Hii ndiyo Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo


Habari za leo ndugu yangu na rafiki yangu, ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua za kufikia mafanikio. Leo hii tunaenda kuangalia maabara pekee ambayo kila binadamu anayo, kila sehemu na anaweza kutembea nayo popote pale aendepo

Maabara ni sehemu ambapo wanasayansi hufanya majaribio ya kusanyansi. Hivyo maabara ipo kwa ajili ya watu kufanya utafiti na kutoa majibu juu ya utafiti huo. Wengi wamezoea kwamba maabara
nyingi ziko mashuleni, vyuoni, mahospitalini au viwandani. Lakini kumbe hii sio kweli.

Soma zaidi hapa; Ufahamu Uovu Wa Lazima Kwenye Maisha Yako

Unahitaji Kufanya Haya Kila Siku

Kila mtu ana maabara ambayo imemzunguka kila sehemu alipo na akiitumia vizuri basi hiyo maabara itamsaidia sana.

Kumbe tayari unayo maabara iliyokuzunguka na unaweza kufanya kazi humo na kujifunza sana. Hii maabara inakupa mfano wa kila kitu unachotaka. Yaani, maabara hii ina kila aina ya kifaa. Maabara hii itakufanya ujifunze sana kama utakuwa tayari na unaweza kuitumia bila gharama wala bila kodi.

Wewe kama mtafiti unahitahi kufanya na kufuata mbinu ambazo wanasayansi hutumia ili juweza kufikia matokeo bora.

Soma zaidi hapa; Je, Wajua Kwamba Mlango Mmoja Ukifungwa, Milango Saba Inafunguliwa

Unahitaji Kufanya Haya Kila Siku

Je maabara yenyewe ni ipi?
Maabara yenyewe ni binadamu, kila mtu anao binadamu ambao wamemzunguka wenye tabia tofauti tofauti. Unaweza kujifunza kutokana na tabia za watu ambazo ni za kila aina na kuamua ufanye nini kizuri zaidi ili uweze kufikia mafanikio.
Inashangaza sana watu hawataki kufanya utafiti na kuitumia hii maabara ambayo ni ya kipekee sana ambayo kila mtu amepewa bure.

Soma zaidi hapa: Ufahamu Uovu Wa Lazima Kwenye Maisha Yako

Mbinu Muhimu Za Kujenga MafanikionKatika Biashara
Anza sasa kuitumia maabara hii ili uweze kujifunza zaidi

Hivi ndivyo jinsi unavyoweza kuitumia

1. Kuitumia moja kwa moja
Hii ni pale unapoamua kuuliza watu wamewezaje kufanya jambo fulani na kufaniikiwa. Sikiliza majibu yao na uyaangalie ni yapi yanakufaa. Yachukue yanayokufaa na uyafanyie kazi.

2. Kujifunza kwa kuangalia.
Ni pale unapoamua kuangalia watu wengine wanafanyaje na kuamua kuiga mbinu na taratibu zao nzuri wanazofanya.

Unapoamua kujifunza kutoka kwa wengine tafadhari hakikisha unajifunza yale yatakayokufikisha kwenye mafanikio. Narudia tena hakikisha unajifunza yale yaatakayokufukisha kwenye mafanikio. 

Kabla hujatumia mbinu yoyote kati ya hizo  mbili kwanza angalia ni mbinu gani itakufaa zadi na itumie hiyo. Baada ya kuitumia angalia je  inaleta matokeo fulani yaliyotegemewa. Na kama haileti kwa nini?
Kumbuka hakuna mafanikio yanayokuja kwa siku moja. Hivyo angalia ni wapi unakosea ili uendelee kusongambele

Endelea kusoma  makala za kuelimisha na kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maarumu kila wiki bonyeza HAPA

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


5 responses to “Hii ndiyo Maabara Pekee Ambayo Kila Mtu Anayo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X