Zifahamu njia za Kufanya Pesa Ikufanyie kazi


Tofauti kubwa sana kati ya matajiri na maskini ni kwamba matajiri hutengeneza faida na maskini hutumia faida. Ni muhimu sana kufahamu kwamba hela ni kifaa ambacho kinaweza kukusaidia kufikia malengo yako. Ili wewe uweze kufikia uhuru wa kiuchumi unahitaji  kuanza kuitumia pesa ikutengenezee pesa sio wewe ufanye kazi ili upate pesa.

Hapa kuna baadhi ya mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuanza kuitumia pesa ikutengenezee pesa. Zinaweza pia kukusaidia kuanza kuondoa matumizi mabaya ya pesa.
Na kama utazifuata vizuri utaanza kuwa na hela nzuri ikiyowekwa kwenye akiba yako kwa ajili ya matumizi yako ya badae.
1.Bajeti.
Moja ya mbinu za kubadili mbinu zako za kutumia pesa ni kuwa na bajeti. Unapoweka bajeti unaamua pesa ikufanyie nini, sio unanunua kila kitu kinachokuja mbele yako. Kwa hiyo unakuwa na uwezo wa  kuamuru kila senti kwenye mfuko wako iende wapi na itumike kufanya nini?
Bajeti yako ni kifaa kikubwa ulichonacho kwa ajili ya ya kuendeshea kipato  chako. Bajeti inakupa uwezo mkubwa na inakuruhusu kufanya maamuzi kila mwanzoni mwa mwezi.
Ukiweza kuweka bajeti na kuifuata  utakuwa umepiga hatua kubwa na itakusaidia kuepuka madeni.
Kama kweli unataka kubadili mwonekano wako wa kipesa, bajeti ni kitu muhimu sana na inabidi iwe hatua ya kwanza wewe kuchukua.
Watu wengi huweza kutengeneza bajeti na kuacha kuifuata baada ya mda mfupi au kuacha kuifuata baada ya mwezi. Unahitaji kutengeza bajeti kila mwezi na kuhakikisha unaifuata. Ni muhimu sana kujijengea utaratibu wa kutumia kidogo zaidi ya kile unachoingiza. Unapoweka bajeti mwanzoni mwa mwezi unaweza kuamua vitu gani ni kipaumbele na uvifanye kwanza ili kuweza kufikia malengo yako.
2.Weka akiba.
Baada ya wewe kujiwekea utaratibu wa kuwa na bajeti ya kila mwezi, basi sasa bila shaka kuna kiasi fulani cha pesa ambacho kitabaki baada ya wewe kuweka bajeti. Kiasi hiki kitunze wala usikiguse. Ukiweza kuweka akiba baada ya mda fulani kiasi cha akiba kitakuwa kimeongezeka. Sasa unaweza kukitumia kiasi hiki katika kununua rasilimali, ili uongeze kipato chako kikue zaidi na zaidi hapa utakuwa umeanza kuitumia pesa, kutengeneza pesa
Hizi mbinu anaweza kuzitumia mtu yeyote, uwe umeajiriwa, umejiari hata kama wewe ni mwanafunzi .
Ni mimi ndugu yako 
Godius Rweyongeza 
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante 
.Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X