Habari za leo ndugu msomaji wa SONGA MBEL ni imani yangu unaendelea vyema katika hatua za kuelekea mafanikio.
Leo tunaenda kuona jambo moja la lazima katika maisha yetu ambalo haliepukiki. Jambo hili ni kufikiri.
Kufikiri ni uovu usioepukika katika maisha yetu. Tunafanya hivyo mda wote, kila siku. Wanasayansi wanasema hatuachi kufikiri mda wote. Hata kama tumelala bado kuna mawazo yanayozunguka ndani yetu.
Kiufupi ni kwamba binadamu anaweza kuongea maneno 150 hadi 200 kwa dakika.Ana uwezo wa kufikiri maneno 1300 mpaka 1800 kwa dakika. (Lakini pia ana uwezo wa kusoma maneno 200 mpaka400) kwa dakika. Hii inaweza kueleza ni kwa jinsi gani akili yetu ina uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kufanya mambo makubwa.
Kufikiri hakuepukiki.Kukwepa kufikiri ni sawa na goli kipa kukwepa mpira, Atafungwa tu.
Sasa kufikiri ni nini?
Kufikiri ni kutoa mawazo akilini mwetu. Huku ni kujiongelea nafsini mwetu, Mara nyingi haifanyiki kwa sauti. Kila mtu anaweza kufikiri hasi au chanya.
Kwa binadamu mawazo hasi ndio mara nyingi hutawala akilini mwa mtu. Na mtu unakuwa jinsi ulivyo kwa sababu ya jinsi unavyofikiri. Ukifikiri mambo ambayo ni hasi basi utakuwa vivyo hivyo. Ukifikiri chanya utakuwa vivyo hivyo.
Mfano:
Ukifikiri jambo fulani huliwezi hutakuja kuliweza. Hii ni kwa sababu kile kitu ambacho akili yako hujisemea, ndicho unachokuwa.
Lakini pia ni muhimu kwa ligha ambazo tunazitumia kwa watoto. Akili zao zipo katika hatua za ukuaji. Wakati wapo katika hatua za ukuaji wana imani na kila kitu wanachosikia. Kama mtu atawaambia ni wazembe au wajinga au hawataweza kupata chochote maishani. Watachukulia ni ukweli hata kama wakikua, Itakua vigumu kuondoa ile hali ambayo ilipandikizwa wakati wa utoto. Ni kweli kwamba inabdi wakosolewe wanapokosea ila isiwe katika hali ya kudhalilisha na kuingiza hali ya kufikiri hasi.
Kumbuka mambo yote katika akili huanzia kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa SUB-CONSIOUS. Hiki ndicho kiwanda ambacho huzalisha mawazo yote. Kama utatumia vizuri hiki kiwanda basi utafikia mafanikio makubwa sana maishani. Hakuna sehemu nyingine yanapozalishwa mawazo tofauti na subconsious mind.
Muhimu: Anza kufikiri chanya. Jisemee mawazo chanya mda wote.Jijengee utaratibu wa kujisemea na kujikumbusha yale ambayo unataka kuyafanya kila siku. Jisemee maneno kama haya; nawezaje kukipata hicho? Ntafanya nini ili niweze kufika huko? Nahitaji nini ili niweze kufanikiwa?
Ukijiwekea utaratibu kama huo utaweza kujijengea hali ya kufikiri taratibu kukuza uwezo wako wa kufikiri taratibu.
Anza sasa kufanya hivyo.
Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza.
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante
Endelea kusoma blogu hii kwa makala zaidi za kuelimisha na kuhamasisha.