Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG karibu sana katika makala ya leo ambapo tunaenda kuangalia chakula ambacho kila mtu anahitaji kupata kila siku. Naamini kitabadilisha maisha yetu na kutupeleka kwenye sehemu ya juu zaidi kimafanikio.
Mara nyingi tunapozungumuzia chakula wengi wetu kinachokuja akilini mwetu ni vitu kama wali, ugali, kachumbari n.k. Ndio hujakosea rafiki lakini kumbuka kwamba kuna vyakula vingine ambavyo unaweza kujilisha mwenyewe ili ukue zaidi na kuendelea na vyakula hivi sio kama hivyo nilivyovitaja hapo juu bali ni vyakula ambavyo vinaendana na kile ambacho wewe binafsi unafanya au unataka kuwa. Chakula kinaweza kuwa ni cha mwili, roho lakini pia na akili. Kwa leo ningependa tuzungumzie zaidi chakula cha akili. Chakula ndicho kitakachotuambia wewe unataka kwenda wapi, chakula hiki kidogo ni tofauti na chakula cha kawaida, kwa mfano kama unataka kuwa mchezaji bora, chakula unachohitaji ni mazoezi ya kutosha ili uweze kufikia hatua ya uandishi bora. Kama wewe unataka kuwa mwanariadha chakula kikubwa unachokihitaji ni kufanya mazoezi ya kukimbia. Kama unataka kuwa mwandishi chakula kikubwa unachokihitaji ni kuandika kila siku. Hiki ni chakula cha kimwili zaidi. Ambacho lengo lake ni kukupatia ujuzi ingawa bado kinahitaji kutumia akili.
Je, wewe unataka kuwa nani? Chakula kikubwa unachohitaji ni kipi?
Soma zaidi hapa; Hili Ndilo Duka Lako Lenye Kila Kitu
Kuna chakula kimoja ambacho kila mtu anayefanya kazi yeyote, au anayetaka kuwa chochote na kufikia hatua njema ya kimfanikio. Ndio chakula kimoja kinahitajika. Chakula hiki ni kukuza akili yetu. Tofauti kubwa iliyopo kati ya binadamu na wanyama wengine ni akili. Tofauti na hapo kiumbe hicho hatuwezi kukiita binadamu labda tutakiita nguruwe au mbuzi. Akili ya binadamu ni kitu kikubwa sana ambacho sisi kama binadamu tunapaswa kukitumia kwa kwa weredi wa hali ya juu sana. Inasemekana mpaka sasa hivi binadamu anatumia chini ya asilimia kumi ya ubongo wake. Yaani mambo yote ambayo binadamu anafanya na maendeleo aliyofikia yote ni matokeo ya matumizi ya akili yetu ila chini ya kiwango cha asilimia 10.
Muda mwingi binadamu anautumia kufikria na kuogopa mambo ambayo hayawezi kutokea. 40% ya vitu anavyoogopa binadamu havitakuja kutokea. Na hii ni kweli ebu ifikrie tena rafiki . umeona ee. 30% ya vitu anavyoogopa vimeshatokea na haviwezi kutokea tena. 12% ni uoga usio na maana juu ya afya zetu. 10% ni uoga wa vitu ambavyo havipo. 8% ndio uoga halisi. Sasa nahisi unajua kwa nini binadamu wanatumia chini ya asilimia kumi ya ubongo wake.
Kitu pekee katika dunia ambacho kinaweza kukufikisha kwenye ndoto yako ni akili yako.
Soma zaidi hapa; Hii ndiyo maabara ambayo kila mtu anayo
Akili yako unailisha nini rafiki?
Kama nilivyosema mwanzoni mwa makala hii kwamba kitu ambacho kila mtu anyaefanya kazi yeyote au shughuli yeyote anahitaji ni kuilisha akili yako. Anza sasa kuilisha akili yako mambo mazuri. Wataalamu wanasema kile ambacho unalisha akili yako dakika sitini baada ya kuamka ndicho kitakachokupa mwelekeo wa siju yako.
1. Anza siku yako kwa kusoma kitabu cha kuelimisha au makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu kama songambele blog.
2. Anza siku yako kwa kusoma malengo yako uliyojiwekea na andika walau mambo matano ambayo utayatimiza ndani ya siku husika.
Soma zaidi hapa; Huu Ndio Ujumbe Aliouandika Raisi W Marekanu
Usipendelee sana kufuatilia na kusikiliza habari hasi hizi zitaathiri na kukuharibia mwelekeo wa siku yako.
1. Usijijengee utaratibu wa kusikiliza taarifa ya habari au matukio asubuhi baada ya kuamka. Taarifa nyingi zinzokutwa kwenye vyombo vya habari zinakuwa hasi, za kuogogya na zisizojenga.
2. Usiitembelee makundi au kurasa za mitandao ya kijamii ambazo zinatoa habari hasi, bali tembelea makundi yanayoelimisha na kuhamasisha kama kundi la SONGA MBELE LA WASAPU
Unaweza kubonyeza hapo kujiunga.
Hakikisha kile unachokisikia, unachokisoma, au unachokiongea saa moja baada ya kuamka ni cha kujenga sio cha kubomoa.
Ili upate makala maarumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA