Huu Ndio Ujumbe Aliouandika Raisi Wa Marekani


Habari za leo rafiki na ndugu yangu ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua za kufikia mafanikio na karibu sana katika makala yetu ya leo.

Katika makala yetu ya leo tunaenda kuona ujumbe mzuri ambao tunaweza kuupata kutoka kwa raisi wa Marekani  Mheshimiwa Donald Trump. Ujumbe huu ameuandika katika vitabu vyake vingi sana vikiwemo vitabu vya art of the deal  na think like a champion


Umuhimu wa kujifunza. Donald Trump anaamini kwamba kila siku ni siku mpya inayokuja kwenye maisha ya mtu lazima mwanadamu aitumie siku hiyo kusaka na kutafuta maarifa mapya. Anasisitiza kwa kina kujifunza kwa watu na kuwa tayari sana kujifunza kutoka kwa watu, kuwa tayari kupokea mabadiliko mapya na kupokea ushauri wa watu wengine. Anasisitiza kwamba ukiwa makini kwa kile ambacho kinachokuzunguka hapo ndipo unaweza kupata wazo bora la kibiashara.

Soma zaidi hapa. Hii Ni Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo

Umuhimu wa kufanya kazi. Donald Trump anasema kwamba alipogundua kwamba dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana basi aliamua kuongeza mda wa kufanya kazi. Hii inaonesha kwamba na sisi inatupasa kubadilika kwa kasi kubwa sana kadri ya mabadiliko yanyotokea kwenye jamii zetu na mazingira yaliyoyuzunguka.
Anaendelea kusisitiza kwamba hakuna mafanikio bila gharama. Kama kuna chochote kikubwa unataka kwenye maisha yako jua gharama ambayo unapaswa kutoa.

Hekima imo kwenye vitabu. Donald Trump anasisitiza sana kuhusu kusoma vitabu. Anamtaka kila mtu ajijengee utaratibu wa kusoma vitabu kila siku bila kukoma.  Anaendelea kusema kwamba kama unahitaji busara wewe soma vitabu tu na busara zitakuja tu.

Soma zaidi hapa Faida Sita Za Kusoma Vitabu Na Makala Za Kuelimisha

Ushindi ni kupiga hatua ya ziada. Washindi ni watu ambao hutumia mda wao mwingi kujiandaa kuhusu jambo fulani. Mshindi ni mtu ambaye anajifunza kwa watu wengine.
Na mshindi ni mtu ambaye anaonyesha ujuzi wa hali ya juu katika jambo fulani.  Trump anataka kila mtu awe mshindi katika hatua anayoipiga. Lakini anaendelea kusema kwamba kushindwa ni kitu ambacho kila mtu amekutana nacho mara nyingi sana. Mshindi yeyote ameanguka mara nyingi sana. Lakini hakukata tamaa wala kushindwa hakujamfanya aache kile alichokuwa anataka kufanya.  Mshindi lazima aende hatua zaidi na kusongambele.

Katika suala zima la ushindi anaishia kwa kusema siku zote hakuna njia ambayo imenyooka katika kufikia mafanikio. Siku zote njia ya mafanikio ni njia ambayo imepinda na yenye utata mwingi sana.

Hayo ndio mambo baadhi ambayo nimeweza kukuchambulia kwa leo katika kile alichokiandika raisi wa marekani. Unaweza kusoma mengine zaidi kwa kujipakulia vitabu vyake viwili ambavyo nimeviweka hapo juu

Endelea kusoma makla za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.

Kujiunga na mfumo wetu maarumu wa kupokea makala maalumu za kila wiki kutoka songambele BOYEZA HAPA NA KUJIUNGA NA UJAZE FOMU HII

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755847391
Asante.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X