Mbinu Za Kukusaidia Kufikia Ndoto Yako Kabla Mwaka Haujaisha


Habari za leo ndugu yangu na rafiki yangu.  Leo ni siku nyingine mpya ambapo kama kawaida yetu tunaenda kuitumia siku ya leo vizuri katika kuongeza maarifa na kufanya kazi zetu vizuri ili kuweza kufikia mafanikio.

Leo pia ni siku ambayo tumeuanza mwezi mpya na mwaka wetu unakaribia ukingoni. Swali la kujiuliza Je, mipango yako uliyoiweka mwanzoni mwa mwaka umeitimiza kwa asilimia ngapi sasa?
Ni kawaida sana kila mwaka mpya unapoanza kika mtu huwa ana mipango mingi sana ambayo buwa anapenda kuitimiza mwishoni mwa mwaka lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo, mipango mingi ya inavyozidi kukwama huku mingine ikikamilika nusu.
Je, wewe ya kwako umeitimiza kwa kiasi gani? Au hukuwa na mpango kabisa kama hukuwa na mpango bonyeza hapa
Kama bado hujaitimiza usikate tamaa, huu ndio muda muafaka wa kutimiza mipango yako. Leo hii nakupa mbinu ambazo zitakuwezesha kufikia na kukusaidia kufikia malengo yako ya mwaka huu.

Soma zaidi hapa; Mbinu Muhimu Za Kujenga Mafanikio Katika Biashara

Chagua lengo lako moja la kubwa sana.
Ni imani yangu utakuwa na malengo mengi sana umeyapanga ambayo unataka yatimie mwaka huu, lakini kati ya hayo una lengo moja kubwa sana kuliko yote. Je, hilo ni lipi?
Sasa liwekee lengo lako kuu malengo madogo madogo ambayo utakuwa ukiyakamilisha hatua kwa hatua.
Likamilishe lengo dogo moja baada ya jingine na furahia kila hatua unayoiipiga.

Soma hapa; Yafahamu Mambo Manne Ambayo Huwezi Kujifunza Shuleni

Jisemee kila siku ambavyo ungependa kuwa kabla ya januari.
Bila shaka mpango wako ungependa ukamikike kabla ya januari na ndio maana unaendelea kusoma makala hii. Ungependa kuona mabadiliko makubwa mwishoni mwa mwaka huu.
Moja ya mbinu ambayo inatumiwa na watu wakiofikia mafanikio ni kujisemea mwenyewe kila siku juu ya kile ambacho ungependa kuwa au ungependa kufikia. Yaani yale mafanikio ambayo ungependa kuyaona kabla ya mwaka kesho, jijengee utaratibu wa kurudia na kujisemea juu ya kile ambacho ungependa kuwa.
Yaone mafanikio katika mtazamo wako.
Sasa kwa nini nasema ujisemee mwenyewe kila siku amaneno juu ya yale ambayo ungependa kuyaona au kuyafukia?
Kila kitu huanza na wazo. Lakini wazo bila kuwekwa matendo haliwezi kukamilika.
Mawazo yote katika akili ya binadamu huanzia kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa AUTO SUGGESTION.
Auto-suggestion ni kisima kizuri cha mawzo ya kila aina. Humu ndimo huzaliwa mawazo yote yaani mazuri na mabaya. Lakini uwepo tu wa mawazo haumaanishi kitu ndo kinakuwepo unahitaji kujisemea juu ya jambo fulani mara kwa mara ili liwe sehemu ya maisha yako na kuvutia mafanikio.
Mawazo yote yanayotoka kwenye auto suggestion huingia kwenye SUB CONSIOUS MIND. Lakini sio kwamba yanaingia moja kwa moja, bali huingia taratibu kutokana na kile ambacho wewe unajisemea mara kwa mara. Kama una lengo la kuwa mwandishi mzuri basi jisemee hilo jambo kila siku kwamba nataka niwe mwandishi mzuri sana. Fanya mazoezi ya uandishi. Kile kitu kinachotawala akili yako kwa muda mwingi sana ndicho utakuja kuwa. Je, wewe kitu gani kinatawala muda wako mwingi?

Soma zaidi hapa; Jinsi Ya Kuepuka Kujiua Mweyewe Kiakili

Kuwa na imani kila kitu kitakuwa kama unavyotaka.
Imani ni kitu cha msingi sana katika kazi au shughuli zote unazozifanya. Ukiamini kwamba utapoteza umepoteza
Ebu soma shairi hili kwa umakini

Kama unafikiria umepigwa,umepigwa
Kama unafikiri umeshindwa,umeshindwa
Kama unafikiri huwezi,huwezi
Kama unataka kushinda lakini unafikiri huwezi,karbia huwezi.

Kama unafikiri utapoteza,umepotea
Kwa sababu katika dunia ushindi unaanza na msukumo wa ndani ya mtu,
Hiyo inaitwa hali ya akili.(state of mind).
Kama unafikiri umepitwa na wakati,umepitwa
Inabidi ufikiri mbali kujiinua
Inabdi ujiamini mwenyewe kabla ya kushinda tuzo.

Kumbe imani ndio msingi mkubwa katika kufikia mafanikio.

Kwa bahati mbaya watu wengi sana wameshindwa kueleza ni kwa jinsi gani mtu unakuwa na imani maana ni vigumu kuelezea hili suala kama ilivyo vigumu kumweleza kipofu rangi nyekundu inavyofanana.
Lakini mojawapo ya mbinu ya  kuwa na imani juu ya jambo fulani imeelezwa kwenye pointi namba mbili hapo juu. Kama hukumbuki namba mbili inasemaje rudi hapo juu ukaisome tena.
Kadri unavyorudia rudia jambo linakujengea imani kwamba utaweza kulifanya na utafanikiwa tena sana.

Anza sasa kuutekeleza mpango wako.
Watu wengi wamekuwa wakijifariji kwa maneno matamu kwamba kesho wataweza kufanikisha jambo fulani, na kulifikia bila tatizo lolote.
Kiukweli kesho huwa haiji na vigumu sana kuifukia.
Siku zote muda wa wewe kuanza jambo lolote ni sasa. Kesho huwa haiji
Usiruhusu hali ya kushindwa ikukataze kuendelea na safari yako ya mafanikio.
Ebu badilika sasa,anza sasa, muda ni sasa hujachelewa hata kidogo kiasi cha kutoanza.

Nakutakia safari njema sana ya mafanikio na ninakusihi usikose kusoma makala zote ambazo zimewekewa soma zaidi hapa, maana zina maarifa zaidi yanayohusiana na mada ya leo.

Usikose pia kujiunga na mfumo wetu wakupokea makala nzuri kwa njia ya e-mail kila wiki kwa kujiunga hapa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.


Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X