitu na anajua hana kitu cha ziada cha kuendelea kujifunza. Anafikiri amemaliza na anajua kila kitu!
Lakini kiongozi anajua lazima ailishe akili yake kila siku kama ambavyo anavyoilisha tumbo lake.

Soma zaidi hapa; Huu Ndio Ujumbe aluouandika Raisi Wa Marekani.

Je, shule na maisha vinaendana?

Chukua hatua sasa badilika sasa na muda ni sasa na songambele
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii
Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalimu kutoka SONGAMBELE BONYEZA NA UJAZE FOMU
 Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X